Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

dokta pole na kazi hii kubwa ya kuwajibu watu na maelelezo mazuri. .

dokta nilisoma kikaratasi cha maelekezo ya dawa ya Spironolactone nikaona eti haitakiwi kutumiwa kwa pamoja na DIGOXN, sasa mi dawa zote hizo ni zaidi ya mwaka sasa natumia tena kwa pamoja(nilipewa hospital) je kuna tatizo lolote linaweza kujitokeza hapo? maana mi huwa nakunywa zote kwa wakati mmoja na dokta hajawah nitahadhalisha hilo.
 
Danny [URL="https://www.jamiiforums.com/" said:
Job
arrow-10x10.png
[/URL];12374478]dokta pole na kazi hii kubwa ya kuwajibu watu na maelelezo mazuri. . dokta nilisoma kikaratasi cha maelekezo ya dawa ya Spironolactone nikaona eti haitakiwi kutumiwa kwa pamoja na DIGOXN, sasa mi dawa zote hizo ni zaidi ya mwaka sasa natumia tena kwa pamoja(nilipewa hospital) je kuna tatizo lolote linaweza kujitokeza hapo? maana mi huwa nakunywa zote kwa wakati mmoja na dokta hajawah nitahadhalisha hilo.
Hello mkuu Danny Job,
Ndio kuna minor interaction kati ya spironolactone na digoxin.Digoxin ni dawa ambayo mabadiliko madogo ya plasma concentration yanaweza kusababisha fluctuations na kupeleka digitalis toxicity.Spironolactone inaweza kupunguza tubular secretion ya digoxin na kupelekea plasma clearance(amount of drug eliminated from the body) to decrease and hence increase plasma levels in blood.Dawa hizi mbili zikichanganywa ni muhimu mhusika achekiwe dalili za digoxin toxicity kama Caridac glycoside toxicity ,Central nervous system(CNS)symptoms,Gastrointestinal symptoms and visual symptoms.
Cardiac symptoms include:
  • Palpitations:mapigo ya moyo kuongezeka na kubadilika
  • Shortess of breath
  • Miguu kuvimba
  • Presha kushuka
  • Syncope:kuzimia au kupoteza faham
Gastrointestinal symptoms include:
  • Kupungua uzito wa mwili
  • Kichefchef
  • Kutapika
  • Maumivu kwenye tumbo
  • Kuhara
Central nervous system symptoms include:
  • Kizunguzungu
  • Kuchoka
  • Kitendo cha kujisikia kulala mchana
  • Kuchanganyikiwa
  • Maumivu ya kichwa
  • Hallucinations:Kufikiri vitu ambavyo havipo
  • Seizures
  • Neuropathic pain
Visual symptoms include:
  • Kuchanganya rangi ya kijani na njano,au nyekundu,brown,bluu na nyeupe
  • Photophobia-kutoweza kuwa kwenye mwanga
  • Mapungufu kwenye kuona n.k

Kama unapatwa na dalili zozote nilizozitaja hapo juu nakushauri ukaonane na daktari ili kucheki plasma concentration ya digoxin na kumaintain right dosage.Kila la kheri.
 
Hello mkuu Danny Job,Ndio kuna minor interaction kati ya spironolactone na digoxin.Digoxin ni dawa ambayo mabadiliko madogo ya plasma concentration yanaweza kusababisha fluctuations na kupeleka digitalis toxicity.Spironolactone inaweza kupunguza tubular secretion ya digoxin na kupelekea plasma clearance(amount of drug eliminated from the body) to decrease and hence increase plasma levels in blood.Dawa hizi mbili zikichanganywa ni muhimu mhusika achekiwe dalili za digoxin toxicity kama Caridac glycoside toxicity ,Central nervous system(CNS)symptoms,Gastrointestinal symptoms and visual symptoms.Cardiac symptoms include😛alpitations:mapigo ya moyo kuongezeka na kubadilika-Shortess of breath-Miguu kuvimba-Presha kushuka-Syncope:kuzimia au kupoteza fahamGastrointestinal symptoms include:-Kupungua uzito wa mwili-Kichefchef-Kutapika-Maumivu kwenye tumbo-Kuhara Central nervous system symptoms include: -Kizunguzungu-Kuchoka-Kitendo cha kujisikia kulala mchana-Kuchanganyikiwa-Maumivu ya kichwa-Hallucinations:Kufikiri vitu ambavyo havipo-Seizures-Neuropathic painVisual symptoms include:-Kuchanganya rangi ya kijani na njano,au nyekundu,brown,bluu na nyeupe-Photophobia-kutoweza kuwa kwenye mwanga-Mapungufu kwenye kuona n.kKama unapatwa na dalili zozote nilizozitaja hapo juu nakushauri ukaonane na daktari ili kucheki plasma concentration ya digoxin na kumaintain right dosage.Kila la kheri.[/QUOTE

aisee Dokta asante sana. .maana hapo kwenye CNS esp uchovu na kulala mchana mimi kwangu ilikuwa tatizo..

nashukuru & unachofanya si kidogo. .
Mungu akubariki.
 
