Najutia tukio hili: Sikuweza kumsaidia rafiki yangu akajinyonga

Najutia tukio hili: Sikuweza kumsaidia rafiki yangu akajinyonga

Mbona tayari dalili zimeanza.
Ndio maana niliwaambia wapuuzi fulani, inawezakuwa jamaa huyu alikukwaza kwa namna moja au nyingine, kitendo cha yeye kufa na bado unamtukana unajitafutia ugonjwa mbaya sana wa majuto.

Kifo ni form nyingine ya maisha ya kiumbe, hatujui labda kinapewa uwezo zaidi ya huu tulio nao,au kinakuja kwa namna tofauti hapa hapa duniani tena.
Wee..kuna dalili.?kwa kina nani hao?
 
Kama alishaamua kujinyonga hata ungefanyaje ni lazima angejimaliza tu !! kifo kikianza kukuita mwanadamu hamna namna!! cha msingi ni kusahau na kama kuna kuonana huko kuzimu basi mtaonana!! isharah - ila kwako wewe maisha lazima yaendelee.
 
Wakuu Salaam,

Kama kichwa cha habari kinavyosema,
Niliwahi kuwa na rafiki yangu wa karibu sana,alikuwa sio mgonjwa au sikujua anaumwa. Tulikuwa tukikutana ana tabasamu zaidi ya mimi na muda wote alikuwa anafuraha mpaka mimi alikuwa ananishauri akiniona sina furaha.

Siku moja aliniambia anafikiria kujiua sikushtuka nikamshauri kidogo kama vile ushauri wa vijana, wiki mbili baadaye akajinyonga. Nimekaa na hili jambo muda mrefu sana lakini limegomakutoka kwenye nafsi yangu, sina furaha, najilaumu, ninahisi sikutimiza wajibu wangu sehemu fulani ambayo ukiniuliza ni sehemu ipi siijui lakini ninahisi kama rafiki yake nilifeli kumsaidia.

Huu ni mwaka wa 12 sasa naishi kwa maumivu makali sana na sijui nitajitoaje. Je, kuna mtu alishawahi kuwa katika mazingira kama yangu na alisahau vipi akawa na furaha na amani kama zamani?,Mimi nimeshindwa kutojilaumu! popote ulipo Suleiman Nisamehe!

Kama uliwahi kujutia kitu ambacho unahisi ungekifanya na hukukifanya hebu tirirka hapa tuone msaada unaoweza kupatikana.
HIVI ALIPOKUAMBIA ANATAKA KUJINYONGA!
ulimuliza au kumhoji kwanini,sababu gani anataka fanya maamuzi hayo

Ova
 
Kifo cha rafiki yako ni mlima.

Huu mlima umeubeba.

Huu mlima unatakiwa kuupanda na kuuvuka.

Am saying stop carrying this mountain, climb it.

Pengine huwezi peke yako, kuna mtu anaweza kukusaidia. Out there there is someone who can help you.

NB. Sikuwahi kujua wewe ni mwanaume.
 
" Guilty Consciousness "
hali hio watakuwa nayo wanamatusi wa humu na kwengineko dhidi ya ushujaa wa kamanda JPM.

Ina nguvu sana hio kitu itawaandama daima kwa matusi walio na wanayo toa kwa Baba yetu JPM ,its hard to escape from it

watajiona wanahusika moja kwa moja na kifo chake kama ilivyo kwako hapo sasa ( Mtakuja kujionea wenyewe )
@Behaviourist msikilize huyu mat..k.oh
 
Wakat wake ulifika mkuu, huna namna ya kujilaum
 
" Guilty Consciousness "
hali hio watakuwa nayo wanamatusi wa humu na kwengineko dhidi ya ushujaa wa kamanda JPM.

Ina nguvu sana hio kitu itawaandama daima kwa matusi walio na wanayo toa kwa Baba yetu JPM ,its hard to escape from it

watajiona wanahusika moja kwa moja na kifo chake kama ilivyo kwako hapo sasa ( Mtakuja kujionea wenyewe )

Ama kwa hakika hayupo chizi ajuaye kuwa yeye ni chizi.

Itoshe kusema: Hiiiiii bagosha!
 
Wakati nipo shule ya msingi kuna siku natoka shule kwenda nyumbani, njiani nikakuta jamaa anapewa kipigo kitakatifu na jamaa wengine wawili. Nikauliza mtu aliyekuwepo eneo la tukio kuna tatizo gani? Akajibu walimkuta jamaa anataka kujitundika ndo wanamwadhibu kwa hilo kosa alilotaka kufanya. Nikashangaa sana kwamba baada ya kile kipigo si ndo ataharakisha zaidi kujiua? Sikuwahi kufuatilia nini kiliendelea ila hadi leo nikipiga hesabu za hatua walizochukua wale ndugu zake nashindwa kuelewa.
 
Hivi yule dogo anaendeleaje?😔 sorry kuuliza hapa
Wangari Mungu amekuwa mwema sana kwetu,anaendelea vizuri sana ana afya njema sana no complains so far.Anahudhuria clinic kuchekiwa after every six months ataend hii june i think.Namshukuru sana Dr Josephine,Mungu amlipe kwa yote aliyotufanyia kama Familia.
 
Wangari Mungu amekuwa mwema sana kwetu,anaendelea vizuri sana ana afya njema sana no complains so far.Anahudhuria clinic kuchekiwa after every six months ataend hii june i think.Namshukuru sana Dr Josephine,Mungu amlipe kwa yote aliyotufanyia kama Familia.
Amen amen ...nimefurahi kusikia hili jamani....! Dah...so lovely..bado yuko kule kule? Alafu alihisg mm mama mdogo😜
 
Mkuu acha tu...nakumbuka miaka ya 90 huko maeneo ya mburahati barafu....kuna mtu alijinyonga, tukaenda kuona, tulivyorudi mmoja wa mdada tulioenda nae alikuwa Nesi....akatoa kauli kuwa "mimi siwezi kujinyonga yani".
Baada miezi kadhaa yule Dada alijiua kwa kujikata koromeo! Inasemekana alikorofishana na shemeji yake...

Kauli yako imenikumbusha huu mkasa...

Ni makosa sana mkuu ACCOUNT, hata kama mtu amekukera kiasi gani lakini kuchukua uwamuzi wa kujitoa uhai sio kwakweri.

Allah atuamrisha katika Qur'an


Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipo kuwa kwa haki. Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa.

Halafu hapo hapo tunasema Mungu amepanga kifo chake, kweli Mungu anataka Mtu ajiuwe kweli!!!! sometimes tunamkosea sana Mungu.
 
Back
Top Bottom