NAJUTA SANA: Nilizaa nje ya ndoa, mke wangu haniamini tena. Natamani siku zirudi nyuma

Naona tujitahd kuruk sarakas ILA kuzaa nje na mkewako anazaa vzr ni Hatar

Bora ungekuw nae kabla


ILA WANAUME tunawez tegewa
 
Wewe na kiherehere chako , we uliwaona madingi wanaoficha siri watoto wanakuja tambulishwa siku ya msiba wao ni wajinga eeh???......we ulitakiwa upige kimyaaaa heri ya kufa leo Bora ufe kesho...angalau ungesubiri mkeo walau akue apate busara flani za kiutuuzima....ndo hvo tena mzee ushaharibu. Kwanza ni dharau sana eti unaenda kumwambia mkeo nimezaa nje kwa gia eti unaomba msamaha.....
 
Mkuu ukisoma vizuri ilo swala nilishafikisha mpaka kwa viongozi wa dini , walinishauri mengi sana ikiwepo na hayo uiliyosema na nilishayafanya
 
Pole sana ndugu,mke wako yuko sahihi.Kuchepuka ungechepuka lakini usingezaaa huko maana asingejua hivyo asingeumia.Sasa umemdhihirishia kwamba ulichepuka kipindi ambacho alikuwa anateseka ili kuleta kiumbe chako duniani.
 
Mkuu ukisoma vizuri ilo swala nilishafikisha mpaka kwa viongozi wa dini , walinishauri mengi sana ikiwepo na hayo uiliyosema na nilishayafanya
Sisi tunao na bado wake zetu wanatutii! Fanya hivi, muondoe hapo nyumbani huyo mtoto wako akaishi kwa mama yako. Amani itarudi. Unajua mkeo anaumia anapomuona huyo mtoto. Na ukichunguza sana hata mnaposex lazima hakojoi.

Pili anza kumspy ili ukimfuma ulianzishe! Hapo itakuwa ndiyo pona yako
 
Mke wako hana akili.
 
Kwanza mtoto ni wako
Mwanao Hana baba mwingine bali niwewe
Mateso ya mkeo ni mateso ya muda mfupi, mwanao anaweza kubadili mateso yako mbeleni ukawa na furaha.

Mpende mwanao, mjali, hakikisha hakosi mahitaji ingawa kuwa makini, nunua nguo za watoto wote, watoe out wote, kama unauwezo mpeleke mtoto boarding ili mkeo as iendelee kumuona hapo kila siku.

Mbembeleze mkeo, mpe zawadi, chukua Mshahara wako mpatie, muombe msamaha Mara kwa mara. Muoneshe mapenzi at asahau na maisha yataendelea
 
Siku zote majuto ni mjukuu na wala siku siku zote zinakwenda mbele wala hazitarudi nyuma hata sekunde. Kubali makosa muendelee au umruhusu naye azae nje uone raha yake
 
Huko mwanzo umeanza vizuri ila paragraph ya mwisho nawe unaonekana wale wale ampe mshahara wake ili iweje?

Hapo dawa ya moto ni moto, ningeendeleza ubinafsi kama anavyofanya huyo mwanamke, sisi ni binadamu tumeumbiwa makosa, for Gods sake kama hamna mapenzi waachane, siyo mmoja anajaribu kutengeneza mwingine ana block jitihada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…