NAJUTA SANA: Nilizaa nje ya ndoa, mke wangu haniamini tena. Natamani siku zirudi nyuma

Naona mnajaribu kumpa moyo mwenzenu kuwa ni kawaida. Yes ni kawaida, lakini SI KWAKE. Dhamiri yake iko hai ndo maana inamshtaki. Na dhamiri ikikushtaki si rahisi mambo yakaenda. Anajiona amelose pakubwa.

Sio siri, as a woman, naelewa huyu mwanamke alichopitia. Unampa mtu ushirikiano wote, unakuwa mwaminifu, unakuwa a wife package na unajitahidi as hard, lakini unapokea surprise yako, inauma.

Ila MUNGU hasinzii wala halali. Anajua unayopitia. Kama alisababisha nyinyi kuwa pamoja, anaweza kurestore that broken home. Mlitakiwa kuwa mahali fulani, na hao watoto wanatakiwa kufikia destiny zao, na shetani ameliona ndo maana anajitahidi kuwatoa kwenye reli.

Rudini msalabani. Hakuna linaloshindikana kwake. Nawaambia ukweli. Muombeni Mungu awafinyange upya, huo moyo uliojeruhiwa utengenezwe upya. God can fix and ammend broken stuff ambazo mwanadamu wala technology haiwezi. Trust in the work of Jesus at the cross. God can do what you can never imagine. Ask HIM to fix your home. Mnayo ndoa nzuri sana, its just a test of time, na mtalishinda hili. Pole sana kwenu wote. Usikosee tena sasa.
 
Sijaona kosa lolote hapo,,yaani nimkane mwanangu kisa mwanamke? Hupaswi kujutia lolote. Labda kama wewe unategemea kipato cha huyo mwanamke kimaisha. Be a man.
Tupo wengi tuna watoto nje,
Cc Equation x
Kuzaa nje si kosa, kosa ni kuendeleza yale mahusiano ya nje; akifikisha miaka 55+ ataona umuhimu wa kuwa na watoto, muhimu ni kuwapa msingi sahihi tu.
 
Tunavoona mitazamo ya wanawake tunajifunza zidi sisi wanaume kwenye hili suala coz we get to see your perspective.
Swali la kizushi, hapo jamaa anasema wife ako na mbanga zake hana time na msela, sasa akianza maombi ya kukemea pepo si ndo atamtema kabisa??
 
Mambo ya rohoni yanaeleweka kwa jinsi ya rohoni. Huyu mwanamke ana majeraha ya moyoni, haya hayaponagi kwa jinsi ya kimwili, only GOD can do this. Unafikiri jamaa anatakiwa kukemea...never, anatakiwa aingie katika program ya toba ya muda mrefu. Ni mwendo wa toba tu.

Kuna mtu kashauri vizuri sana kule juu. Aintergrate both methods. Aanze kama kumtongoza upya mke wake. Aoneshe tena interest na mke wake. Asijifanye anaweza kupambana kwamba yeye ni mwanaume. Kama mke kabeba kisasi atakua anatwanga maji kwenye kinu. Aonyeshe efforts za kuijenga familia yake tena upya. Aapply efforts both kimwili na kiroho. Akifix hapa, michongo itanyooka.

Mwanamke akiwa na kinyongo afu umemkoroga wewe, na anafanya majukumu yake kama kawaida..wewe mwanaume ndo utapata tabu. Mnataka amani tafuteni amani na wake zenu. Hasa kama una mke mzuri Mungu amekupa, kaza fuvu na jione unaweza kufight mwenyewe...utajua hujui.

Kuna kipindi mshua alishampigaga bimkubwa wangu tukio kama hili, maza akagundua mdogo wangu wa nje akiwa na 12 years..basi bimkubwa akawa anaishi na sononeko, heheeeeee...mambo yalipinda nyumbani kwa miaka 10, mpaka mama alipoanza kuitafuta neema ya Kristo na kumsamehe mshua ndo mzee mambo yakawaga sawa sawia. Na kuanzia kipindi kile ndo mpaka leo wako vizuri sana Glory to God. Anayedharau ni sawa..kila mtu ana itikadi zake. Siwezi kumuaminisha mtu.
 
I understand unachosema. But nisaidie kidogo kwenye hili suala la imani, umesema this giy ajae kwenye toba n.k, but hyo yoote ina faida gani kama huyu mwana.ke bado ako na uchingu na kusononeka.?
Wouldn't it be better kama huyo mams pia angeenda kupiga ma toba pia?
 
Kwa nini?
Mwanaume kumletea mtoto ni vizuri zaid kuliko angemletea maradhi.
Mwanamke si mtu wa kuuachilia moyo wake ni mtu wa kubeba vitu moyoni tatizo.

