Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

nilienda kwa dokta akaniambia nina fungus wa mdomo na alisema wakikaa kwa muda mrefu tumbo nalo huweza kuathiriwa. Na kweli kuna mda tumbo lilikuwa linaunguruma na kuumwa chin ya ktovu lkn saiv halitokei. Sasa sikujua kama ni systemic fungus hakunambia. Na dawa alizonipa ni MICONAZOLE OROMUCOSAL GEL BP 20g ya kumung'unya then unaimeza kwa kujaza kijiko kidogo. Pia fungus ktk sehem za siri na alinipa dawa ya ktumia lkn kwnyw nilipona na huw nikiona dalili naitumia hiyo iitwayo FUNGIGEN CREAM/MICONAZOLE CREAM BP 2%. Naomba unisaidie hyo SYSTEMIC FUNGUS INA DALILI GANI NA NINI TIBA YAKE ? NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU DR.JF
Mkuu kama una weak immune system fungus ya kawaida inavamia deeper tissues.Nakushauri urudi hosp uchukuliwe vipimo vya dam kujua kama una tatizo hilo au lah.Na kama unalo utahitaji triazole mfano voriconazole au amphotericin(hii ni toxic kwa mafigo).

Dalili ni tofauti kutoka kwa mtu na mtu, kama homa, kikohozi, baridi, kutoka jasho usiku, kupoteza ham ya kula, kupungua uzito, kuchoka na depression.

Kila la kheri mkuu
 
Mkuu kama una weak immune system fungus ya kawaida inavamia deeper tissues.Nakushauri urudi hosp uchukuliwe vipimo vya dam kujua kama una tatizo hilo au lah.Na kama unalo utahitaji triazole mfano voriconazole au amphotericin(hii ni toxic kwa mafigo).Dalili ni tofauti kutoka kwa mtu na mtu,kama homa,kikohozi,baridi,kutoka jasho usiku,kupoteza ham ya kula,kupungua uzito,kuchoka na depression.Kila la kheri mkuu

Asante sana mkuu. Mungu akubariki zaidi na zaidi.
 
Hio dawa ya pili mkuu ni rabeprazole(ni PPI),fluconazole(anti-fungal) na heligokit ni trippelcure ya Peptic ulcers with positive Helicobacter pylori
Dosage ni:
  1. Aidha Protonpumpinhibitor + amoxicillin 1g × 2 + clarithromycin 500mg x 2 Kwa siku saba mfululizo

  1. Au protonpumpinhibitor(lansoprazole au pantoprazole 40mg × 2 ) + metrodinazol 400mg /tidinazol 500mg x 2 + amoxicillin 750mg x 2 /clarithromycin 500mg x 2 kwa siku 7
Tiba inaweza kurefushwa mpaka 2 weeks(Heligokit ina clarithromycin 250mg,tidinazole 500mg na lansoprazole 30mg)if im correct!So clarithromycin itabidi ule vidonge viwili mara mbili kwa siku na hivo vingine kimoja mara mbili kwa siku kwa siku saba!
 
Hellow wapendwa,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu dawa zozote zenye active ingredients (DRUGS). Kama una maswali kuhusu matumizi yake, matumizi yake pamoja na dawa nyingine, vyakula (interactions), athari zake (side effects) au hata kama unataka kujuzwa jinsi dawa inavyofanya kazi kutibu ugonjwa!!

Karibuni sana..

Hongera sana dokta na asante sana kwa ushauri na majibu ya maswali mbalimbali toka kwa wanajamvi. Mola akulipe mbadala kwa ukarimu wako.

Swali langu.

Nina tatizo la kutopata haja kubwa kwa muda mrefu. Ninaweza kukaa siku mpaka tano bila kupata choo au napata kiasi kidogo ukilinganisha uwingi wa mlo ninaokula.

Kuna wakati huwa sisikii maumivu ya haja kubwa. Kuna wakati nikienda haja kubwa, niki-push (nikijikwinya) ili mzigo ushuke, mzigo haushuki ama unashuka lakini hautoki nnje, unaishia ktk tundu ya njia ya haja kubwa, hilo naligundua pindi ninatawaza. Baazi ya wataalamu walinishauri ninywe maji mengi na mapapai. Nikifanya hivyo huwa naenda sana haja ndogo (in terms of frequences).

