Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

nashukuru sana nina maswali 3

1.Nini tofauti kati ya Diabetes type-1 na diabetes type-2

2.Je kwa nini mtu mwenye diabetes type-2 anashindwa kufanya vizuri tendo la ndoa na nini dawa yake

3. je kama tatizo limesababishwa na over weight je akipunguza tatizo linakuwa limeisha? au kuna dawa anatakiwa kutumia pia
 
Habari doctor hivi mvulana akitembea na msichana baadae mvulana awe anachubuka tatizo linakuwa ni nini?
 
Nini madhara ya aviam nostril spray kwa mtoto anayeitumia kwa mda mrefu?
 
Niliwai kutumia sindano za penadul wkt wamenidiagnose R.Athritis je hiyo dawa inaponya moja kwa moja au kwa muda na nini side effect zake?
 
Misoprostosol inatumika kama maintainance dhihidi ya vidonda vya tumbo hasa kwa watu wanaopata treatment ya
NSAID´s(Non-steroid anti-inflammatory drugs) na wana vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na NSAID´s.Inaweza kutumika pia kuinduce birth na kama treatment ya kutokwa na dam nyingi baada ya kujifungua,kutoa mimba na kama treatment baada ya spontaneous abortion.

zinapatikana wapi?je ni legal kuziuza?
 
Dokta,mke wangu anakula sana udongo na mchele mbichi, je kuna tiba yoyote ya kumsaidia ili aache?

pia wakati wa tendo la ndoa anatoka uchafu kama maziwa mgando au mchele uliolowekwa sana,ni nini tatizo?na tiba ni ipi?

Tips:huwa anaosha sehemu zake za siri juux2 tu na maji...hatumii sabuni wala haingizi kidole,ndivyo alivyofundishwa kwao.
 
hello Huwa naskia kuna vyakula unaweza kutumia vikaongeza umbile la uume!Kama ni kweli ni vyakula gani?Je kuna madhara yoyote?Majibu please
Hakuna vyakula vinavyoongeza umbile la kiume,kuna vyakula vya kuongeza hamu/mihemeko(afrodisiac)).
 
hallow mtaalam, does your speciality cover things like addiction ya sigara?
Capt Nemo
Kuacha kuvuta sigara ni kujitolea na kuweka malengo.Na swali la muhimu la kujiuliza ni je una matarajio gani ukiacha kuvuta sigara?Kuna vitu viwili vya muhimu unavyotakiwa kuviovercome navyo ni:
  1. Physical addiction ya mwili kuzoea nicotin
  2. Physcological addiction ya uvutaji wa sigara:Ili kuepuka phsycological addiction ni muhimu uwe na motivation na uipe kipaumbele hio motivation.Epuka kuwa katika hali au vitu ambayo vitakuvutia kuvuta sigara.Jiambie wewe mwenyewe na walio wa karibu yako kwamba huvuti sigara.
Kuna dawa zinazoweza kutumika kusaidia kuacha uvutaji wa sigara na pia products zinazoweza kutumia kucover nicotin addiction kama

  • nicotin mouth spray,
  • nicotin chewing gums,
  • nicotin lozenges na
  • nicotin plasters.
Hizo products zina nicotin lakini katika kiwango kidogo ukilinganisha na sigara,kiwango ambacho kitasaidia kucover abstinence symptoms.Baada ya miezi 3 ukiacha taratibu mwili utazoea low doses za nicotin kutoka kwenye products na kupelekea kuacha uvutaji wa sigara taratibu.Ni muhimu mwanzoni utambue unavuta sigara ngapi kwa siku.Kwasababu dosage na strength za nicotin products ni tofauti.Ni kawaida kuanza na high doses na kushuka kwenye low doses.Na nicotin chewing gums/lozenges zina utafunaji wake maalum,hazitafunwi kama chewing ngum ya kawaida.Unatafuna mpaka upate ladha kali ya nicotin.Unaihifadhi chewing gum/lozenge kwenye shavu mpaka ladha ipungue na unarudia tena upya.Plaster unatumia kwa masaa 24.Unaiweka juu kwenye mkono,mgongoni au pajani.Dawa zinazoweza kutumika ni:

ZYBAN(BUPROPION) ni dawa mmojawapo ina inhibit reuptake ya dopamin na nor-adrenalin neurotransmitter vinavyotolewa kutoka kwenye central nerve system.Inasemekana pia dawa hii ina effect kwenye nicotin receptor.Siku 6 za mwanzo unakula kidonge kimoja kwa siku na baada ya hapo kidonge kimoja mara mbili kwa siku.Zikipita wiki 7 bila mafaniko inabidi tiba isimamishwe.Dawa hii inasababisha kukosa kwa usingizi ili kuepuka hali hio ni vyema kuepuka kutumia usiku.

