Najutia kupata Mke kupitia Facebook.

Najutia kupata Mke kupitia Facebook.

Ni sawa na kununua simu mtaani kariakoo iliyopo ndani ya box na ukalipia bila kufungua box. Unaweza kuta ni simu kweli ila sasa.

Ulioa haraka sana. Shida sio FB, shida ni hukujua unaoa nani.
Hapo shida sio kuoa haraka, shida ni NDOA🤣🤣🤣 Wakiambiwa wasioe hawaelewi,
na Sisi wanandoa tulivyo na roho mbaya hata hatuwaambiii ukweli, michango tunatoa na miuno tunamwaga siku ya harusi.....
 
Hapo shida sio kuoa haraka, shida ni NDOA🤣🤣🤣 Wakiambiwa wasioe hawaelewi,
na Sisi wanandoa tulivyo na roho mbaya hata hatuwaambiii ukweli, michango tunatoa na miuno tunamwaga siku ya harusi.....
Kama ww ni mwanandoa basi bado kupaa na ungo tu. 😄
 
Bora hata wewe ulishamuona live, kuna mwamba aliona jiko facebook huko akatongoza wakakubaliana, binti ni mzenji jamaa kavaa kanzu kapeleka mahari...ubwabwa ukaliwa mwezi uliofata ndoa ikafa kibudu.
Wee jamaa muongo sana 😂😂🤜🏿🤛🏿
 
Huyo ujampata Facebook acha masingizio , alafu Facebook sio kigezo cha kupat mke/mume Bora au asie bora
 
ASilimia kubwa hiz ishu huwa mnaleta hata sio serious.
Huwez ukawa na muda wa kuandika hapa wakati hujui hata nin hatua za kuchukua ku fix issue.

Juz kat nilikutana na sintofaham ndani ya nyumba , na ile katika kuwaza na kuwazua nin cha kufanya ndio likanijia wazo kuwa hiv hawa wanaoandikaga ishu zao private hapa huwa wanapata nguvu wapi.. sio kwamba hakuna muda wa kuandika ila tu reasoning ya kawaida inakataa kabisaa na kujiliwa na mawazo yale ya "niandike THEN WHAT??".. HOW is t going to help resolving the matter???.
"Okay hata kama kanikosea hiv, why should i expose her ?? Hata kama hawamjui, wapo wanaonijua mimi, why should i embarrase myself??

Is it ethical?? Huu muda naandika kuhusu yeye na mimi kwann nisiurumie kuzungumza nae kuhusi hili suala??

Nika conclude hapa jukwaan mostly zinakuja chai.. au ukiona hivyo basi ni memory ya muda mrefu sana ambayo ilishapatiwa ufumbuz ila tu mtu anajaribu ku share experience like how would people have reacted if they were in his/her position...
 
Mimi nilioa mke niliyesoma nae tangu primary….nilipata muda wa kumsoma….kuoa mtu hata miez3 bado ni kutafuta matatzo
 
Madem wa fb wengi Wana njaa , usiwaamini kupitiliza .
Nakumbuka kuna mmoja altaka kulichapa tukio kimasihara nikamshtukia
 
Tatizo ni facebook au ni wewe ulikurupuka mwendo wa ngiri mkia juu jombaa? Facebook ni platform ina kila aina ya kitu, play your cards wisely!
 
Mke kumpaa talaka hiyo ni hiyari yako, Madhali anakupenda kumuacha ujinga wako..........
 
Mnamo mwaka X weds nakumbuka nilibahatika kukutana na huyu bint uso kwa uso katika Phase flan katika kutafuta maisha.
Tulipoteana tena kama baada ya mwaka mmoja bila kutongozana kuzoeana wala bila kuongea neno lolote.
Dada huyu alikuwa mzuri kwa Sura na rangi nzuri.
Maisha kusonga tukiwa tumepoteana niko kwa online Facebook ndipo nikamuona tena akiwa na rangi yake nzuri mcheshi kwenye picha dah.
Kutokana na usingle wangu wakitambo nikamtongoza Facebook bhanaa nika mpa ahadi kuwa lazima nitakuoa.
Mwamba nikapata vijicent vyangu vya mahari nikaenda kwao chap nikavuta chombo ndani.
Yaani bila kukaa kwa uchumba live pasipo hata miezi 3.
Ndugu yenu ninayo pitia kwa sasa heeh.
Nikiorodhesha naweza msimalizie hii thread.
Sasa Age 40+ Sijui dah acha tuone
Bro mbona hakuna shida, mtoto wa kwanza mwite Facebook!
 
if there is no intimacy in your relationship please don't get marriage
"Intimacy is everything"
 
Back
Top Bottom