Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Asante sana kwa uchambuzi murua, endelea kubarikiwa, sasa nn tiba ya anxiety au fear?
Tiba zipo tofauti za anxiety:
Cognitive therapy:ni therapy inayofanywa na psychologist kusaidia kuondokana na stress,fikra hasi na kukusaidia kukupa fikra chanya.
Dawa pia zinaweza kutumika kama
  1. Benzodiazepines(diazepam,oxazepam):Hii ni first choice kwa emergence situations,hazitakiwi kutumika muda mrefu kutokana na kusababisha toleranse na addiction,zinapaswa zitumike Kwa wiki 2-4,matumizi ya muda mrefu zaidi ya huo ni baada ya makubaliano na psychiatrist.
  2. Betablockers ni dawa ya presha na moyo lakini pia zinaweza kutumika temporarily kucontrol symptoms za anxiety kama za kimwili mfano kutetemeka,moyo kuenda mbio,kutoka jasho n.k
  3. Antidepressant ni dawa za depression kama venlafaxin zinazoweza kutumika pia kutibu anxiety/symptoms lakini zinachukua muda wa wiki 2-4 mpaka upate nafuu.
  4. Pregabalin ni antiepileptic,dawa hii pia inaweza kutumika kutibu anxiety na ina effekt sawia kama Benzodiazepines au venlafaxin.
 
Please mkuu msaada wa haraka mke wangu anasumbuliwa na tosess koo linauma sana! Amechoma sindano hazimsaidii naomba kujua zinasabishwa na nini na tiba yake ni nini zinamsumbua kwa muda mrefu kama 10 yrs! Huwa zibaibuka mara zinapotea nisaidie dawa ya kutibu kabisa.
Anachoma sindano gani?akiumwa na tonsils probably ana infection(bacterial/viral) au inflammation so ni muhimu ichukuliwe culture ya kwenye koo na vipimo vya damu ili apate tiba sahihi!
 
Anachoma sindano gani?akiumwa na tonsils probably ana infection(bacterial/viral) au inflammation so ni muhimu ichukuliwe culture ya kwenye koo na vipimo vya damu ili apate tiba sahihi!

Asante ngoja nifuatilie sindano alichoma nione...!
 
Nina tatizo la kutokwa na vipele au chunusi wakat wa ovulation na siku nikiwa nakaribia period inakuwa zaidi kama ndio nimebaleghe!

Samahan naweza fanya nn kuondokana na hadha hii na type ya ngozi ni ngozi ya mafuta
 
Naomba tiba ya ugonjwa wa kwikwi
Kwikwi ni involuntary action inayotokea kunapokuwa na contraction ya diaphragma muscle na vocal cords.
attachment.jpeg
attachment-1.jpeg
Kwikwi inaweza kusababishwa na vitu tofauti kama
  1. Kula kwa fujo/haraka
  2. Kinywaji cha baridi,pombe
  3. Stress
  4. Surgery
  5. Kwiwi ya muda mrefu inaweza pia aghalabu kusababishwa na vitu kama:

  • Majeraha kwenye central nervous system(mfano stroke,inflammation kwenye ubongo,brain tumor)
  • Irritation kwenye nerves zilizopo kwenye kifua zinazochochewa na pleurisy,pneumonia,heart attack,diaphramatic hernia n.k
  • Irritation kutoka kwenye tumbo inayoweza kusababishwa na cancer au billiary disease
  • Irritation kwenye nerve zilizopo kwenye koo zinazochochewa na Goiter,lymphnoma
Vipi unaweza kuondokana na kwikwi ya kawaida


  1. Kujizuia usipumue kwa sekunde kadhaa kwikwi ikikubana
  2. Kunywa glass ya maji ukiwa umeinama mbele kidogo
Kwikwi zikiwa za muda mrefu na zinazokuja mara kwa mara nakushauri ukaonane na daktari ili kupata uhakika haijachochewa na sababu nilizoziainisha hapo juu kwa wino mwekundu.
 
Hellow wapendwa,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu dawa zozote zenye active ingredients (DRUGS). Kama una maswali kuhusu matumizi yake, matumizi yake pamoja na dawa nyingine, vyakula (interactions), athari zake (side effects) au hata kama unataka kujuzwa jinsi dawa inavyofanya kazi kutibu ugonjwa!!

Karibuni sana..