Na pia najamba ushuzi unaonuka harufu ya mapapai. Kuna baazi ya dawa za asili na kisasa nikitumia huwa napata choo ila kwa muda. Nilienda hospital kufanya checkup halikuonekana tatizo la kutisha. Pia nilifanya kipimo cha colonoscopy na majibu hayakuwa mabaya sana. Kuna dokta alinishauri nisile vyakula vya ngano.

Nikaamia ktk ugari wa dona kwa mbogamboga na viaz na mihogo ya kuchemsha kama vitafunio vya chai. Hii ilisaidia kidogo. Je kuna tiba ya kudumu ama ndio ni-stick ktk dona mbogamboga na viaz na mihogo ya kuchemsha???, na niachane na vyakula vya ngano na wali???
 
Dokta pia nina maswali mawili kama ifuatavyo:

1. Swali toka kwa mke wangu.

Yeye idadi ya siku zake za hedhi haziko fixed. Zina-fractuate mara kwa mara. Zina-range kati ya 33 hadi 60. Yaan mwez huu zaweza fika 45 wakti mwezi ulopita zilikuwa 36 na mwezi ujao zaweza fika 54. Inatupa shida kupanga uzazi kwa kutumia karenda. Je, tatizo laweza kuwa nini? Na je kuna tiba?

2. Swali toka kwa msaidizI wetu wa kazi tunayeishi nae hapa nyumbani.

Yeye huwa anaishiwa nguvu kiasi cha kushindwa kufanya kazi zake za ndani ambazo ndizo alizoajiriwa kuzifanya. Tulimpeleka hospital kufanya checkup lakini hakukutwa na tatizo.

Huwa anapungukiwa sana na damu. Tukampima na sickle cell lakini pia kipimo kilionyesha hakuwa na sickle cell.

Kuna dokta alinambia huenda ana tatizo la kupoteza damu nyingi wakat wa hedh. Nilipomuuliza na baada ya kumfaniyia study, nikapata jibu kuwa ni kweli anatokwa na damu nying wakt wa hedh.

Study yangU niliifanya kwa kumchorea graph na nikagundua kuwa kila tarehe zinazofanana kwa kila mwez ndio hupatwa na tatizo lake linalomsumbua pamoja na maumivu makali ya tumbo.

Kupunguza tatizo la kuishiwa damu nikamuanzishia dozi ya dawa ya kuongeza damu. Namnunulia chupa mbili za dawa ya kuongeza damu (iron tonic ama hemovit), moja anaitumia katikati ya mwezi na nyingine anaitumia anapokaribia kuingia ktk hedhi.

Mwez huu umepita salama, sikumsikia akilalamika kusikia kizunguzungu na kuishiwa na nguvu. Limebaki tatizo la maumivu ya tumbo.

Je, tatizo lake la kupoteza damu nyingi wakat wa hedhi linatibika? Ama ndio atatakiwa awe anakunywa dawa za kuongeza damu kila anapokaribia kuingia ktk hedhi?
 
Fanya mazoezi ya mwili na kegel exercise.Ukienda kujisaidia haja ndogo fanya kama unakojoa kidogo kisha unazuia mkojo usitoke hesabu mpaka tano,kojoa kidogo kisha zuia tena kwa kucontrol misuli(usichanganye misuli hii na ya miguu,tumbo na makalio) na usijizuie kupumua!!!Rudia zoezi hilo mara 10 kwa siku mara tatu.Kila la kheri mkuu

Dr hapa umegusa mahali penyewe!wanaume wengi tatizo kubwa ndio hilo la nguvu za kiume! Je tofauti na zoezi la kegel ulilolitolea maelezo kwa kukojoa na kubana huo msuli naomba utupatie mbinu nyingine ya kuutambua vizuri huu msuli na namna bora ya kuufanyisha mazoezi~nashukuru dr
 
Kuna kama vijipu na mba zinanitokea kichwani na nyuma ya shingo,nilienda hospitali nikapewa,cloxacilin vikaisha,vikajirudia tena nikapewa dawa hiyo hiyo na sasa vimeanza kurudi kwa kasi.Nitumie dawa gani?
 
