Dr. Mke wangu hakuona siku zake na alipofanya 'pregnancy test' ilikuwa positive. Akashauriwa kutumia 'Misoprostal' vidonge vinne ambapo viwili alimeza na viwili alivitumbukiza ukeni. Usiku akaingia hedhi lakini damu ilitoka kwa kiwango kidogo sana. Baada ya siku 6 hivi akapima tena bado jibu likawa positive. Akatumia tena jana. Akaona tena hedhi damu ilikuwa nyingi kiasi lakini ilitoka kwa muda mfupi. Leo amefanya tena kipimo na jibu ni positive. Matukio yote haya yamefanyika ndani ya majuma mawili haya. Baada ya kuwasiliana na tabibu, pamoja na mambo mengine alimshauri kutumia tena lakini atumie wakati wa kulala.
Sasa, swali langu je ni ipi njia sahihi ya kutumia hizo dawa? Na, je, ni sawa akiirudia?
Natanguliza shukrani.
#Kaka