Wakuu Salaam,
Kama kichwa cha habari kinavyosema,
Niliwahi kuwa na rafiki yangu wa karibu sana,alikuwa sio mgonjwa au sikujua anaumwa. Tulikuwa tukikutana ana tabasamu zaidi ya mimi na muda wote alikuwa anafuraha mpaka mimi alikuwa ananishauri akiniona sina furaha.
Siku moja aliniambia anafikiria kujiua sikushtuka nikamshauri kidogo kama vile ushauri wa vijana, wiki mbili baadaye akajinyonga. Nimekaa na hili jambo muda mrefu sana lakini limegomakutoka kwenye nafsi yangu, sina furaha, najilaumu, ninahisi sikutimiza wajibu wangu sehemu fulani ambayo ukiniuliza ni sehemu ipi siijui lakini ninahisi kama rafiki yake nilifeli kumsaidia.
Huu ni mwaka wa 12 sasa naishi kwa maumivu makali sana na sijui nitajitoaje. Je, kuna mtu alishawahi kuwa katika mazingira kama yangu na alisahau vipi akawa na furaha na amani kama zamani?,Mimi nimeshindwa kutojilaumu! popote ulipo Suleiman Nisamehe!
Kama uliwahi kujutia kitu ambacho unahisi ungekifanya na hukukifanya hebu tirirka hapa tuone msaada unaoweza kupatikana.

Mkuu pole kwa masahibu lakini hongera kwa kuwa tayari kutushirikisha kilicho moyoni mwako.
Ni sawa kabisa wala sio tatizo kuhisi unavyohisi kwa sasa,Wanasema ITS OKAY NOT TO BE OKAY.
Kwa kuwa umetambua ni jambo linalokusumbua na unaendea kufanya juhudi kupata msaada ,Naomba nishauri jambo.
Kuna wadau wa masuala ya Afya ya akili ,Ambao kwa kuwa una nafasi ya kutembelea mitandao ya kijamii unaweza kupata msaada kwa wakati sahihi wanaitwa MENTAL HEALTH TANZANIA,Ukiwasiliana nao kuna uwezekano wa kupatiwa ushauri au msaada wa kifikra wa nini ufanye ili kuendelea na shughuli zako nyingine.
DAR ES SALAAM wako Ubungo karibu na Ubungo Plaza ,mtaa wa National Housing,ukitumia namba hizi utapata maelezo zaidi 0766 501 848.
Wana akaunti Instagram ,Facebook na hata twitter ,Pia kwa sasa wamefungua forum kama ilivyo jamii forum,Lakini yenyewe inahusika na masuala ya Afya ya akili.Search mental health Tanzania forum,Kule kuna majukwaa pia ambayo ukipost mada kama hii ,ni rahisi kuzidi kupata msaada wa kitabibu maana kuna wataalam wako online muda wote kwa ajili ya msaada wa issue kama yako.
Kila mmoja ana mapokeo yake ya namna gani jambo linamuumiza moyoni.Hivyo sio lazima ninavyohisi mimi nawe iwe hivyo kwako.
Usikatae kuwa moyo wako haujahuzunika ili tu ufanane na walio kuzunguka ,Kama mwanaume ikifika wakati una huzuni na unahisia nafsi inakwambia kulia,Unatakiwa kulia tena kwa hisia kwelikweli ,Kufanya hivi ni sehemu ya tiba na kuupa moyo nafasi ya kuendelea kufanya mengine.
Kwa lolote karibu PM.