Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Kaka nasumbuliwa jipu kwenye kwapa.. nilienda hospital wiki iliyopita nikapewa dawa inaitwa ampoxin nikaitumia jipu likaisha but wiki hii naona kama tena linaanza.. kuna dawa nyingine naweza kutumia lakin isiwe sindano..
Natanguliza shukurani
 
Mkuu anaemia zipo aina tofauti kama nilivyokujibu awali inaweza kusababishwa na blood loss(mfano kutokana na kujifungua,vidonda vya tumbo,matumizi ya baadi ya dawa n.k), mapungufu ya uzalishaji wa chembechembe nyekundu za dam(mf. erytropoetin hormone inayotengenezwa kwenye figo ili kustimulate uzalishwaji wa chembechembe nyekundu kutoka kwenye bone marrow haiwajibiki ipasavyo) au kuharibika kwa chembechembe nyekundu za dam kwasababu zinatengenezwa zenye kasoro(sickle cell anemia)!
Haemoglobin ikiwa chini ya 13g/dL cells za mwiloihazitopata oxygen ya kutosha.Na dalili mojawapo ni mwili kuchoka ni kwasababu viungo vya mwili vinakosa mahitaji muhimu ili vifunction ipasavyo.

Asante dr. Ubarikiwe kwa kutuelimisha
 
Dear dr. eti myopia eye defects inaweza kuwa corrected kwa lishe au mfumo flani wa vyakula bila kuvaa miwani? Je nifanye nn ili nipone bila kutumia miwani?
 
Kwani watu wenye HIV hupewa bactrime/septrin kama tiba opportunistic inffectons na nini madhara ya septrine kama ikitumiwa kwa muda mrefu
 
1:Mkuu,naomba kujua kama kuna permanent pharmacological remedy for masterbation-induced premature ejaculation,loss of morning erections and weak erections2:Ni astringent gani nzuri itumike in management of external hemorrhoids


Tunapopata msisimko wa kimwili, nerve impulses zinatumwa kutoka kwenye ubongo kwenda kwenye corpus carvenosa, ambapo signal substance Nitrogen monokside(NO) inazuia kuvunjwavunjwa kwa GTP(Guanine-5-triphosphate) - cGMP(Cyclic Guanine monophosphate) inayosababisha muscles zirelax na uume usimame.
  • Ili uume usimame ipasavyo venes must be compressed.Compressionmechanism ikiwa defect erection inapotea partially au totally kwasababu kunakuwa na venous leckage.
  • Kitu kingine ni nerveimpulses nilizozitaja kwenye first paragraph(sympathic and parasympathic motor neurons) zinaweza kuwa disturbed na kupeleka weak erection n.k So through masterbation you could triggering reflexes too often uncautionally or defeating compression mechanisms.
  • And these are just my speculations.Hakuna direct scientific explanation how can masterbation prior to premature ejaculation.
  • Unaweza kutumia scheriproct/alcos anal suppositories/cream kama management ya external hemorrhoid!
 
Ninatatizo aleji ya vumbi,pua zinawasha kupita maelezo+chafya za nguvu kila mara mpaka kichwa na macho vinauma na kupoteza nguvu ya kuona+kamasi sisizo kauka+harufu mbaya ya kamasi na pua kwa ujumla na kunakipindi niliwahi kutoa kamasi zenye mchanganyiko na damu kwa njia ya mdomo.inasabashwa na nn?Na Nini tiba yake?
 
Nina bibi yangu anatafuna meno mpka kichwa kinamuuma na akiwa anatafuna ukimsemesha huwa hasikii.

