Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

Jamanieeee!!!!!!!!!! Tusimfuatefuate huyu dada, alipoamua kuwa msanii kitu alichofikiria ni maslahi yake yeye, na alipoamua kuingia chadema aliangalia pia maslahi, sasa kama hayo maslahi upande wa chadema anaona yatachelewa au kutopatikana kabisa hasa ukichukulia huku kumejaa watu wanao endekeza maslahi ya taifa kwanza, unategemea afanye nini hasa ukichukulia huenda amefuatwa na vigogo kwamba mzee atakupa ukuu wa wilaya au uwakilishi fulani., kama mtoto wa kike yeyote umtongozaye humo barabarani lazima ashoboke tuu. Mimi namtakia kila la kheri huyu dada. Hapa kazi tuu, ilimradi mkono uende kinywani na mguu uingie saloon.
 
Nakaaya Sumari amerudisha kadi ya Chadema jioni ya leo na kumkabidhi JK kwenye mkutano wake ulio fanyika leo mkoani Arusha, JK amempongeza sana kwa kitendo hicho na kumwambia karibu mama CCM ndicho chama pekee Tanzania.

Mkuu Mganyizi, Masahihisho kidogo; Nakaaya hajarudisha kadi ya chadema kwani haikutoka ccm. yeye ameipeleka ccm kadi ya chadema.
 
OOhh Nakaya umepotea watakutumia kama Co....m wakimaliza wanaachana na wewe! Yote maisha kila laheri

Ametumia haki kama mpenzi wa siasa... She is smart aliona anakosa majingle na kwa kupanda na kikwete anaweza pata dili za kutumbuiza.... All her cotracts zimefulia sasa anataka kutoka upya

Hongera kwa kutanguliza tumbo, maana hukua na haja ya kurudisha kadi kwenye public... Hukuichukulia kwenye mhadhara
 
Nakaaya?!!!!! hivi hili jina nalenyewe ni la kutaja katika uwanja wa siasa? hii ni bongo walah!
 
Hivi kwa nini watu hawana misimamo katika maisha.
Mtu hujui unahitaji nini???loh haya i wish her good lucky..:confused2::confused2:
 
hebu tuwekeeni link ya alipokuja kutangazwa kuwa anawania nafasi ya ubunge viti maalum chadema.
 
Jamani haka kasisimizi tu, kaache Kaende, wameondoka kina Kabouru AMANI WARID SEMBUSE huyo mdada, amekua corrupted kama kawaida ya ccm
 
sita sikiliza nyimbo yoyote ya nakaya, na wala sita nunua cd yoyote

mhanjo hizo ni hasira za mkizi, tuko hapa kutafuta mabadiliko tanzania na hao mapambano yoyote hayakosi majeruhi; mwache akatafute riziki yake ccm.
 
Duuu ! Mimi sielewagi kwanini kadi ya ccm upelekeke Chadema na ya Chadema upeleke CCM mbele ya Hadhara hizi tabia za Kununuliwa wazi wazi !
 
Haki ya nani aisee! Hutambui umuhimu wa huyu binti kwa jamii?! Naamini ndiyo maana mnapiga piga kelele tu kutwa nzima hapa bila points. Huyu binti anaweza infuence watu zaidi ya 1000 kubadili mwelekeo. Unaelewa lakini maana yangu? Uliza nikupe maelezo? Mwambie na mwenzako mlionaye dark city. Kama hamtaki, endeleeni na jamvi la style yenu

Very true anaweza kuwaconvince sio watu 1000 tu ila hata milioni 1 ila wawe na level ya uelewa kama wako!!!
 
Ametumia haki kama mpenzi wa siasa... She is smart aliona anakosa majingle na kwa kupanda na kikwete anaweza pata dili za kutumbuiza.... All her cotracts zimefulia sasa anataka kutoka upya

Hongera kwa kutanguliza tumbo, maana hukua na haja ya kurudisha kadi kwenye public... Hukuichukulia kwenye mhadhara

Uamuzi wa Nakaaya - kama msanii wa kizazi kipya - uliwahamasisha Sugu, Mkoloni na wengineo, kuchukua uamuzi huo, lakini tofauti na wao, hawa ni wasanii na wazalendo pia.

Uzalendo ni kujitoa kwa ajili yako. Nakaaya anaweka maslahi yake mbele ya maslahi ya taifa; historia itamhukumu.

Lakini pia, kutokana na umri wake kuwa mdogo, huenda hana uwezo wa kubaini yatakayokuja kutokea siku zijazo. Unahitaji umri kuwa na busara za kionambali. Sugu, Mkoloni na wengine wameliona hili. Hata kama CHADEMA hawatachukua Urais (sidhani JK na wenzake wataridhia hili...), Bunge lijalo SIO la CCM.

Kisanii, ukimweka Nakaaya na Sugu, wafanye onesho la pamoja, utawapata washabiki wengi zaidi wa Sugu kuliko Nakaaya. Na kwa hili alilolifanya jana, kujitakia umaarufu kutamkosesha mauzo sokoni, kama wenzake walio kwenye kampeni tayari. Ndio, watamwingiza kwenye kampeni, ataenda kumpigia debe JK. Sawa, anataka maslahi, yake. Ya taifa? Hana habari nayo, hata kidogo.

Kila la kheri.

-> Mwana wa Haki
 
nakaaya sumari amerudisha kadi ya chadema jioni ya leo na kumkabidhi jk kwenye mkutano wake ulio fanyika leo mkoani arusha, jk amempongeza sana kwa kitendo hicho na kumwambia karibu mama ccm ndicho chama pekee tanzania.

cha ajabu nini kama ccm ilifikia hatua ya wagombe wake katika majimbo mbali mbali kuchalisha kadi feki na kuwagawia wananchi kwa nia moja tu ya kusaka riziki. Ilikuwa hatari zaidi kubaki na puppate kama huyu tena ambaye alitaka kui8ngia hadi kwenye sebule za chadema.

Nilipata kutoa somahapa tofauti kati ya kazi ya siasa na kazi chama. Wengi wetu tunavutiwa na jinsi chadema wanayoendesha kazi zao za chama kiasi cha kuweza kuwa na siasa safi yenye kuleta matumaini ya uongozi bora.

Mtu asiye na msimamo kama nakaaya angeweza kujipenyeza kirahisi katika kazi za chama za chadema na kutuvurugia utaratibu mzima wa utendaji wa kazi za kisiasa wa chadema tofauti na ilivyokuwa 2005 hadi 2010.

Taarifa zilizopo ni kuwa aliwekewa vitisho kutokana na ushiriki wa criminal activities akiwa nje ya nchi

mwache aende huko kwa mafisadi wenzanke walioko icu!!!!!!!!!!!!!!
!
 
" i'm a country girl from Tanzania, but i'm a modern African woman. I am tired of man telling me what a woman can be and tired of man telling me what a woman can do. And stop telling me how to dress and what to say"......... Nakaaya to CNN

Kukimbilia CCM ni kwenda kuhakikisha msimamo wake huo anautekeleza or she have decided to have money telling her what to say and do instead of man?
 
Jamani Wana jamvi kuna mtu ana e-mail yake ili nimu inbox coz nataka ajue nini alichokifanya.
 
kuna mtu ana e-mail yake coz nataka nimu inbox, ajue nini alichofanya
 
Back
Top Bottom