Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Kuna mtu nimemjibu kuhusu oligomenorrhea ambayo ipo classified kama amenorrhea isipokuwa amenorrhea inaweza kuanzia miaka 16 na hedhi inaweza ipotee zaidi ya miezi 6.Na jinsi inavyosababishwa nimeandika pia.Nikagusia polycystic ovarian syndrome(kupata viuvimbe/cysts vingi kwenye mayai) ambayo husababishwa na kuongezeka/disturbance ya homoni ya kiume(androgens) ambayo husaabishwa pia imbalance ya homoni nyingine kama estrogen. Hii hupelekea msawajiko ktk mfumo wa hedhi,kuota kwa ndevu au vinyoleo kwa wanawake,matatizo kwenye mfumo wa uzazi na hata kisukari(Diabetes Type II).Hali hio hujitokeza kipindi cha balehe mpaka miaka 19 na watu wenye tatizo hili mara nyingi wanasumbuliwa na uzito vilevile.
Tiba ni tofauti:

  • Kama unataka ujauzito ni clomifen.

  • Kupunguza male characteristics vidonge vya uzazi wa mpango vinaweza kutumika mf ethinylestradiol(vinasaidia kuweka sawa mfumo wa hedhi,NB:inachukua miezi 8 mpaka uone mabadiliko) au spironolactone(aldactone) na dexamethasone ili kupunguza production ya homoni za kiume.
  • Kama una kisukari dawa za kisukari zinahusika mf metformin/Glucophage.Hizi itasaidia kucontrol kisukari na kupunguza uzalishaji wa homoni za kiume,kuuweka mfumo wa hedhi sawa,na hatimae kuongeza possibilties za kupata ujauzito.

Dr naomba kujua dawa ambazo zinaongeza hormone za kiume na side effects Zake, shukurani
 
Pole na majukumu mimi naomba kujua tatizo la mtu kutokwa na jasho jingi husababishwa na nini au ana tatizo gani?
 
Hellow wapendwa,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu dawa zozote zenye active ingredients (DRUGS). Kama una maswali kuhusu matumizi yake, matumizi yake pamoja na dawa nyingine, vyakula (interactions), athari zake (side effects) au hata kama unataka kujuzwa jinsi dawa inavyofanya kazi kutibu ugonjwa!!

Karibuni sana..

Natanguliza shukrani kwa msaada unaotoa kwa jamii. Nina tatizo la kutoka vipele sehemu za mikono na miguu, vikipasuka vinakauka na hiyo sehemu inatoa alama kama ya mapunye (mduara)

Je mapunye hutokea sehemu yoyote ya mwili ukiacha kichwani? Na dawa gani inaweza kunisaidia?
 
Nadhani tatizo lako unalijua mkuu...Unakuwa una anxiety na una stress jamiiana kabla?Hali hii ilishajitokeza au inajitokeza kwasababu hamjawahi kukutana kimwili!![/

hiyo anxiety sijajua maana yake na je, kuna dawa ya kukabiliana na hiyo hali
 
Nilienda kupima mkojo dr akaniambia ninabakteria na wameanza kushambulia figo,amenipa doxy za siku tano,je nitapona kwa hii dawa? Naomba Msaada wa tiba nyingine pia. Asante
 
Dr nina tatizo la malaria nimetumia dawa ya mseto mwishoni mwa mwezi february 2015 nimepima tarehe 15 March nimekutwa tena na malaria na nimerudia dawa hiyo ya mseto tena
Kwa sasa sijisikii vzr !kichwa kinauma na viungo vinauma pia
Dr naomba ushauri wako-nifanyeje na nitumie dawa gani kukabiliana na tatizo hili
Nashukuru sana
 
Nilienda kupima mkojo dr akaniambia ninabakteria na wameanza kushambulia figo,amenipa doxy za siku tano,je nitapona kwa hii dawa? Naomba Msaada wa tiba nyingine pia. Asante
Sijawahi kuona doxylin ikitumika kwaajili ya infection kwenye mkojo/mafigo.Sijui daktari alokupatia tipa amechukua maamuzi hayo kwa minadhili gani lakini nakushauri uendelee na tiba ulopatiwa since umeshaanza.Dawa inayotumika kwa tatizo ulonalo ni trimetoprim-sulfametoxazol(septrin) au flourokinoloner kama cirpofloxacin au cephalosporines mf cefalaxin,cefuroxim n.k na tiba inatakiwa iwe ya siku 7-10.
 