Hongera sana dokta na asante sana kwa ushauri na majibu ya maswali mbalimbali toka kwa wanajamvi. Mola akulipe mbadala kwa ukarimu wako.Swali langu.Nina tatizo la kutopata haja kubwa kwa muda mrefu. Ninaweza kukaa siku mpaka tano bila kupata choo au napata kiasi kidogo ukilinganisha uwingi wa mlo ninaokula. Kuna wakati huwa sisikii maumivu ya haja kubwa. Kuna wakati nikienda haja kubwa, niki-push (nikijikwinya) ili mzigo ushuke, mzigo haushuki ama unashuka lakini hautoki nnje, unaishia ktk tundu ya njia ya haja kubwa, hilo naligundua pindi ninatawaza. Baazi ya wataalamu walinishauri ninywe maji mengi na mapapai. Nikifanya hivyo huwa naenda sana haja ndogo (in terms of frequences). Na pia najamba ushuzi unaonuka harufu ya mapapai. Kuna baazi ya dawa za asili na kisasa nikitumia huwa napata choo ila kwa muda. Nilienda hospital kufanya checkup halikuonekana tatizo la kutisha. Pia nilifanya kipimo cha colonoscopy na majibu hayakuwa mabaya sana. Kuna dokta alinishauri nisile vyakula vya ngano. Nikaamia ktk ugari wa dona kwa mbogamboga na viaz na mihogo ya kuchemsha kama vitafunio vya chai. Hii ilisaidia kidogo. Je kuna tiba ya kudumu ama ndio ni-stick ktk dona mbogamboga na viaz na mihogo ya kuchemsha???, na niachane na vyakula vya ngano na wali???
Mkuu una IRRITABEL BOWEL SYNDROME.
Tiba za constipation zipo na nimeziorodhesha hapo juu kwenye swali la constipation!Nakushauri ujaribu kubadili lifestyle
1.Kunywa maji ya kutosha
2.Kula dried prunes au apricots kila siku iwe rutine
last ned.jpg
Prunes
last ned (1).jpg
Apricots
3.Hakikisha unakuwa physically active kila siku
4.Usijizuie ukijisikia kwenda chooni na usijilazimishe kama huna choo.Kila la kheri mkuu
 
Asante kwa ushauri dokta.
Prunes na apricots kwa kibongo ndio vyakula gani hivyo??? Sijawahi kuvisikia au kuviona!!!
 
Mimi ni msichana wa miaka 24 nina tatizo la siku zangu kusogea mbele mara kwa mara nikahama mkoa au kama niliumwa nikatumia dawa yoyote basi zinaenda mbele sana mpaka napata wasiwasi je hili ni tatizo au ni kitu cha kawaida
Pole,Ni kawaida... stress au mabadiliko ya mazingira yanaweza kuathiri mzunguko wa hedhi!
 
Nini tiba ya Allopecia Areata? (kichwani). Nimetumia Dermovate kwa miezi 2 baada ya kushauriwa na Dr. ila tatizo bado lipo pale pale. Na je ni sahihi kutumia shampoo ya Ketoconazole?
 
Nini tiba ya Allopecia Areata? (kichwani). Nimetumia Dermovate kwa miezi 2 baada ya kushauriwa na Dr. ila tatizo bado lipo pale pale. Na je ni sahihi kutumia shampoo ya Ketoconazole?

Huo ugonjwa hauna tiba mkuu ni autoimmune disease.Dermovat inapunguza symptoms tu lakini haitibu ugonjwa!Inabidi ujufunze jinsi ya kuishi nao!
 
Dokta pia nina maswali mawili kama ifuatavyo:1. Swali toka kwa mke wangu.Yeye idadi ya siku zake za hedhi haziko fixed. Zina-fractuate mara kwa mara. Zina-range kati ya 33 hadi 60. Yaan mwez huu zaweza fika 45 wakti mwezi ulopita zilikuwa 36 na mwezi ujao zaweza fika 54. Inatupa shida kupanga uzazi kwa kutumia karenda. Jee tatizo laweza kuwa nini??? Na jee kuna tiba???2. Swali toka kwa msaidiz wetu wa kazi tunayeishi nae hapa nyumbani.Yeye huwa anaishiwa nguvu kiasi cha kushindwa kufanya kazi zake za ndani ambazo ndizo alizoajiriwa kuzifanya. Tulimpeleka hospital kufanya checkup lakini hakukutwa na tatizo. Huwa anapungukiwa sana na damu. Tukampima na sickle cell lakini pia kipimo kilionyesha hakuwa na sickle cell. Kuna dokta alinambia huenda ana tatizo la kupoteza damu nyingi wakat wa hedh. Nilipomuuliza na baada ya kumfaniyia study, nikapata jibu kuwa ni kweli anatokwa na damu nying wakt wa hedh. Study yang niliifanya kwa kumchorea graph na nikagundua kuwa kila tarehe zinazofanana kwa kila mwez ndio hupatwa na tatizo lake linalomsumbua pamoja na maumivu makali ya tumbo. Kupunguza tatizo la kuishiwa damu nikamuanzishia dozi ya dawa ya kuongeza damu. Namnunulia chupa mbili za dawa ya kuongeza damu (iron tonic ama hemovit), moja anaitumia katikati ya mwezi na nyingine anaitumia anapokaribia kuingia ktk hedhi. Mwez huu umepita salama, sikumsikia akilalamika kusikia kizunguzungu na kuishiwa na nguvu. Limebaki tatizo la maumivu ya tumbo.Jee tatizo lake la kupoteza damu nyingi wakat wa hedhi linatibika??? Ama ndio atatakiwa awe anakunywa dawa za kuongeza damu kila anapokaribia kuingia ktk hedhi???