Matumizi ya Bio Oil,ufanyaji wake kazi pamoja na side effects kama zipo
 
Nina tatizo la kutokwa na vipele au chunusi wakat wa ovulation na siku nikiwa nakaribia period inakuwa zaidi kama ndio nimebaleghe! Samahan naweza fanya nn kuondokana na hadha hii na type ya ngozi ni ngozi ya mafuta
Hello mkuu,
Pole kwa tatizo linalokusumbua,
Ukiwa una ovulate au kwenye siku zako za hedhi unakuwa na muongezeko/mabadiliko ya hormones mwilini kama estrogen, progesteron na testosteron.

Mayai(ovaries) kipindi hiki yanatengeneza zaidi kichocheo cha testosteron ambayo inajihusisha zaidi na chunusi.Kipindi hiki wanawake wengi wanapatwa na Premenstrual syndrome(PMS),hii inapeleka dalili kama stress/mood swings/cravings n.k.Stress/mood swings inasababisha adrenal glands zinakuwa overactive na kuzalisha zaidi homoni za kiume kuliko kawaida.

Androgens ni hormones pia zinazochochea production ya mafuta kwenye ngozi(sebaceous glands) ambayo hupelekea muongezeko wa blocked pores hatimae chunusi.

  • Since PMS inasababisha cravings jaribu kuepuka kula vitu vyenye mafuta mengi na sukari nyingi kipindi hiki kula matunda/mbogamboga (balanced diet) ili upate antioxidants za kutosha.Jijengee tabia ya kunywa maji mengi pia kama bilauri 8 kwa siku.

  • Epuka kuzigusa au kutumbua hizo chunusi,Utajiachia makovu.Hand hygiene ni muhimu.

  • Kama unapenda make ups.Hakikisha unaziondoa kabla hujalala,safisha uso na cleansers.
 
Bio oil si dawa,haina active ingredient!!!Hio ni cosmetic mkuu!!

Sawa mkuu,ila niliambiwa inaweza kuremove scars katika ngozi.Naomba kujua kama inaeffect yeyote kwa rangi ya ngozi na kama ni kweli inafanya kazi ili nijue kama naitumia au la
 
Sawa mkuu,ila niliambiwa inaweza kuremove scars katika ngozi.Naomba kujua kama inaeffect yeyote kwa rangi ya ngozi na kama ni kweli inafanya kazi ili nijue kama naitumia au la

Ndio inasemekana inapunguza ukali wa makovu,stretchmarks na kusaidia kama rangi yako ya ngozi si moja kuwa rangi moja!(balance skin tone)
 
Safi kwa kazi nzuri sana kutujuza sisi watumiani na wenye madukuduku ya matumizi ya dawa nk....

Nidadavulie hii kitu hufanyaje kazi "Anesthesia" je hutumika hospital tu au na kwa majasusi...nikipata sikia wakati wa ukombozi wa Afrika ya Kusini makabulu waliitumia kwa watu wapigania uhuru ili wavujishe siri zao za ukombozi.

Na kuna mahusiano gani kati ya kuvuuta pumzi kwa nguvu wakati unanaandaliwa na kwa hiyo kitu General Anesthesia?!
#gorgeousmimi
 
Mkuu nisaidie watu na madaktar wamekuwa wakineyeyusha, niite kuyeyushw kwa sabb sijapata mafanikio yyt, miguu kuwaka moto kwenye nyayo, hii hali hupungua au hupotea wakati wa majira ya baridi. Lakini wakati wa joto huwa miguu huwaka moto.

Sisikii hii hali nikiwa matembea au nikiwa busy na kazi.

napata usumbufu mkubwa.

asante
 
Naulizia dawa ya ugonjwa wa macho yani ukavu macho nakuwa sioni vizuri mtu anapokuwa mbali mpaka nimsogelee ndipo namtambua vizuri
 
Naulizia dawa ya ugonjwa wa macho yani ukavu macho nakuwa sioni vizuri mtu anapokuwa mbali mpaka nimsogelee ndipo namtambua vizuri
Nenda kwa daktari wa macho inawezekana unahitaji miwani.

Zipo eyedrops zinazosaidia kuondokana na macho makavu,ukavu wa macho unasababishwa na kutokuwa na production ya machozi ya kutosha mfano artelac, na kama macho makavu sana tunashauri eye gel mfano oftagel eyedrops, viscotears eye gel/drops kwasababu inafanya kazi muda mrefu na consistency ni nzito zaidi.
 