Ameshindwa kuacha.Inasababishwa nanini?na nini tiba yake?Tumeshaenda sana hosp lakin bado
 
Ninatatizo aleji ya vumbi,pua zinawasha kupita maelezo+chafya za nguvu kila mara mpaka kichwa na macho vinauma na kupoteza nguvu ya kuona+kamasi sisizo kauka+harufu mbaya ya kamasi na pua kwa ujumla na kunakipindi niliwahi kutoa kamasi zenye mchanganyiko na damu kwa njia ya mdomo.inasabashwa na nn?Na Nini tiba yake?
Mkuu kumbuka njia ya hewa iko karibu na njia ya chakula kwahio si jambo laajabu kilichopuani kwenda mdomoni mf ukikosea kula ukipaliwa punje ya wali inaweza itokee kwa njia ya hewa.

Allergy inasababishwa na allergens inapojiunga kwenye IgE-antibody na inapostimulate mastcells kuproduce inflammatory substance like histamine.

Histamine inasababisha tunapata allergic reaction!Allergens ni vitu kama vumbi,vyakula n.k!Na ndio maana tukiwa na allergy tunatakiwa tutumie anti-histamins kama cetirizin, loratadin, kestine/ebastin, desloratadin au phexofenadinhydrochloride!Kama una running nose na macho yanaewashwa unapaswa kutumia cortison nostril spray ili kupunguza inflammation kwenye pua au antihistamin nostril spray na antihistamin eyedrops kwaajili ya macho yanayowasha!
CC MAULA
 
Asante kwa mada hii

Nina maswali

1. Nini dawa ya constipation?

2. Nina ndugu yangu mwanamke amejifungua mwezi mmoja uliopita anapata constipation ambayo inampelekea kutokwa na damu wakati wa kujisaidia haja kubwa, tatizo ni nini? dawa gani zitamsaidia kumbuka ananyonyesha?

3. Madhara ya constipation na/au hemmoroids ni yapi kwa mwanamke?
 
Dah mkuu,mungu akulinde na akupe umri mrefu ukiwa mwenye afya njema.Mwisho naomba unisaidie kuhusu masikio kuziba(hayaumi), tiba tafadhali,
Mkuu kumbuka njia ya hewa iko karibu na njia ya chakula kwahio si jambo laajabu kilichopuani kwenda mdomoni mf ukikosea kula ukipaliwa punje ya wali inaweza itokee kwa njia ya hewa.Allergy inasababishwa na allergens inapojiunga kwenye IgE-antibody na inapostimulate mastcells kuproduce inflammatory substance like histamine.Histamine inasababisha tunapata allergic reaction!Allergens ni vitu kama vumbi,vyakula n.k!Na ndio maana tukiwa na allergy tunatakiwa tutumie anti-histamins kama cetirizin,loratadin,kestine/ebastin,desloratadin au phexofenadinhydrochloride!Kama una running nose na macho yanaewashwa unapaswa kutumia cortison nostril spray ili kupunguza inflammation kwenye pua au antihistamin nostril spray na antihistamin eyedrops kwaajili ya macho yanayowasha!
 
Mkuu salito,Hali ya mkeo kula udongo na mchele mbichi kipindi cha ujauzito ni carving inayotokana na ujauzito.Ni aghalabu kushauri tiba kwa wajazito kama wanaafya njema na wanatatizo kama la mkeo.Mjamzito anapaswa apate tiba pale tu inapoidi kwa sababu afya yake ni muhimu na ugonjwa wake unaweza kuwa na madhara kwa mtoto.Ningependa kama ungefunguka zaidi je mkeo ana washwa ukeni?amekuwa mwekundu kwenye eneo la uke?

Hapana docta,mke wangu sio mjamzito ila kula udongo na mchele mbichi ndio kawaida yake,hapana kwenye uke hakujawa kwekundu,ila anasema anawashwa kidogo sio sana.
 
Last edited by a moderator:
Yaani katika siku nimefurahi kuwa JF ni leo....na nina furaha sana kwamba ni Mwanamke amenifurahisha hivi.

Ubarikiwe sana na Mwenyenzi Mungu Gourgeousmimi, Mungu azidishe moyo huu. Am so proud of you.