Kutokumshirikisha mume wake kama zamani tayali inaonyesha katengeneza matabaka kwa familia kitu ambacho ni cha kijinga.

Mtu kumkasirikia mume ambae tayali amekiri kosa na kuonyesha kujuta hiyo ni chuki na inamaanisha hajaubeba udhaifu wa mwenzie na kumrekebisha ila alichoamua ndicho kitachokuja kumtesa zaid mbele.

Somo alilopewa na kungwi na mama ake halikumuingia.
 
Ulie zaa nae endelea nae kea mkeo pia atakuwa anapigwa nje kwani kisha kutoa thaman
Agakuthamini siku nawe umemfumania
Ulie zaa nae, nae ni mkeo mpe haki zake pia
Ona mazingira anayo Ishi muone e huruma
Usimdharau kutokana na maisha anayoishi ya uswahilin ndo kipato chake kinamtoshereza kuishi huko, ilimrad sio malaya na wala ajiuzi
Mkeo atajirudj baadae kabisa akiona uteseki
We jioneshe huruma huruma uone cha moto
 
Ni kweli unachokisema mkuu. Lakini sasa mimi ninaemshauri hapa ni huyu kaka. The power of God atakayoipata ndio itakayopelekea na huyu mams afunguke na kusamehe. Yani Mungu huwa anataka hata mmoja katika wanandoa wasimame vizuri na yeye afu aingie hapo kati na kulisababisha.

Sasa kwa story hii, hii nyumba ina ukiwa, ina utupu, upendo wa kwanza umeondoka, usifikiri kutatokea maendeleo humu. Ninao wajomba, baba wadogo, punde walivyofanya mambo ya mfanano huu, na uchumi wa familia ukacollapse. Ninadhani mpaka leo mama na shangazi zangu wana maumivu kwa sabbu uchumi hauko ok katika familia zao. Mke halali wa kiagano, aliyejitahidi kutembea katika ukamilifu, akiumia afu akalazimika kutulia katika ndoa ili kumuheshimu Mungu, uwe na uhakika kisago cha uchumi ni inevitable.

Huyu mleta mada anatumika katika adhabu ya uzinzi. Na hii hali inamletea sonona. Inamuumiza. Ndo maana kaandika. Angekua anaweza kuhimili asingejisumbua kutype. Hakuna jambo swadakta kama kumpata mwandani wa uhakika..first class wife. Anamtaka mke wa ujana wake back, ili maisha yawe mazuri ndani ya nyumba. Mwanamke ndo mwenye maumivu. So kama alivyofanya efforts kutafutana na mcheps, afanye sasa efforts kuutafuta USO WA MUNGU. Naomba nimuache na mstari wa Isaiah 59:1-21.
 
Umemshauri vizuri kweli. Mleta mada naomba usome hapa kwa hatua ili upate suluhisho la mambo yako. Nami nimepata kitu hapa.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Isomwe na michepuko, dada hafai tena wakati alikusitiri, ulivyo na roho ndogo ukijua wife nae ana kamchepu kake au akikubambikia mimba tunakuzika,, pambana na hali yako
Pale michepuko inapojikutaga nani sijui kumbe wanatumika tu kwa starehe ya muda mufupi!!

Kwakweli mtoa mada endelea kua matunda ya matendo yako.
 
Kilichonishangaza una miaka 42 halafu bado huna akili.
Acha kumuita mwenzio hana akili,
Wewe unavyojiona unazo akili,
Kwenye uzi mmoja nakumbuka ulisema ulivyotoka ughaibuni ulizini na wake za watu ambao ni ex zako eti walikuwa na shida na pesa.

Biblia imesema wazi kuishi nao kwa akili sasa wewe umeshindwa kutumia akili.
Biblia yenyewe imesema azinie na mwanamke hana akili,
Yani wewe unafanya unamuona mwenzio hana akili kumbe wewe mwenyewe upo kundi lile lile.

Hahaha binadamu bhana,
Na PHD yako still hata wewe unazini na mwanamke.
 
We miaka 42 lkn huna tofauti na mtoto wa miaka mitano! Hao watoto wa nje hua hatusemagi tunatunza kimya kimya mpaka mke ajue mtoto ana miaka 15 mpaka 20
Huyo hajui kama mapadre wana Watoto kwa siri na wanawahudumia kwa siri.
 
Matatizo ni mawili tu hapo.

1. Kumtegemea mke katika kipato
2. Kuwa vuguvugu na kukosa akili ya mahusiano. (Walokole huwa na hili tatizo)

Suluhisho ni moja tu.
1. Kuwa mwanaume mwenye uwezo wa kujisimamia kifedha na kimsimamo.

Kila la heri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…