Prednisolone ni sythethic glucocorticoid ambayo inafanya kazi kwa kustimulate glucocorticoid receptor iliyopo kwenye cells tofauti za mwili.Glucocorticoid inapunguza inflammation response:Inapunguza inflammation kwa kupitia vyanzo kadhaa mfano inapunguza release ya chembechembe zinazosababisha inflammation itokee.
Glucocorticoid inatengenezwa pia mwilini kwenye adrenocortopic hormone.Ukiwa unatumia glucocorticoid bila mpangilio hasa systemic inasababisha negative feedback kwenye kwahio uzalishaji wake kwenye pitutary glands una pungua.
Unaweza kuepka hilo kwa kula dawa wakati wa asubuhi kwasababu production ya cortisol mwilini inakuwa juu asubuhi ili kuepuka adrenal suppression.
Na ukiwa unataka kuacha kutumia dawa unaacha kwa kuwithdraw taratibu kwa wiki kadhaa,ukiacha ghafla tu mwili hautopata muda kwa kuanzisha utengenezaji wa glucocorticoid kama awali kwenye pitutary glands na inaweza kupeleka dalili za ukosaji wa glucocorticoids ambayo hupeleka maumivu kwenye joints and muscles.
Glucocorticoid inafanya kazi kwenye baadhi ya viungo kama mifupa inazuia osteoblast kwenye bone tissue na kupeleka kuongezeka kulika kwa bone tissue na kupeleka kusababisha ugonjwa kama OSTEOPOROSIS ni sideeffect mmojawapo ya matumizi ya glucocorticoid kwa muda mrefu.
Na ndio maana tunashauri ukiwa unatumia prednisolone kwa muda mrefu ule calcium tablets with vitamin D[SUB]3[/SUB] ili kuepuka chances za kupata Osteoporosis,Calcium inasaidia kujenga mifupa kuwa imara na Vitamin D[SUB]3 [/SUB]inaongeza absorption ya calcium kutoka kwenye utumbo mpana.
Effects nyingine ni kama metabolic effects:Kuongezeka kwa sukari(bloodsugar),Tendency ya kupata infection haswa ukiwa unatumia dozi kubwa inasababisha immunosuppressive effect.Na kuongeza tendency ya kupata viralinfecton kama herpes au fungiinfection kama candida.
Side effects ziko tofauti nimeshaorodhesha osteoporosis na high bloodsugar/diabetes juu lakini ukumbuke zinapatikana baada ya matumizi ya muda mrefu na nyingine ziko kwenye picha niloiweka.
View attachment 236146
Dawa hii inatumia kutibu magonjwa mengi mno kuanzia astma/chronic obstructive pulmonary disease,allergies,reumathoid arthithis,mpaka cancer(in combination with other drugs).Kama ilivyo kila dawa kuna faida na kuna hasara.Tukipata tiba tunaipa kipaumbele afya yetu na ugonjwa unaotukabili.Side effects zina variety na ziko individual si kila mtu atapata athari nilizoorodhesha ila ni possibilty.Usiache kutumia dawa bila kushauriana na watu wa afya.Uwe na siku njema.