Ametumia haki kama mpenzi wa siasa... She is smart aliona anakosa majingle na kwa kupanda na kikwete anaweza pata dili za kutumbuiza.... All her cotracts zimefulia sasa anataka kutoka upya
Hongera kwa kutanguliza tumbo, maana hukua na haja ya kurudisha kadi kwenye public... Hukuichukulia kwenye mhadhara
Uamuzi wa Nakaaya - kama msanii wa kizazi kipya - uliwahamasisha Sugu, Mkoloni na wengineo, kuchukua uamuzi huo, lakini tofauti na wao, hawa ni wasanii na wazalendo pia.
Uzalendo ni kujitoa kwa ajili yako. Nakaaya anaweka maslahi yake mbele ya maslahi ya taifa; historia itamhukumu.
Lakini pia, kutokana na umri wake kuwa mdogo, huenda hana uwezo wa kubaini yatakayokuja kutokea siku zijazo. Unahitaji umri kuwa na busara za kionambali. Sugu, Mkoloni na wengine wameliona hili. Hata kama CHADEMA hawatachukua Urais (sidhani JK na wenzake wataridhia hili...), Bunge lijalo SIO la CCM.
Kisanii, ukimweka Nakaaya na Sugu, wafanye onesho la pamoja, utawapata washabiki wengi zaidi wa Sugu kuliko Nakaaya. Na kwa hili alilolifanya jana, kujitakia umaarufu kutamkosesha mauzo sokoni, kama wenzake walio kwenye kampeni tayari. Ndio, watamwingiza kwenye kampeni, ataenda kumpigia debe JK. Sawa, anataka maslahi, yake. Ya taifa? Hana habari nayo, hata kidogo.
Kila la kheri.
-> Mwana wa Haki