Nakanusha: Hospitali za Umma hazipendi kutoa huduma mbovu isipokuwa majukumu yanawalemea

Point tupu
 
serikali inalijua hilo lakini ipo kimya, zahanati huko vijijini zinaemdeshwa na mtumishi mmoja, mda mwingine hata yeye anachoka anafunga anajificha, ndo maisha yanavyoenda ivyo

lawama waipelekee CCM sio watu wasiohusika
Very good tena mtumishi mwenyewe unakuta ni medical attendant
 
Wao ndiyo wanaajili?
 
Bro umetumia nguvu kubwa kueleza mambo yaliyo wazi(hongera)
Kwa mtanzania mkaazi anaelewa jinsi sekta zote za umma zilivyo choka mbaya.Ukiondoa mtima nyongo,kila mwenye roho safi juu ya watumishi haya anayajua.Mimi niseme 'wananchi wa Tanzania mara nyingi hujenga chuki dhidi ya watumishi wa umma bila sababu!
Siyo huko tu,watu wanaenda kazini lakini anaja anaenda kutimiza baadhi ya majukumu na mengine anajua hatashughulika nayo kwani yapo juu ya uwezo wake.
Niulize tu swali,
NI SEKTA/IDARA GANI HAPA TANZANIA INAFANYA VIZURI NA KULETA MATOKEO BORA?
Nijijibu,HAMNA! maana hata saccos 'CCM' imeshindwa ku-deliver!!
 
Mfumo mbovu wa Ujamaa alioujenga Nyerere ndiyo umetukwamisha kiuchumi. Uchumi ukikwama, hata huduma za afya zinakuwa mbaya. Ndiyo maana vigogo wakiugua wanaenda kutibiwa nje ya nchi.
V8 ya mwigulu ambayo ingeweza kununua vifaa Kibao vya maabara, napo lawama kwa nyerere.
 
Utawasikia wanasema kasomee afya kazi zake ni za heshima na malipo mazuri ila ukiwaona wamepauka sana kuliko sisi Administrators wa Taasisi za Serikali.
Suala la kupauka halina uhusiano wowote na afya wala elimu wala huo uadministrator wako, kukuza kipato ni weledi tu wa mtu, wapo darasa la 7 wana maisha mazuri kuliko degree holders
 
Duh, muhimbili pale na ukubwa wote nimekaa jam kuanzia 12 asubuh mpaka 12 jion na Bado, majibu Sasa inakaribia wiki Sasa Bado, yaan unachoka hoi
 

Amtaki hao mkiletewa watu wenye uwezo wa kupigana kubadili tabia za wahudumu na kufahamu regulations za huduma mnaanza kuwatukana.

Si mlikuwa mnamtaka ‘Ummy Mwalimu’ haya sasa kila mtu apambane na hali yake kutokana na mfuko wake, ukiona vipi nenda Kenya au South Africa kama matajiri wanavyofanya.
 
Private ndio zinawahudumu tosherezi?
 
Elewa mada kwanza ndugu yangu
 
Duh, muhimbili pale na ukubwa wote nimekaa jam kuanzia 12 asubuh mpaka 12 jion na Bado, majibu Sasa inakaribia wiki Sasa Bado, yaan unachoka hoi
huwenda mnaosubiri majibu mpoa hata 600
 
Wengi wanaoropoka huko mitandaoni wanashindwa kuelewa ukweli kwamba hospital za serikali zimezidiwa na wagonjwa, upungufu wa dawa na vifaa tiba,kukosa wataalamu au upungufu,vifaa tiba nk..

Hao hao ndio utakuta wanapinga hata ujenzi mpya unaendelea , watakwambia majengo sio huduma sasa sijui huduma zitafanyika chini ya miti au vipi..

Rais anapambana kutatua upungufu ambapo zaidi ya wahudumu wa Afya 15,000 wanaingia kazini mwesi huu,ikumbukwe Miaka ya hapo kuna watu waliokuwa hawaajiri kwa visingizio vya kujenga sgr and such nonsense..
 
V8 ya mwigulu ambayo ingeweza kununua vifaa Kibao vya maabara, napo lawama kwa nyerere.
Nyerere angetuachia mfumo wa demokrasia, ingekuwa rahisi kumdhibiti huyo Mwigulu na wenzake. Lakini Nyerere alikataa demokrasia.
 
Fikiria ni Mara ngapi Ummy Mwalimu amepiga ngonjera bungeni juu ya bima ya afya kwa wote!. Utasikia bunge lijalo serikali italeta mswada wa bima ya afya kwa wote; bunge likianza maigizo ni yaleyale ya bunge lijalo serikali italeta mswada wa bima ya afya kwa wote!.

Kwa hiyo, kwa hiyo, kwa hiyo (narudia,kwa hiyo) kinacholeta shida katika nchi hii hata katika sekta ya afya sio wahudumu/ wataalamu wa afya bali siasa imeharibu kila kitu. Tunao madakatari wenye weledi na utaalamu wa kiwango cha kustahili lakini hawahusishwi katika mipango na maamuzi katika sekta ya afya bali maamuzi yanatolewa na mtu ambae hata hana utaalamu wowote kwenye sekta ya afya.

Madakatari na wahudumu wengine wa sekta ya afya wanafanya kazi kubwa Sana ya kututibu sisi ila kikwazo kipo kwa wanasiasa ambao wanasema bungeni hawaendi kubeba zege bali kuchanganya maneno tu yawe ya kweli au ya uongo (nikimrejea Augustino Lyatonga Mrema).

Sisi tunaambiwa elimu bure; haya tafuteni watoto wa wanasiasa Kama mtawakuta kwenye hizo zinazoitwa elimu bure Kama sio mtawakuta Feza boys/girls, Casmiri, Marian boys and girls. Haya, tuendelee kushangilia elimu bure wakati darasani Mwalimu hawezi kupata nafasi ya kudhibiti wanafunzi wapiga kelele waliopo pale backbench.

Matatizo ya nchi hii yanaanzishwa na kusababishwa na wanasiasa forehence no room of blaming civil servants unless proved viz scientific research.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…