Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Kwani watu wenye HIV hupewa bactrime/septrin kama tiba opportunistic inffectons na nini madhara ya septrine kama ikitumiwa kwa muda mrefu
Madhara hayana umuhimu kama afya ni dhoofu!Kama ilivyo antibiotics zote unaweza kutengeneza resistence!!
 
Hio dawa ya pili mkuu ni rabeprazole(ni PPI),fluconazole(anti-fungal) na heligokit ni trippelcure ya Peptic ulcers with positive Helicobacter pylori
Dosage ni:
  1. Aidha Protonpumpinhibitor + amoxicillin 1g × 2 + clarithromycin 500mg x 2 Kwa siku saba mfululizo

  1. Au protonpumpinhibitor(lansoprazole au pantoprazole 40mg × 2 ) + metrodinazol 400mg /tidinazol 500mg x 2 + amoxicillin 750mg x 2 /clarithromycin 500mg x 2 kwa siku 7
Tiba inaweza kurefushwa mpaka 2 weeks(Heligokit ina clarithromycin 250mg,tidinazole 500mg na lansoprazole 30mg)if im correct!So clarithromycin itabidi ule vidonge viwili mara mbili kwa siku na hivo vingine kimoja mara mbili kwa siku kwa siku saba!

Doctor je naweza kuzinywa zote kwa pamoja yaani heligo, rabeprazole na fluconazole kwa wakati mmoja? make nilipoenda kununua yule muuzaji kaniuzia heligo tu dozi ya kunywa siku 7 akaniambia ikiisha ndo nikachukue rabeprazole afu ndo maliza na fluconazole, eti hairuhusiwi kuzinywa kwa pamoja ila mie sijamwamini kabisa,
 
Doctor je naweza kuzinywa zote kwa pamoja yaani heligo, rabeprazole na fluconazole kwa wakati mmoja? make nilipoenda kununua yule muuzaji kaniuzia heligo tu dozi ya kunywa siku 7 akaniambia ikiisha ndo nikachukue rabeprazole afu ndo maliza na fluconazole, eti hairuhusiwi kuzinywa kwa pamoja ila mie sijamwamini kabisa,
Fluconazole unaweza kula na heligo kit,kisha baada ya siku 7 endelea na rabeprazole!
 
Trevo-food suppliment ndio mpango mzima. Inavirutubisho kutoka mimea 174. Nimeumwa Miguu kwa Muda mrefu nikitumia dawa tofauti.

Tangu nilipoelezwa kuhusu Trevo nakuanza kutumia miguu imepona na ninaona improvements kwenye maeneo mengine ya mwili pia.
 
Mtaalamu, nina tatizo la kukoroma nitumie dawa gani kwa tatizo hili

Kabla ya kutumia dawa jaribu kwanza kutumia snoring mouthpieces - mandibular advancement device na tongue stabilizing device - kama unaweza kuvipata. Hizi devices zinafanya kazi vizuri sana.

Pia lala kifudifudi. Usilale chali.
 
Asante sana dokta hopefully other professionals watathubutu.Je ni sahihi kutibu UTI kwa AZUMA ya vidonge vitatu?Ubarikiwe!
 
Huo ugonjwa hauna tiba mkuu ni autoimmune disease.Dermovat inapunguza symptoms tu lakini haitibu ugonjwa!Inabidi ujufunze jinsi ya kuishi nao!
Thanks kwa jibu Dr. na vipi kuhusu shampoo ya Ketoconazole.. ina madhara yoyote nikitumia huku napaka hiyo dermovate?
 
Dr. Mke wangu hakuona siku zake na alipofanya 'pregnancy test' ilikuwa positive. Akashauriwa kutumia 'Misoprostal' vidonge vinne ambapo viwili alimeza na viwili alivitumbukiza ukeni. Usiku akaingia hedhi lakini damu ilitoka kwa kiwango kidogo sana.

Baada ya siku 6 hivi akapima tena bado jibu likawa positive. Akatumia tena jana. Akaona tena hedhi damu ilikuwa nyingi kiasi lakini ilitoka kwa muda mfupi. Leo amefanya tena kipimo na jibu ni positive.

Matukio yote haya yamefanyika ndani ya majuma mawili haya. Baada ya kuwasiliana na tabibu, pamoja na mambo mengine alimshauri kutumia tena lakini atumie wakati wa kulala.

Sasa, swali langu je ni ipi njia sahihi ya kutumia hizo dawa? Na, je, ni sawa akiirudia?

Natanguliza shukrani.

#Kaka
 
Dr. hujanijibu swali langu. tafadhari Naomba kujibiwa.
Hormone unbalance inasababishwa na kutawala kwa homoni ya kike estrogen au kuongezeka kwa homoni ya estrogen na mapungufu ya progesterone mwilini.

