Najutia tukio hili: Sikuweza kumsaidia rafiki yangu akajinyonga

Namba moja!
 
Namba moja!

Kwa hiyo ndugu kedekede ulipewa taarifa kwa ajili ya kuzingatia tu. Ujue tu kwamba jamaa ana mpango wa kujiua. Ila wewe hukuwa na kauli yoyote ya kuidhinisha au kuzuia kujiua. Kwa hiyo kwa sasa wewe umebeba mzigo mzito usiokuhusu, kwa vile hukuwa sehemu ya maamuzi.
 

Uzi rejewa kwenye linki hapo juu unaweza kuwa wa manufaa.
 
Pole sana. Jaribu kusahau kwani sioni kosa lako liko wapi. Nakuhakikishia huna kosa. Kuna story ya mpiga picha wa Africa Kusini ambayo nadhani baadhi wameshaisikia inaitwa ''The vulture and the little Girl''. Huyu mpiga picha alikuwa anapiga picha Sudan kuhusu njaa miaka ya 90. Siku moja akakutana na mtoto aliyedhoofika sana hata kutembea hawezi, anajitahidi kutambaa kwenda kwenye kambi ya kutoa msaada huku ndege mla mizoga akimnyemelea kwa nyuma, ikitokea akifia njiani amle. Ile picha ilileta simanzi sana na mpiga picha alipouzwa hatua alizochukuwa alidai alimfukuza yule ndege mla mizoga. Hili lilifanya watu wengine wamlaumu kwa sababu walisema ilitakiwa pia atoe msaada kwa yule mtoto. Jambo hili lilimuuma sana yule mpiga picha na akaamua kujiua mwaka mmoja baadae.
 
Anaitwa Kevin Carter mkuu!Alijiua 1994 nadhani!
 
Ulithamini mpira kuliko rafiki yako!?
 
Naelewa mkuu lakini "ninge" haiwezi kutoka akilini mwangu!
 
Dah I feel ur pain,pole sana
 
Kubali ulikosea na nisamehe nafsi yako, hii ndio njia ya kutoka hapo ulipo, usipojisamehe itakuandama maisha yako yote
 
Naelewa mkuu lakini "ninge" haiwezi kutoka akilini mwangu!
Kübler-Ross alitoa modeli ya hatua tano za kuomboleza. Kwa modeli hiyo, inawezekana "ninge" zinaashiria hatua ya tatu ya modeli hiyo.

Modeli ya Kübler-Ross inataja hatua tano:

1. Kukanusha (Denial)
2. Hasira (Anger)
3. Kubembeleza (Bargaining)
4. Sononi (Depression)
5. Kukubali (Acceptance)

3. Kubembeleza (Bargaining)
Hapa mtu hutamani hali irudie kama ilivyokuwa hapo kabla.

"Kama ningeongea naye kuhusu kujiua asingejiua."
"Kwa kuwa sikuongea naye kuhusu kujiua mimi ndie niliyesababisha ajiue."
"Ningeweza kurudisha muda nyuma, ningeongea naye kuhusu kujiua."
"Mtu yoyote mwingine akitaja kujiua, nitatenda tofauti na siku ile rafiki aliponiambia."

Ukiona vema, kawaone washauri wa unasihi kwa msaada wa kitaalam.
 
Asante mkuu kwa kunielewesha na kunifariji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…