Tuonekane kwa mazuri zaidi ya jinsia yetu.
 
mie tatizo langu ni chafya.
sina mafua kabisa ila per hour Zinafika hata kumi.
zinanifanya pia kichwa kuuma.
je kuna tiba?
 
Kuna mtu ameuliza juu kuhusu dawa ya genital warts naomba uscroll ukasome!

OK nimeona ukishauri dawa iitwayo condolyine/wartec. Nina swali bado kuhusu hili, warts ni magonjwa ya zinaa lakini hii ya pearly penile papules haiambukizi na haihusiki na magonjwa ya zinaa, sasa unaimanisha hiyo dawa inatibu kotekote? Thanks
 
Asante kwa mada hii

Nina maswali

1. Nini dawa ya constipation?
2. Nina ndugu yangu mwanamke amejifungua mwezi mmoja uliopita anapata constipation ambayo inampelekea kutokwa na damu wakati wa kujisaidia haja kubwa, tatizo ni nini? dawa gani zitamsaidia kumbuka ananyonyesha?
3. Madhara ya constipation na/au hemmoroids ni yapi kwa mwanamke?

send to: @gorgeousmimi, Riwa, MziziMkavu na wengine wote wenye ujuzi bila ubaguzi




(Constipation) UKOSEFU WA KUTOPATA CHOO LAINI.


UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.


Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.


MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?
Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa. Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?
Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?
Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda msalani. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil' muda mfupi kabla ya kwenda kulala. Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.

MARADI YA BAWASIRI Hemorrhoid



Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.

AINA ZA BAWASIRI

  1. NJE
    Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.
  2. NDANI
    Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
  3. Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:

Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.
Je bawasiri husababishwa na nini?


BAWASIRI HUSABABISHWA NA NINI?
Bawasiri husababishwa na;


  • Tatizo sugu la kuharisha
  • Kupata kinyesi kigumu
  • Ujauzito
  • Uzito kupita kiasi (obesity)
  • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
  • Umri mkubwa


DALILI ZA BAWASIRI


  • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
  • Maumivu au usumbufu
  • Kinyesi kuvuja
  • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa


MATATIZO YANAYOWEZA KUTOKEA KUTOKANA NA BAWASIRI


  • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
  • Strangulated hemorrhoids

VIPIMO NA UCHUNGUZI


  • Digital rectal examination
  • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
  • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)

MATIBABU

Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri


  • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.

  • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano

  • Coagulation (infrared, laser and bipolar)

  • Upasuaji;
Hemorrhoidectomy
Stapled hemorrhoidopexy



NJIA ZA KUZUIA BAWASIRI


  • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
  • Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)
  • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa

Mgonjwa Aende hospitali kutibiwa asipo poona nitafute mimi kwa wakati wako dawa ninayo ninakukupatia
Ukinitaka bonyeza hapa.Mawasiliano
 
OK nimeona ukishauri dawa iitwayo condolyine/wartec. Nina swali bado kuhusu hili, warts ni magonjwa ya zinaa lakini hii ya pearly penile papules haiambukizi na haihusiki na magonjwa ya zinaa, sasa unaimanisha hiyo dawa inatibu kotekote? Thanks
Inaweza kutumika kwenye warts zilizosababishwa na human papilloma virus!Ili kupata warts si lazima uwe umezini skin contact is enough to transmit it!
 
Hapana docta,mke wangu sio mjamzito ila kula udongo na mchele mbichi ndio kawaida yake,hapana kwenye uke hakujawa kwekundu,ila anasema anawashwa kidogo sio sana.
Ana fungus kwenye uke!Atumie clomatrizol 1% ointment + vaginal tablett !kuhusu kula udongo ni craving anayotakiwa aache coz udongo si kitu kinachohitajika kwenye mwili wa mwanaadamu hasa kwenye utumbo mpana/appendix thats a foreign substance!
 
Back
Top Bottom