Estrogen inatengenezwa kwenye mayai na ina husika na kujamiiana.Ina husika pia na hedhi na inahakikisha mwili unakuwa katika hali ipasayo kwenye kipindi ambacho mwanamke anaweza kubeba ujauzito yaani akiwa fertile!Estrogen inahakikisha mayai yanapevuka ipasavyo kwenye follicle phase na progesterone inaharibu yai ambalo limepevuka na halikurutubishwa.

Jinsi umri unavyokwenda ndivyo mayai(ovaries yanapunguza)uzalishaji wa estrogen na progesterone na kupeleka hormonal in balance.

Tiba ni hormone replacement therapy
 
ninasumbuliwa na tatizo la maeneo mbalimbali ya mwili wangu nahisi kama joto kali linalonipa maumivu kwa ndani, nikiwa katika mazingira ya baridi hali hii hubadilika na kuhisi baridi kali kati ya maeneo yafuatayo hasa miguuni, mapajani, kiunona na mgongoni pia, hali hii husababishwa na nini? na tiba yake inakuwaje? natanguliza shukrani.
 
Hormone unbalance inasababishwa na kutawala kwa homoni ya kike estrogen au kuongezeka kwa homoni ya estrogen na mapungufu ya progesterone mwilini.Estrogen inatengenezwa kwenye mayai na ina husika na kujamiiana.Ina husika pia na hedhi na inahakikisha mwili unakuwa katika hali ipasayo kwenye kipindi ambacho mwanamke anaweza kubeba ujauzito yaani akiwa fertile!Estrogen inahakikisha mayai yanapevuka ipasavyo kwenye follicle phase na progesterone inaharibu yai ambalo limepevuka na halikurutubishwa.Jinsi umri unavyokwenda ndivyo mayai(ovaries yanapunguza)uzalishaji wa estrogen na progesterone na kupeleka hormonal in balance.Tiba ni hormone replacement therapy

owkey asanteh kwa ufafanuzi ingawa sijasikia baadhi ya hormone kama zile ambazo huzalishwa kipindi cha mwanamke anavoingia utu uzima .mfano zile zinazochochea mabadiliko ya mwili kama sauti na kifua tukiachana na izo ambazo ushazielezea. sasa kwa izo nilizoongelea zikiwa hazijabalance huleta effects zipi? na ni namna gani ya kutatua tatizo?
 
habar dr,me nikajana wa kiume nasumbuliwa na tatizo la kuwashwa sana sehem za siri yan najikuna had nachubuka afu tena kuna layer ya ngoz huwa inajitengeneza na kutoka, pia kwenye mapaja na mikononi huwa natokwa na vipele afu vinato maji nikikamua vinawasha sana had nakosa amani,naomba na tiba tafadhal
 
Mkuu naomba unisaidio ckio langu linakua linafavuma na pia lna uma kwa waktcmmoja naomba jb
 
owkey asanteh kwa ufafanuzi ingawa sijasikia baadhi ya hormone kama zile ambazo huzalishwa kipindi cha mwanamke anavoingia utu uzima .mfano zile zinazochochea mabadiliko ya mwili kama sauti na kifua tukiachana na izo ambazo ushazielezea. sasa kwa izo nilizoongelea zikiwa hazijabalance huleta effects zipi? na ni namna gani ya kutatua tatizo?
Kuna mtu nimemjibu kuhusu oligomenorrhea ambayo ipo classified kama amenorrhea isipokuwa amenorrhea inaweza kuanzia miaka 16 na hedhi inaweza ipotee zaidi ya miezi 6.Na jinsi inavyosababishwa nimeandika pia.Nikagusia polycystic ovarian syndrome(kupata viuvimbe/cysts vingi kwenye mayai) ambayo husababishwa na kuongezeka/disturbance ya homoni ya kiume(androgens) ambayo husaabishwa pia imbalance ya homoni nyingine kama estrogen. Hii hupelekea msawajiko ktk mfumo wa hedhi,kuota kwa ndevu au vinyoleo kwa wanawake,matatizo kwenye mfumo wa uzazi na hata kisukari(Diabetes Type II).Hali hio hujitokeza kipindi cha balehe mpaka miaka 19 na watu wenye tatizo hili mara nyingi wanasumbuliwa na uzito vilevile.
Tiba ni tofauti:

  • Kama unataka ujauzito ni clomifen.

  • Kupunguza male characteristics vidonge vya uzazi wa mpango vinaweza kutumika mf ethinylestradiol(vinasaidia kuweka sawa mfumo wa hedhi,NB:inachukua miezi 8 mpaka uone mabadiliko) au spironolactone(aldactone) na dexamethasone ili kupunguza production ya homoni za kiume.
  • Kama una kisukari dawa za kisukari zinahusika mf metformin/Glucophage.Hizi itasaidia kucontrol kisukari na kupunguza uzalishaji wa homoni za kiume,kuuweka mfumo wa hedhi sawa,na hatimae kuongeza possibilties za kupata ujauzito.
 
Back
Top Bottom