Last edited by a moderator:
Kuna ndugu yangu anasumbuliwa na choo anaweza asipate choo wiki . tatizo ni nin? Au afanyeje
 
Dokta pole na kazi,mke wangu husumbuliwa na kichomi,kinakuwa kinambana tumboni hivi....kinambana saaana(kwanguvu) mpaka anatokwa na machozi sana, kichomi kikimshika hawez kuongea au kupumua vizuri zaidi yakuhangaika hangaika tu, na mara nyingi humtokea usiku usiku, humtokea kwa wastani wa mara moja kwa wiki hivi...atumie dawa gani tafadhari?
 
Kuna ndugu yangu anasumbuliwa na choo anaweza asipate choo wiki . tatizo ni nin? Au afanyeje
Nimeshajibu swali kama lako sehem za nyuma naomba uperuzi usome!Anywe maji ya kutosha,ale mboga za majani na matunda mengi!
 
naomba kuuliza hivi kuna sabuni rasmi za kuoshea sehemu za siri au hamna na kama zina madhara pia dondoshea madhara yake
 
Dokta pole na kazi,mke wangu husumbuliwa na kichomi,kinakuwa kinambana tumboni hivi....kinambana saaana(kwanguvu) mpaka anatokwa na machozi sana,kichomi kikimshika hawez kuongea au kupumua vizuri zaidi yakuhangaika hangaika tu,na mara nyingi humtokea usiku usiku,humtokea kwa wastani wa mara moja kwa wiki hivi...atumie dawa gani tafadhari?
  1. Je hali hio inamtokea akishapata mlo?
  2. Maumivu yapo eneo gani la tumbo?
  3. Maumivu yanasambaa kutoka tumboni kwenda mgongoni mpaka upande wa kulia wa bega?
  4. Akipewa scale ya 1-10 maumivu anayaweka kwenye namba ngapi?
  5. Naomba ufafanue zaidi anasumbuliwa na gesi tumboni?anacheua na kujamba sana?
 
Samahan doctor mm tumbo langu Mara kwa Mara linajaa sana gesi na choo kupata inakuwa kwa nadra sana naomba ushauri wako
 
naomba kuuliza hivi kuna sabuni rasmi za kuoshea sehemu za siri au hamna na kama zina madhara pia dondoshea madhara yake
Ndio kuna sabuni maalumu za kuoshea sehem za siri zenye low pH ya 3,5 na zina lactic acid bacterias ili kusaidia kubalance kiasi cha hao bacterias ukeni.

Sabuni hizi zinakuwa hazina mapovu na hazina harufu kali vilevile.Hazina madhara!!
 
Samahan doctor mm tumbo langu Mara kwa Mara linajaa sana gesi na choo kupata inakuwa kwa nadra sana naomba ushauri wako
Nimeandika kuhusu IRRITABLE BOWEL SYNDROME mtu aliuliza swali kama lako naomba uperuzi kwenye uzi kuu utaona hilo!!
 
Mkuu ahsante kwa maelezo yako ya kina, je, hapa nchini ni hospitali ipi ambayo naweza kufanyiwa uchunguzi wa kina wa kimaabara, mbali ya muhimbili? Pia suala la kuzidi, kuwa chini ama katika kiwango cha kawaida kwa vichocheo lina tambulika vipi?mbona viwango kwa kiasi kikubwa vipo in a required range mfano testosterone ranges from 1.9-15ng/ml na majibu yangu ni 6.36ng/ml ama kuna tatzo jingine sambamba na hilo? tafadhali.
Kiwango cha kawaida cha testosterone kwa wanaume kinatakiwa kiwe >8,5 nmol/l,kikiwa chini ya hapo una low levels of testosterone.Sifaham hospitali yoyote wanayoweza kukusaidia tatizo lako utanisameh kwa hilo!
 