Safi kwa kazi nzuri sana kutujuza sisi watumiani na wenye madukuduku ya matumizi ya dawa nk....

Nidadavulie hii kitu hufanyaje kazi "Anesthesia" je hutumika hospital tu au na kwa majasusi...nikipata sikia wakati wa ukombozi wa Afrika ya Kusini makabulu waliitumia kwa watu wapigania uhuru ili wavujishe siri zao za ukombozi.

Na kuna mahusiano gani kati ya kuvuuta pumzi kwa nguvu wakati unanaandaliwa na kwa hiyo kitu General Anesthesia?!
#gorgeousmimi
Hello displayname,
Hakuna ulazima wa kuvuta pumzi kwa nguvu ukiwekewa anaesthetic unatakiwa uvute pumzi kawaida tu.Na si anaestethic zote zi za pumzi(General anaesthetics), kuna nyingine ni sindano na nyingine ni local anaesthetics ambazo zinafanya kazi pale zinapohitajika tu.

Na ya kuvuta pumzi ni halogens mfano isofluran au sevofluran ambayo inatoa complete anaesthetic effect kama consiousness, inarelax muslces na kuondoa maumivu vilevile.

Kawaida inachanganywa na nitrogendioxide , sedatives, opoid analgetics, na neuromuscular blockers.
Anaesthetics zipo tofauti in potency, duration of action , toxicity ,ability to penetrate the mucous membrane.

Jinsi zinavyofanya kazi ni very complicated. Nitajaribu kufafanua kwa urahisi. Most of anaesthetics are weak bases that only exits in protonated form at body pH. They penetrate the nerve in a non-ionized(lipophilic )form but one inside the axons some ionized molecules are formed and these block the Na+ channels preventing the generation of action potentials and prevent opening of h-gates(by increasing inactivation)They cause a reversible block of conduction along nerve fibers.

Kuhusu matumizi yake kwenye kuvujisha siri naweza kusema unwanted effect inaweza kutumika.One of the side effect is on the central nervous system it produces sedation, light headedness,haswa kile kipindi ambacho unaamka unakuta mtu anabwabwaja tu kwasababu unakuwa half consious au anaesthetic kama Ketamine ni mojawapo ambayo haitumiki sana siku hizi lakini inaweza kusababisha vivid dreaming, illusions, extracorporeal experience.

Wanaopatiwa anaesthetic hii wanakuwa macho na wanaweza kucontrol baadhi ya reflexes za kimwili.
 
Hellow dr.. Natumia miwani na nna myopia, natamani kuacha kuvaa miwani na nione vizuri kama zamani, je nifanyaje nipone? Au nitumie dawa gani? Asante
 
Hello displayname,
Hakuna ulazima wa kuvuta pumzi kwa nguvu ukiwekewa anaesthetic unatakiwa uvute pumzi kawaida tu.Na si anaestethic zote zi za pumzi(General anaesthetics),kuna nyingine ni sindano na nyingine ni local anaesthetics ambazo zinafanya kazi pale zinapohitajika tu.Na ya kuvuta pumzi ni halogens mfano isofluran au sevofluran ambayo inatoa complete anaesthetic effect kama consiousness,inarelax muslces na kuondoa maumivu vilevile.Kawaida inachanganywa na nitrogendioxide ,sedatives,opoid analgetics,na neuromuscular blockers.
Anaesthetics zipo tofauti in potency,duration of action ,toxicity ,ability to penetrate the mucous membrane.
Jinsi zinavyofanya kazi ni very complicated.Nitajaribu kufafanua kwa urahisi.Most of anaesthetics are weak bases that only exits in protonated form at body pH.They penetrate the nerve in a non-ionized(lipophilic )form but one inside the axons some ionized molecules are formed and these block the Na+ channels preventing the generation of action potentials and prevent opening of h-gates(by increasing inactivation)They cause a reversible block of conduction along nerve fibers.
Kuhusu matumizi yake kwenye kuvujisha siri naweza kusema unwanted effect inaweza kutumika.One of the side effect is on the central nervous system it produces sedation,light headedness,haswa kile kipindi ambacho unaamka unakuta mtu anabwabwaja tu kwasababu unakuwa half consious au anaesthetic kama Ketamine ni mojawapo ambayo haitumiki sana siku hizi lakini inaweza kusababisha vivid dreaming,illusions,extracorporeal experience.Wanaopatiwa anaesthetic hii wanakuwa macho na wanaweza kucontrol baadhi ya reflexes za kimwili.

