Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Hongera kwa uzi huu, hakika unatoa faida kubwa, madhara gani hupatikana kwa kukithirisha matumizi ya Omeprazole?
 
Hongera kwa uzi huu, hakika unatoa faida kubwa, madhara gani hupatikana kwa kukithirisha matumizi ya Omeprazole?
Ukizidisha matumizi ya omeprazole kuliko kawaida overodose unapatwa na dalili za mapito kama kichefchef,kuumwa na tumbo,kizunguzungu,kutapika,kuhara,kuumwa na kichwa,depression na hata kuchanganyikiwa!
 
gorgeousmimi nilikwenda pharmacy kutafuta hiyo misoprostosol wakakataa kuniuzia ni lazima cheti cha daktari?
 
Last edited by a moderator:
Hellow wapendwa,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu dawa zozote zenye active ingredients (DRUGS). Kama una maswali kuhusu matumizi yake, matumizi yake pamoja na dawa nyingine, vyakula (interactions), athari zake (side effects) au hata kama unataka kujuzwa jinsi dawa inavyofanya kazi kutibu ugonjwa!!

Karibuni sana..
wapi nitapata librium aka chlorodiazepoxide
 
mama anasumbuliwa na maumivu ya mkono kuanzia kwnye bega mpaka mwisho,pia unawasha kwa ndani na unakufa ganzi, umri yuko kwenye 50's
 
pia kuna mtu ana ile cjui ni fangas ambayo wanaitaga utango tango ndo imemuanza maeneo ya usoni,anaweza kutumia dawa gani
 
Huu Uzi nimeupenda sana...nini dawa ya dry coughing ?mgonjwa ana kama 3yrs ameshatumia dawa za vikohozi nyingi napia dawa za minyoo kikohozi kinatulia muda mfupi kinaanza tena.
 
Diazepam iko classified kama benzodiazepinederivate. Benzodiazepines zinajiunga kwenye receptor mwilini iliyopo kwenye ubongo inayoitwa GABA-receptor.

Na inasababisha muongezeko wa inflow ya chloride ions kwenye nervecells.Matokeo yake inapooza baadhi ya parts za ubongo. Hali hio inaweza kuleta;

Pshycological effects
: Nazo ni anxiety withdrawal au sedative effect (kusaidia mwili urelax kama mfano unatakiwa kufanyiwa surgical procedure)

Hypnotical effect:
Inachosha ubongo kwahio inaweza kutumika kama sleeping inducer (dawa ya usingizi), Au inaweza kutumika kama muscel relaxer na kusaidia na cramps/spasms!

= muscle

Nyuzi kama hizi ndiyo zenye maana, zina faida kubwa sana kwa jamii na zitatufundisha mengi wengi.

Ahsante sana mleta mada.
 
Dokta nilivunjika mguu mifupa yote miwili 27/8/2004, muhimbili walinitibia vbaya, mguu mpaka leo bado unauma Mara moja moja. Cwezi kukimbia wala kuvaa viatu vyenye visigino virefu kiasi. Nitumie dawa gani dokta?
 
pia kuna mtu ana ile cjui ni fangas ambayo wanaitaga utango tango ndo imemuanza maeneo ya usoni,anaweza kutumia dawa gani
Tumia Hydrocortison cream in a thin layer mara mbili kwa siku kwa muda wa wiki moja/ mbili.
 
Dokta nilivunjika mguu mifupa yote miwili 27/8/2004, muhimbili walinitibia vbaya, mguu mpaka leo bado unauma Mara moja moja. Cwezi kukimbia wala kuvaa viatu vyenye visigino virefu kiasi. Nitumie dawa gani dokta?
Pole sana mkuu sidhani kama tatizo lako naweza kukusaidia kwasababu liko nje ya uwezo wangu.

Dawa pekee ninazoweza kukushauri ni zakupunguzia maumivu kama tramadol/codeinphosphosesquihydrat au dawa za (neuropathic pain) kama pregabalin, gabapentin, carbamapezin, amitriptylin tu kwasababu umesema mguu unauma.
 
mama anasumbuliwa na maumivu ya mkono kuanzia kwnye bega mpaka mwisho,pia unawasha kwa ndani na unakufa ganzi, umri yuko kwenye 50's
Namshauri mama akacheki ugonjwa wa moyo(STABLE ANGINA PECTORIS).