Mkuu huyo dada wa kazi anatatizo linaloitwa MENORRHAGIA:Anaweza kutibiwa na vidonge vya uzazi wa mpango hio ni alternative moja.

Nyingine ni antifibrolytics kama tranexamic acid ni inhibitor ya fibrinolysis ili kupunguza kiwango cha damu kinachotoka au NSAID´s mfano ibuprofen au naproxen.

Mkeo ana tatizo linaloitwa OLIGOMENORRHEA:Hedhi inayokaa kati ya siku 35-miezi 6
Inasababishwa na aidha failure kwenye

  • Pitutary gland kupelekea low levels of estradiol,low FSH(Follicle stimulating hormone)/LH(Leutenizing hormone),au
  • Failure kwenye ovaries kupelekea low levels of estradiol,high FSH/LH,
  • Polycystisk ovranian syndrome(PCOS),
  • Kuzaliwa na mapungufu kwenye viungo vya uzazi.
  • Hypo/hyperthyroidism.

Tiba ni kwa Gondotropines au clomifen inayo induce gonadotropinrelease na ovulation baada ya kupata right diagnosis.
Diagnosis inatolewa kwa hormone analysis ya estradiol,FSH,LH,Prolactin na TSH.
 
Kuna kama vijipu na mba zinanitokea kichwani na nyuma ya shingo,nilienda hospitali nikapewa,cloxacilin vikaisha,vikajirudia tena nikapewa dawa hiyo hiyo na sasa vimeanza kurudi kwa kasi.Nitumie dawa gani?
Nenda tena kwa daktari unahitaji topical fucidin with hydrocortison pamoja na hio cloxacillin
 
Mtaalamu, nina tatizo la kukoroma nitumie dawa gani kwa tatizo hili
Tukilala musclature ya upper respiratory system ina relax,kwahio njia ya hewa inakuwa nyembamba na tukipumua eneo hilo lina vibrate, pressure inaongezeka na kupeleka msuguano kati ya soft tissues na kusababisha kukoroma.

Pombe na dawa za usingizi zinasababisha njia ya hewa kuwa nyembamba, na hali inazidi kuwa mbaya ukiwa umelala usingizi mzito.

Uvutaji wa sigara pia unaweza kuwa chanzo na uzito mkubwa. Ili kuepuka kukoroma
  1. kama uzito umezidi jaribu kupungua,
  2. epuka kunywa pombe,
  3. kuvuta sigara na sleeping pills (hypnoticum na sedatives),
  4. Ukilala lala ubavu epuka kulala na mgongo
Tiba zinazoweza kutumika ni nostril spray au plaster unayoweka juu kwenye pua ili kufungua njia ya hewa.
 
Aleji ni ugonjwa?Na hutibiwaje kama ni ugonjwa au sio ugonjwa?Mfano-kutokwa na viuvimbe kichwan vinavyojaa tunga usaa asili ya ring worm ni aleji au na kiasili hutibiwaje?
Aleji ni ugonjwa na kuna mtu nimemjibu kuhusiana na suala hilo na tiba zake, naomba ujaribu kuperuziperuzi niloyaandika kwenye uzi huu utaona.

Hizo ring worm zilizopo kichwani ni seborroheic dermatittis. Nimeandika pia kuhusu suala hilo inaweza kutibiwa na ketokonazole/selensulphide shampoo au topical glucocorticoids kama betnovat 1mg/ml liniment.
 
Back
Top Bottom