Mkuu nisaidie watu na madaktar wamekuwa wakineyeyusha, niite kuyeyushw kwa sabb sijapata mafanikio yyt, miguu kuwaka moto kwenye nyayo, hii hali hupungua au hupotea wakati wa majira ya baridi. Lakini wakati wa joto huwa miguu huwaka moto.

Sisikii hii hali nikiwa matembea au nikiwa busy na kazi.

napata usumbufu mkubwa.

asante
Sehem gani ya unyayo?Kisigino?Hali hio imeanza lini na imeendelea kwa muda gani?

Una hisi kuna kitu chochote ulichofanya kilichochochea hali hio kutokea?
 
Thanks
Yeah nina uzoefu kidogo...mara ya kwanza nazinduka (huwa wanafanya kitu ili urudi concious au) nilikuwa na bwabwaja tu maneno mengimengi..
Atemp ya pil naambiwa nilksumbua sana na nikawa na nguvu za ajabu sana nikazuiliwa na watu walioahiba wa tatu....after nikajikuta namaumivu kwenye shingo, mbavu nk yaliyotokana na kukabwa..wakati ufahamu warudi. Thanka at least nina clues how GA is function
Ndio kuna sindano za antidot ambazo zina reverse effect ya anaesthetic zinaweza kutumika kukuamsha!!
 
Tofauti ya IVF na HSG ni ipi
Hello Dinazarde,
HSG(hysterosalpingogram) ni X-ray inayotumika kuangalia ndani ya kizazi(uterus) na mirija ya kizazi(fallopian tubes).

Njia hii mara nyingi inatumika kwa wanawake wenye matatizo ya kubeba ujauzito. Unapofanyiwa procedure hii rangi maalum(inayoleta mabadiliko ya rangi na mwanga(contrast) inatumika na mrija nyembamba unaowekwa kwenye uke mpaka kwenye mfuko wa uzazi ambapo picha zinachukuliwa kwa kutumia X-ray(fluoroscopy) pale rangi inapopita kwenye mfuko wa uzazi na mirija ya uzazi.

Picha zinazopigwa znaonesha majeraha yaliyopo kwenye mfuko wa uzazi na hata kama kuna mapungufu/kasoro kwenye eneo hilo.Unaweza kuona pia kama kuna kitu kinazuia mayai kufika kwenye mirija ya uzazi,hatimae kuzuia shahawa kufika kwenye mirija ya uzazi ili kupevusha yai.

IVF(In vitro fertilisation) ni njia inayotumika kurutubisha yai kwa kutumia mbegu ya kiume nje ya mwili.Njia tofauti zinatumika kusaidia kuchochea mayai ya mwanamke kuwa tayari kwa kupevushwa.

Mayai ya mwanamke yanatolewa kwenye kizazi yaliyotayari kupevushwa na shahawa zinatumika kurutubisha yai kwenye maabara.

Yai lilorutubishwa linaachwa lipevuke kwa siku 2-6 kisha linarudishwa ndani ya kizazi cha mwanamke kwa dhumuni la ujauzito.
 
Ndio kuna sabuni maalumu za kuoshea sehem za siri zenye low pH ya 3,5 na zina lactic acid bacterias ili kusaidia kubalance kiasi cha hao bacterias ukeni.Sabuni hizi zinakuwa hazina mapovu na hazina harufu kali vilevile.Hazina madhara!!

ahsante sana naomba nikuulize unaweza kunitajia japo aina mbili za sabuni hizo manake vitu ulivonitajia sina utaalam wa kuvitumbua nitakapo nunua sabuni
 
ahsante sana naomba nikuulize unaweza kunitajia japo aina mbili za sabuni hizo manake vitu ulivonitajia sina utaalam wa kuvitumbua nitakapo nunua sabuni
Sifaham kwa huko zinaitwaje jaribu kuulizia lactacyd!
 
Sehem gani ya unyayo?Kisigino?Hali hio imeanza lini na imeendelea kwa muda gani?Una hisi kuna kitu chochote ulichofanya kilichochochea hali hio kutokea?

hapana mkuu mimi pia ninahali hiyo, ni miguu yote eneo lote la unyayo. sikumbuki chochote kinacholeta hali hiyo,

mara kwanza /kupata joto kuwaka moto miguuni ni 2002.

Kutoka hapo hadi leo hii miguu inawaka moto nikiw nimepujipunzisha, au usiku nikiwa nimelala.

nikiwa busy sipati hii hali.

naisaidieni
 
Back
Top Bottom