Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

Kwani nyinyi Nakaaya akihamia CCM ndo amekufa? kwasababu hamumsemi Mwera aliye ihama Chadema wakati alikuwa Mbunge kutoka Chadema, munamsema Nakaaya ambaye hajawahi kushika uongozi wowote na kutoa mchango wowoto katika Chadema, nyinyi vipi Bwana,, ujue siku ya kufa nyani ikifika we utaona tu, miti yooooteeee itateleza sasa hapo nahis kila mtu ataonekana Mchawi.. mi nilisema CHADEMA kuna mamluki ambao wataiharibu,,

Chadema na Mamluki , sasa nadhani mutaanza kukubaliana na mimi
 
Nakayaaa ha ha ha, sasa angalia pia na Afya yako kwa karibu zaidi. Na zingatia ushauri wa drs.
 
Who is she in this country ? she can go anywhere but CHANGE is on its way so soon !
 
ndio kazi ya siasa za tanzania na CCM, kununua watu ambao wanadhani ni popular, lakini wanakosea kwani watazania wa sasa sio wale wa zamani. Huyu nadhanin alijiunda chadema hana muda mrefu saaaaaana, pale Kigoma walimnunua mbunge sembuse msaniiiii
 
Wakati huu ni wakati wa kuwajua wapiganaji wa kweli na wa uongo. hakuna sababu ya kuumiza kichwa eti Nakaaya kahamia CCM. kama kawaida JK kamwahidi cheo akishinda, hii nchi tusipofanya mabadiliko sasa itakuwa mbaya kuliko hata hizi five years zilizopita. Nasikia uchungu sana kusikia kijana tena tuliyedhani ni mwanamageuzi, mpinga Ufisadi leo anaungana nao. Anyway that's democrasy
 
Wahenga walisema, ndege wafananao huruka pamoja. Msishangae sana kuhusu Nakaaya na JK, hawa wanafanana, ingawa si kwa "daraja" moja.

Nyepesi/nyeti nilizozinyaka - katika safari yangu ndefu ya UCHOKONOZI - nimenyetishwa kwamba miaka kadhaa, Nakaaya, wakati akiwa mwajiriwa (cashier/teller) wa benki ya Standard Chartered, jijini Dar es Salaam, aliwahi kukumbwa na kashfa ya wizi wa pesa kadhaa wakati akiwa kazini. Habari za kuaminika (source withheld) zinadai kwamba wakati huo Nakaaya alikuwa anatumia jina lake la Glory/Gloria, lakini baada ya kukumbwa na kasha hiyo iliyomfikisha lupango (na kesi kuzimwa kiaina), aliacha kutumia jina hilo na kuanza kutumia hilo la nyumbani, Nakaaya.

Wenye data zaidi mnaombwa kufuatilia. Tunataka kujua ukweli wa madai haya.

Asanteni.

<(MCHOKONOZI)>
i cant believe yule dada ni mwizi!!!!
 
Nakaya amerudi CCM sababu ya kumtengenezea Baba yake ulaji kumbukeni Mzee wake ni CCM damu sasa alipojitangaza ni mpinzani mzee wake aliambiwa atakosa kibarua sasa akawa hana ujanja bali kula matapishi yake ili amuokoe Mzee Sumary. Pole sana Nakaya hiyo ndio CCM inajua kucheza na akili za watu
 
Wakuu zangu ebu niulize kitu kimoja, Hawa watu wakitoka CCM kuingia Chadema wanaitwa ni watu wenye tamaa waliokosa Uongozi, lakini nachoshangaa CCM hiyo hiyo inapokea watu kutoka vyama vingine sijui hawa wako vipi?!. Hivi huyu binti hafikirii huko CCM anachukuliwa vipi ndani ya CCM?
Kaka... politics is a dirty game, we should expect anything clean out of it!
 
Uamuzi wa Nakaaya - kama msanii wa kizazi kipya - uliwahamasisha Sugu, Mkoloni na wengineo, kuchukua uamuzi huo, lakini tofauti na wao, hawa ni wasanii na wazalendo pia.

Uzalendo ni kujitoa kwa ajili yako. Nakaaya anaweka maslahi yake mbele ya maslahi ya taifa; historia itamhukumu.

Lakini pia, kutokana na umri wake kuwa mdogo, huenda hana uwezo wa kubaini yatakayokuja kutokea siku zijazo. Unahitaji umri kuwa na busara za kionambali. Sugu, Mkoloni na wengine wameliona hili. Hata kama CHADEMA hawatachukua Urais (sidhani JK na wenzake wataridhia hili...), Bunge lijalo SIO la CCM.

Kisanii, ukimweka Nakaaya na Sugu, wafanye onesho la pamoja, utawapata washabiki wengi zaidi wa Sugu kuliko Nakaaya. Na kwa hili alilolifanya jana, kujitakia umaarufu kutamkosesha mauzo sokoni, kama wenzake walio kwenye kampeni tayari. Ndio, watamwingiza kwenye kampeni, ataenda kumpigia debe JK. Sawa, anataka maslahi, yake. Ya taifa? Hana habari nayo, hata kidogo.