Ugonjwa wa endomestrium dawa yake ni nini
Tiba ya Endometriosis ni aidha
  • Progestin ,progesteron,noretisteron au
  • Gonadotropins releasing hormones agonists(buserelin,degarelix,histrelin,nafarelin n.k
  • Njia ya uzazi wa mpango monophasic birth control pills(ina mchanganyiko wa progestin + estrogen) mf Yasmi
 
Dr naomba kujua dawa ambazo zinaongeza hormone za kiume na side effects Zake, shukurani
Athari ziko tofauti mkuu kutokana na aina ya tiba unayopata,muda wa tiba,umri wa muhusika na jinsia.Nakuorodheshea athari zinazoweza kuwapata jinsia ya kiume:
  • Chunusi ni side effect mmojawapo ya kawaida
  • Salt and water retention,inaweza kusababisha muongezeko wa mwili hasa mwanzoni mwa tiba na hata wa madini ya calcium mwilini
  • Mabadiliko kwenye gender character na sexual impairment:Hii inaweza kuuwa direct and indirect impairment ya kwenye genitals na kwenye mfumo wa uzazi.Mfano direct stimulation inaweza kusababisha prostatic hypertrophy na hata kusababisha prostate cancer.High doses inaweza kusababisha uume kusimama muda mrefu na kuuma (priapism).Extreme high doses zinasababisha pia release ya gonadotropin kuzuilika kutoka kwenye pitutary gland na kupelekea mapungufu kwenye uzalishaji wa mbegu za kiume na hata ugumba.
  • Athari zinaweza kwenda vice versa pia na kusababisha feminism mfano gynecomastia(kuota kwa matiti kwa wanaume.Hii inasababishwa na kuvunjwavunjwa kwa androgens kwenda kwa estrogen ambayo inachochea ukuaji wa matiti.
  • Alopeci ni athari nyingine:Huu ni ugonjwa wa kukosa vinyoleo mwilini
  • Mabadiliko ya kisaikolojia ni kawaida:Kuongezeka kwa ham ya kukutana miwili au kupungua(libido)
  • Psychotic reactions kama depression,aggression kwa utumiaji ulokithiri
  • Hepatotoxicity(sumu kwenye ini)
  • Matatizo kwenye moyo,inaongeza LDL-cholesterol,inaweza kusababisha heart attack ukizidisha matumizi
  • Hematological changes:Kuongezeka kwa chembechembe nyekundu za damu.Na hii inasababishwa na uwezo wa androgen kustimulate erythopoesis.
  • Kuongezeka kwa misuli na hii huweza kusababisha rupture kwenye misuli .Chronic fibromyalgia
 
Dr nina tatizo la malaria nimetumia dawa ya mseto mwishoni mwa mwezi february 2015 nimepima tarehe 15 March nimekutwa tena na malaria na nimerudia dawa hiyo ya mseto tena
Kwa sasa sijisikii vzr !kichwa kinauma na viungo vinauma pia
Dr naomba ushauri wako-nifanyeje na nitumie dawa gani kukabiliana na tatizo hili
Nashukuru sana
Zinaweza kuwa athari za kawaida za dawa ambazo zinapotea ukimaliza tiba.Maliza tiba kisha utazame kama hali hio bado inaendelea!
 
Nadhani tatizo lako unalijua mkuu...Unakuwa una anxiety na una stress jamiiana kabla?Hali hii ilishajitokeza au inajitokeza kwasababu hamjawahi kukutana kimwili!![/

hiyo anxiety sijajua maana yake na je, kuna dawa ya kukabiliana na hiyo hali
Anxiety ni kama uoga au hofu flani.Tatizo lako ni la kisaikolojia zaidi.Hali hio imeanza hivi karibuni au ulikuwa hivo wakati wote??
 
Nutritionists watakuwa na ujuzi zaidi wa hili au trainers!!Kwa watu wanaofanya mazoezi makali hawahitaji zaidi 2g per body weight of protein per day.Ukitumia zaidi ya kiwango hiko hutanufaika na chochote.Ni muhimu pia ukitumia vyanzo asilia vya protein kama nyama,samaki,kuku,mayai n.k
Ni muhimu pia kula vitu vyenye protein kabla na baada ya mazoezi changanya na carbohydrates + maji ya kutosha,kwasababu carbohydrates(mf mtindi/peanutcream/mkate) inaongeza release ya hormone ya insulin mwilini ambayo inasaidia misuli kuchukua amino acids kutoka kwenye proteins.
Ukizidisha kiwango cha protein kukithiri haswa inaongeza risk ya mtu kupata matatizo ya moyo na high cholesterol.

​Mkuu asante sana nimekupata vilivyo ntafanyia kazi ushauri wako shukran May God Grant More skills Mkuu
 
Back
Top Bottom