Thanks
Yeah nina uzoefu kidogo...mara ya kwanza nazinduka (huwa wanafanya kitu ili urudi concious au) nilikuwa na bwabwaja tu maneno mengimengi.

Atemp ya pil naambiwa nilksumbua sana na nikawa na nguvu za ajabu sana nikazuiliwa na watu walioahiba wa tatu....after nikajikuta namaumivu kwenye shingo, mbavu nk yaliyotokana na kukabwa.

wakati ufahamu warudi. Thanka at least nina clues how GA is function
 
Hello mkuu,
Gonadotropes(GONADOTROPIN-RELEASING HORMONE)GnRH ni hormone inayozalishwa kutoka kwenye anterior pitutiary iliyopo kwenye hypothalamas(ubongo).Gondotropes inatoa vichocheo vinavyofanya kazi kwenye mfumo wa uzazi wa kike(ova) na wa kiume(testes).FOLLICLE STIMULATING HORMONE(FSH) ni hormone mojawapo inahusika uzalishaji wa mbegu za kiume.LUTENIZING HORMONE (LH)ni hormone nyingeneyo inayochochea interstital cells of leyding zilizopo kwenye testes kusecrete testosterone(hormone ya kiume).
Azoospermia ni ugonjwa unaotokea pale mwanaume anapokuwa hana sperm count zinazohesabika kwenye semen.Huu ugonjwa umegawanyika kwenye makundi makubwa matatu
  1. Pretesticular azoospermia:Kundi hili wanakuwa na hypogondatrope hypogonadisme ambapo hawana release ya kutosha ya gonadotropin-releasing hormone kutoka kwenye ubongo.Wanakuwa na low levels ya FSH,LH na testosterone.Tiba ni kwa gonadotropinderivates/analogue.
  2. Testicular azoospermia:Kundi hili aidha kuna abnormality kwenye testes,mapungufu kwenye uzalishaji wa mbegu za kiume au hata kutokuwepo uzalishaji kabisa.Level za FSH/LH zinakuwa juu na kusababisha Hypergondatrop hypogonadism.Abnormality kwenye testicles inasababisha mbegu kutoweza kupevusha ipasavyo.Testicular retention ni sababu nyingeneyo ambayo watoto wa kiume wanazaliwa nayo.Geminal cells zipo sensitive na temperature na ndio maana mbegu zinakuwa defect na kuharibika kabla hazijafika kwenye korodani.
  3. Posttesticular azoospermia:Kundi hili wanatengeneza mbegu lakini hazitoki through ejaculation.Na wapo wanaozaliwa na mapungufu ya vas deferens(njia ya kutolea ejaculation)(Congenital bilateral absence of the vas deferens) au retrograd ejaculation ambapo mbegu za kiume baada ya kwenda kwenye urethra zinaenda kwenye urinary bladder na kusababisha mbegu kuwepo kwenye mkojo.Tiba ni dexbromfeniramin kwa wenye retrograd ejaculation.
View attachment 240208
View attachment 240194
**Anejaculation:ni uwezo wa kutozalisha mbegu kwa wanaume
**Orichitis:Inflammation kwenye testes inayosababishwa na infection kama STD´s n.k
**Vasectomy:Njia ya kufunga kizazi kwa wanaume
**Epididimytis:inflammation kwenye eneo ambazo mbegu za kiume zinazalishwa na kuegeshwa.Inasababisha maumivu,kuvimba na korodani kuwaka moto.
View attachment 240203

Pretesticular na posttesticular azoosermia vinarekebisihika lakini testicular ni irreversible and permanent.Tiba mojawapo ni kwa IVF(In vitro fertilization) + ICSI(Intro cytoplasmic sperm injection).Ambapo mbegu zinachukuliwa kutoka kwenye testicles na kutumika kuegesha ujauzito.

Mkuu ahsante kwa maelezo yako ya kina, je, hapa nchini ni hospitali ipi ambayo naweza kufanyiwa uchunguzi wa kina wa kimaabara, mbali ya muhimbili?

Pia suala la kuzidi, kuwa chini ama katika kiwango cha kawaida kwa vichocheo lina tambulika vipi?mbona viwango kwa kiasi kikubwa vipo in a required range mfano testosterone ranges from 1.9-15ng/ml na majibu yangu ni 6.36ng/ml ama kuna tatzo jingine sambamba na hilo? tafadhali.
 
Back
Top Bottom