Dalili zake ni kuumwa na mkono na kufa ganzi kama unavyoeleza,na kuhisi kama kuna umeme unatembea kwenye mkono.

Je ana matatizo kwenye kupumua na anasumbuliwa na mgongo na kiuno?anachoka akifanya activity yoyote nzito kama kupanda ngazi?

kupanda kilima?
 
Naomba msaada doctor nasumbuliwa sana na tumbo la mp siku tatu mfululizo ni kulala tu nilienda hosp.wakanipa dawa za kutuliza maumivu tu msaada please
 
Doctor nasumbuliwa sana na tumbo nikiwa mp hata kazi siwezi kufanya naweza tumia dawa zipi ili niweze kuondoa tatizo permanent ikishindikana hata temporarily nimechoka na hii hali kwa kweli
 
Huu Uzi nimeupenda sana...nini dawa ya dry coughing ?mgonjwa ana kama 3yrs ameshatumia dawa za vikohozi nyingi napia dawa za minyoo kikohozi kinatulia muda mfupi kinaanza tena.
Mkuu anakohoa wakati gani na je anapata shida(exertion) kupumua akikohoa?
 
Siyo mtoto ni MTU mzima .miaka mitatu anakohoa akipumzika ni kama wiki au mwezi anaanza tena.hana tatizo la kupumua na minyoo pia hana.
 
Doctor nasumbuliwa sana na tumbo nikiwa mp hata kazi siwezi kufanya naweza tumia dawa zipi ili niweze kuondoa tatizo permanent ikishindikana hata temporarily nimechoka na hii hali kwa kweli
Njia ya uzazi wa mpango inaweza kusaidia tatizo kama lako lisitokee. Au endelea kutumia dawa za maumivu kama ulivyoshauriwa na daktari lakini unapaswa kufanya hivo kila mwezi ukipata hedhi.
 
= muscle

Nyuzi kama hizi ndiyo zenye maana, zina faida kubwa sana kwa jamii na zitatufundisha mengi wengi.

Ahsante sana mleta mada.
Typing error...
Ahsante madam kwako pia kwa kupitia kwenye uzi huu!
 
Siyo mtoto ni MTU mzima .miaka mitatu anakohoa akipumzika ni kama wiki au mwezi anaanza tena.hana tatizo la kupumua na minyoo pia hana.
Nitakujatia magonjwa tofauti yanayoweza kupeleka mtu kupatwa na kikohozi kikavu kwasababu mm sijui mhusika amepata tiba gani mpaka sasa,kama ana magonjwa mengine au ni mvutaji wa sigara au kama yupo exponated na vumbi/moshi n.k
  1. Kikohozi cha kawaida ambacho kinasababishwa mfano na virusi.Kikohozi hiki kinaweza kumuandama mtu kwa wiki kadhaa.
  2. Uvutaji wa sigara unaweza kusaabisha kikohozi hasa asubuhi
  3. Acute Bronchitis:Hiki ni kikohozi kama nilichokianisha namba 1 ila kinakuwa kikali zaidi na mwanzo kinakuwa kikavu na chakukera,koo linauma na baada kinabadilika na kuwa makohozi.Hupatwi na homa ukiwa na kikohozi hiki,na hali yako kiafya haiwi mbaya
  4. Sinusitis:Kifua hiki kinaweza kibane mpaka muda wa mwezi moja.Pua zinabana,unakuwa na maumivu kwenye maeneo ya pua na kutoka kamasi.Inaweza kusababisha kikohozi kwasababu mabaki ya kwenye pua yanaenda kwenye koo.
  5. Asthma: hii ni chronic inflammation kwenye bronchi,huwapata sana watoto.Inasababisha mtu kukosa pumzi,kipindi kirefu cha kikohozi,na kuwatoka wheezing sound kwenye kifua.Kifua kinakuwa worse kipindi cha baridi na unapojituma kupuma sana kama ukifanya mazoezi n.k
  6. Baadhi ya dawa kama ACE-inhibitors zinatumika kutibu presha,moyo,diabetic nephropathy zinaweza kusababisha kikohozi
  7. Reflux ya acid: kutoka kwenye tumbo kwenda kwenye oesophagus inaweza kusababisha pia kikohozi.
  8. Heart failure:Ugonjwa huu wa moyo pia unaweza kusababisha kikohozi na shidha kwenye kupumua.
Yako magonjwa mengine pia yanayohusika na kikohozi chenye makohozi sijayaweka hapo.
 
Back
Top Bottom