Kila la kheri.

-> Mwana wa Haki
I beg to differ... Sugu alianza uharakati kabla nakaaya hajaiba hata benki, sugu was not inspired by Nakaaya kama unajua vizuri histroria ya sugu utanielewa, mkoloni na dr joni walianza harakati from their fvery first song na wanajulika wazi, kumbuka kwamba nakaaya bado ni new generation ingawa she is a talent, kusema nakaaya alimisnpire sugu ni sawa na kusema Ali kiba aliminspire Professor Jay

Tulikua na too proud, hard blasters, kwanza unit na wengine mkuu, wote walikua wanaharakati... ni Clouds na Mkuu ndo wamekuja kubadili upepo na ukumbuke hata akina nature, Temba ni njaa ndo inawaweka pale clouds maana album haziuzi ni concerts na jingle ndo zinazolipa

Now pia tusisahau Karama wa bock 41 - KIKOSI CHA MIZINGA naye yuko kafu and ni mwanaharakati mzuri without nakaya inspiration

LETS NOT MIX UP THINKS HERE
 
Mi ninamtazamo tofauti sana na watu wanaohama vyama hasa kipindi hiki cha uchaguzi, mimi nawafananisha na wale wanawake wa pale ohio, k'ndoni makaburini na Kaumba nite club Moro, ni watu ambao hawana muelekeo na kuiju demokrasia vyema.Utakuta kila anaye hama chama aidha kapigwa chini kwenye kura za maoni au kapewa hela/rushwa, mi sielewi kuwa mtu mzima uanweza kuudhalilisha utu wako wa fedha, Je nikikuita CHANGUDOA WA SIASA nimekosea? Mi namuita Nakaaya "CHANGUDOA WA SIASA", hii ni prostittution in politics,Nakaaya kafanya hivyo aidha apate fursa ya kuonana na Mkwere kwani anamjua kuwa ni dhaifu maana mara utasikia Ridhiwani kapewa kazi ya kumuingiza UVCCM au hata kumpa UDC au hata akamegwa na mkwere na kupewa kazi BOT au sehemu nyeti zenye mshiko, Huyu sio mwana mapinduzi halisi na anayesema eti Nkaaya ni hovo tu huyu "SHE IS NOT STRONG WOMAN BUT A PROSTITUTE OF POLITICS". Unajua njaa zitamuua maana kaaza kusema ataungana na wasanii wengine kukampenia CCM. je si umeona amaeona Marlaw anakula hela ndio maana kaamua kuhama chadema kwani chadema hawaimbi bongo flava bali kutangaza sera tu, Ukisikiliza hotuba za JK n full usanii kama bongoflava tu. Mi nimeisikia Clouds hio news nikawasilianana machalii wa CHADEMA Arusha, wamesema wamemind mbaya kwa hio ajiandae na kupata upinzania sana hapo arusha, labda ahame jiji la Arusha.
 
Mbona mnajadili watu? Jadilini masuala muhimu ya Kitaifa na yenye tija kwa mtanzania. Hawa CCM wanaanzisha mijadala uchwara ya kujadili watu ili tupoteze muda kujadili watu badala ya issues!
Kamwe wana CHADEMA msikubali ulozi huu!
Kama wana ubavu wajitokeze hadharani tuchambue masuala ya msingi yanayohusu taifa hili....!
 
Nakaaya ameonyesha kuwa ni MSANII wa kweli. Msanii anajua siku HAZIGANDI na mambo yote yanapaswa kufanyika kisanii hasa katika siasa za TANZANIA.
 
Huyu nilishamsoma tangu kipindi kile alipofunga "ndoa" na msanii wa Dead Prez akadanganywa atapewa contract na Sony, kumbe chizi anajipigia tu! Akarudi bongo analalamika wamemwonea, hayuko makini huyu sista.
JF Kwa DATA NOMA...
 
Nakaaya alikosa ubunge wa viti maalum wa Arusha baada ya kujitoa dakika za mwisho katika Mkuu wa BAWACHA uliofanyika palepale SabaSaba. Hata hivyo matokeo ya mkutano ule yalibatilishwa na jina lake liliendelea kuwepo katika potential nominees waliopelekwa Tume ya Uchaguzi.

Nahisi (ingawa sitaki kuamini) kuwa Nakaaya alikuwa kimaslahi zaidi na baada ya kuona ameyakosa akaamua kuwa njia pekee ni kurudi CCM ili aweze kupata nafasi ya kuimba kwenye majukwaa kama TMK wanaume wanavyofanya.