CHAMPIX(VARENIKLIN) ni dawa nyingeneyo ambayo inafanya kazi kwa kuactivate nicotin receptor pamoja na kurelease dopamin neurotransmitter kwenye ubongo lakini katika kiwango kidogo ukilinganisha na nicotin.Inasaidia kuondoa haja ya kuvuta sigara na kusaidia through addiction process.Vareniklin inajiunga kwenye nicotin receptor na kuzuia nicotin kujiunga hapo.Kumbuka nictoin ikijiunga kwenye nicotin receptor ndio tunafurahia uvutaji wa sigara lakini vareniklin ikijiunga hapo inazuia nicotin kufanya kazi yake.Tiba hii inachukua muda wa wiki 12.Matumizi yake ni kama ifuatavyo:

  • DAY 1-3:1 tablet of 0,5 mg daily

  • DAY 4-7:1 tablet of 0,5 mg twice a day

  • DAY 8 and further:1 tablet of 1 mg twice a day.
Ukipata sideeffects ya dawa hii ni kawaida kupunguza dozi na kutumia 0,5 mg twice day,Ukipatwa na kichefchef unaweza kula dawa pamoja na chakula.Dawa zote pili zinaweza kuathiri uwezo wako wa kuendesha gari kwasababu zinafanya kazi kwenye central nervous system.Kila la kheri mkuu.
 
Dokta,mke wangu anakula sana udongo na mchele mbichi, je kuna tiba yoyote ya kumsaidia ili aache?

pia wakati wa tendo la ndoa anatoka uchafu kama maziwa mgando au mchele uliolowekwa sana, ni nini tatizo?na tiba ni ipi?

Tips:huwa anaosha sehemu zake za siri juux2 tu na maji...hatumii sabuni wala haingizi kidole,ndivyo alivyofundishwa kwao.
 
Dokta,mke wangu anakula sana udongo na mchele mbichi,je kuna tiba yoyote ya kumsaidia ili aache?pia wakati wa tendo la ndoa anatoka uchafu kama maziwa mgando au mchele uliolowekwa sana,ni nini tatizo?na tiba ni ipi?Tips:huwa anaosha sehemu zake za siri juux2 tu na maji...hatumii sabuni wala haingizi kidole,ndivyo alivyofundishwa kwao.
Mkuu salito,Hali ya mkeo kula udongo na mchele mbichi kipindi cha ujauzito ni carving inayotokana na ujauzito.

Ni aghalabu kushauri tiba kwa wajazito kama wanaafya njema na wanatatizo kama la mkeo. Mjamzito anapaswa apate tiba pale tu inapoidi kwa sababu afya yake ni muhimu na ugonjwa wake unaweza kuwa na madhara kwa mtoto.

Ningependa kama ungefunguka zaidi je mkeo ana washwa ukeni? amekuwa mwekundu kwenye eneo la uke?
 
Last edited by a moderator:
wadada wengi wanasuffer kuwa na weusi katikati ya mapaja, vipi watumie dawa ipi kupunguza au kuondoa kabisa
Weusi katikati ya mapaja inatokana na friction kati ya mapaja, aidha kwasababu wa muongezeko wa kimwili kwamba mapaja yanagusana na kusugana na kupelekea mchubuko na joto likizidi hali hii inaweza kupeleka vidonda na ngozi kubadilika.

Sina experience na dawa inayoweza kubadilisha uhasilia wa ngozi. Lakuepuka ni kuongezeka kwa uzito bila mpangilio au kuvaa tights au suruali ili kuhakikisha mapaja hayagusani.
 
Ni kiwango gani cha haemoglobin mwanaume hutakiwa kuwa nacho ktk damu? Na ferroton capsules husaidiaje kuongeza wingi wa damu?
 
naomba kujuzwa candidas creams zinavofanya kazi kutibu fangus
 
Hellow wapendwa,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu dawa zozote zenye active ingredients (DRUGS). Kama una maswali kuhusu matumizi yake, matumizi yake pamoja na dawa nyingine, vyakula (interactions), athari zake (side effects) au hata kama unataka kujuzwa jinsi dawa inavyofanya kazi kutibu ugonjwa!!

Karibuni sana..


1: Mkuu,naomba kujua kama kuna permanent pharmacological remedy for masterbation-induced premature ejaculation,loss of morning erections and weak erections

2: Ni astringent gani nzuri itumike in management of external hemorrhoids
 
Mtaalamu, nina tatizo la kukoroma nitumie dawa gani kwa tatizo hili
 
Back
Top Bottom