Nakaaya Sumari ameamua kujitosa katika kinyang”anyiro cha kuwania ubunge wa viti maalumu mkoani Arusha kupitia chama cha demokarisia na maendeleo (Chadema) kwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo mjini Arusha.
nakaayasiasa.jpg
Nakaaya ambaye ni katibu mhamasishaji wa baraza la vijana la Chadema wilayani Arusha alichukua fomu ya kuwania kiti hicho juzi katika ofisi za chama hicho zilizopo maneeo ya Esso jengo la Meru Plaza mjini Arusha.
Akiwa ameongozana na mwenyekiti wa vijana wa Chadema wilaya ya Arsuha. Exaud Mamuya sanjari na katibu wa vijana, Arnold Kamnde, mgombea huyo alichukua fomu ya kuwania kiti hicho majira ya saa 3:30 asubuhi katika ofisi hizo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kuwania kiti hicho Nakaaya alisema ya kuwa binafsi anahisi ya kuwa nafasi ya yeye kuwa mwakilishi wa wanawake wa mkoa wa Arusha katika bunge la jamhuri nchini kupitia chadema mkoani Arusha umewadia.
Nakaaya alisema ya kuwa lengo kubwa lililomsukuma kuwania nafasi hiyo ni kutokana na uchungu alionao hususani mateso wanayopata wakinamama katika masusla ya afya ya uzazi katika huku akihaidi kusimamia masula ya afya ya uzazi kwa wakianamama nchini.
“Nahisi muda umefika wa kutenda ninayoyahubiri siku zote,nataka nikasimamie matatizo ya uzazi kwa wakinamama hili linanipa uchungu katika maisha yangu siku zote.Nataka nikawawakilishe wanawake wa mkoa wa Arusha kupitia chama changu nina imani nitashinda nafasi hii kwasababu ninajiamini, hivyo naomba mniunge mkono wanawake’alisema Nakaaya.
Awali akimkabidhi fomu ya kuwania nafsi hiyo katibu wa Chadema wilayani Arusha,Bakari Kasembe aliwataka wanawake wote wa mkoa wa Arusha kupitia chama hicho kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi hiyo.
Kasembe alisistiza ya kuwa awali chama chao hakikuwa na uwakilishi wa kiti hicho mkoani Arusha katika bunge la jamhuri nchini lakini wakati huu wamejipanga kutoa viti vitatu na kiti cha ubunge wa Arusha mjini.
Tayari joto la kuwania nafasi ya ubunge wa viti maalumu mkoani Arusha kupitia chama hicho limeanza kushika kasi ambapo hadi sasa tayari wagombea wawili wameshajitokeza kuwania kiti hicho ambao ni Magreth Olotu na Joyce Muya.

From: Wahapahapa

VIPI UBUNGE ALIKWAMA? Pole sana mama....... Rudi ukale hela za kodi yetu na migodi. Ila angalia usije ukawa umekosea.
 
kaazi kweli kweli hivi naomba kuuliza kwa nini kila mt anakimbilia CCM????
 
I quite agree. Sugu ni mwanaharakati wa zamani sana. Toka akiwa pale Shell ya Gapco anauza mafuta. Enzi hizo muziki tulikuwa tunaurekodo kwenye cassette tapes na sio CD. By that time i am sure Nakaaya was still at school.

I beg to differ... Sugu alianza uharakati kabla nakaaya hajaiba hata benki, sugu was not inspired by Nakaaya kama unajua vizuri histroria ya sugu utanielewa, mkoloni na dr joni walianza harakati from their fvery first song na wanajulika wazi, kumbuka kwamba nakaaya bado ni new generation ingawa she is a talent, kusema nakaaya alimisnpire sugu ni sawa na kusema Ali kiba aliminspire Professor Jay

Tulikua na too proud, hard blasters, kwanza unit na wengine mkuu, wote walikua wanaharakati... ni Clouds na Mkuu ndo wamekuja kubadili upepo na ukumbuke hata akina nature, Temba ni njaa ndo inawaweka pale clouds maana album haziuzi ni concerts na jingle ndo zinazolipa

Now pia tusisahau Karama wa bock 41 - KIKOSI CHA MIZINGA naye yuko kafu and ni mwanaharakati mzuri without nakaya inspiration

LETS NOT MIX UP THINKS HERE
 
Kumbuka, 'mtu na mtu hufanya watu'.
Ninaposema ni watu si mtu namaanisha imejijenga kichama zaidi na si mtu.CHADEMA si kama ilivyokuwa NCCR-Mageuzi alivyoondoka mrema ndiyo ikafa,leo hata aondoke mbowe CHADEMA bado itaendelea kuwepo,nini nakaaya
 
Huwezi kujua mkuu, labda anadhani kuwa akipewa ukuu wa wilaya atasaidia wanawake na watoto wale aliokuwa akiwapigania.

Again, kila la heri Nakaaya.

Mwafrika, mbona unamtetea sana!!!! Ingawa simfahamu huyu mtu nasikitika sana kwa yeye kukubali kununuliwa na mafisadi. Ukumbuke kuwa ahadi za JK si za kuziamini sana!!!
 
Back
Top Bottom