Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

habari zenu wanajf wote...
Doctor naomba msaada wako katika swala lifuatato
mwanamke kafanya mapenzi akiwa katika period ya menstruation sasa damu zinakata mara baada ya siku kadhaa zinatoka tena na inakuwa mara kwa mara ..... je kunanjia ya kuliondoa tatizo hilo?
kama ndio ni kwa namna gani?
msaada wako tafadhali
Nice time Doctor

Kama hali hio imetokea mara moja tu menstruation cycle itarudi tena na kuwa hali yake ya kawaida baada ya muda.

Hauhitaji tiba kwa sasa ila hali hio ikiendelea muda mrefu namshauri akaonanae na daktari.
 
Ukiwa unatumia antibiotic ni muhimu umalize cure yote.Ni kawaida ukianza matumizi y.Unatatizwa na athari gani ya ampiclox?
tumbo kuuma,kuhara,kupatwa na kichechef au hata kutokupata choo.
 
naomba msada kupunguza unene na kutoa kitambi kwa njia rahisi na za kisasa tahadhari
 
Hi Dr., nina tatizo la kuumwa na kichwa sana hasa nyakati za joto na jua hata kama sio kali. Nini dawa yake.?
 
GOOGLE,Hizo athari unazozipata ni za kawaida ukiwa unatumia antibiotic cure...Zitakwisha ukimaliza dawa na kama ungependelea kumantain unaweza kula lactic acid bacteria capsules ukiwa kwenye antibiotic cure ili kubalance hao bacteria wazuri waliyopo tumboni.

Nimeandika hilo kwenye ule uzi nilokupa link.

Naomba urudi ukausome!!
 
Last edited by a moderator:
mabesela,Nakushauri ukaonane na daktari unasumbuliwa na tatizo linaloitwa migraine, Kuna sababu tofauti zinazoweza kutrigger migraine na mwanga ni mmoja wapo,Watu wanaopatwa na tatizo hilo hawapendi kuwa kwenye eneo la mwanga kwasababu linaongeza maumivu ya kichwa.

Nakushauri uanze kula painkillers za kawaida kama paracetamol 500mg na ibuprofen 400mg, kula vidonge hivyo kwa pamoja.

Kama hutopata nafuu kuna group la dawa zinazoitwa TRIPTANS ambazo zinaweza kutumika.Kila la kheri mkuu
 
Last edited by a moderator:
Dr dawa sahihi ya uti kwa mtoto wa miezi 4 ni ipi? Pia anachubuka ktk ya mapaja nimpake nini coz wanasema poda sio nzur,
 
Chelea,Mboga ya majani ya spinachi inasaidia kuongeza madini ya chuma mwilini na madini hayo ndio yanahusika na kuongeza kiwango cha damu.

Nyama nyekundu na maini pia ni chanzo kizuri cha madini ya chuma.Tunda kama zabibu ni chanzo kizuri pia cha madini ya chuma. Matunda ambayo yapo rich in Vitamin C hapa namaanisha citrus fruits kama machungwa,machenza n.k yanasaidia kuongeza absorption ya iron ni vyema ukila vitu hivo pamoja na msosi uliokuwa rich in Iron.
 
Last edited by a moderator:
sawa naomba nijue mazoez gani na vyakula gani

  • Vyakula kama mboga za majani na matunda vina fibers nyingi.
  • Proteins kama samaki na nyama nyeupe (mfano kidari cha kuku) au kama nyekundu mfano filet/biff ni nzuri.Ni vyema vyakula hivi kuliwa vikiwa vimechemshwa au vimechomwa epuka kula mikaango.
  • Epuka kula nafaka zilizokobolewa mfano vyakula vinavyotengenezwa kutoka kwenye unga mweupe wa ngano kama loff bread n.k.
  • Vyakula vya jamii ya kunde ni vizuri mfano maharage,choroko,mbaazi n.k.
  • Epuka kula vyakula vyenye starch nyingi mfano viazi na mihogo
  • Epuka kula refined sugars..kula matunda yana sukari asilia,Ukinywa chai usitumie sukari!
  • Hakikisha ukila unagawa portion ya 1/3 kwenye sahani mfano 1/3 mboga,1/3 protein na 1/3 carbohydrate.
  • Kunywa bilauri mmoja ya maji kabla ya milo.
  • Usile masaa 3 kabla ya kulala.
  • Kula milo 3-4 kwa siku
  • Mazoezi unayoweza kuanza nayo ni simple jogging na ukitaka kujenga misuli nenda gym watakupa muelekeo zaidi.
 
Dr dawa sahihi ya uti kwa mtoto wa miezi 4 ni ipi? Pia anachubuka ktk ya mapaja nimpake nini coz wanasema poda sio nzur,
Ni aghalabu kwa mtoto wa miezi 4 kupata UTI nakushauri ukaonane na daktari atakupatia tiba sahihi...dawa ni kama za wakubwa lakini dosage inakuwa ya watoto na formulation inakuwa inayoweza kutumika kwa watoto mfano kimiminika.

Kwa michubuko kwenye mapaja inaweza kutumika zimc oxide ointment/cream itakuwa na msaada mkubwa!
 
naomba kujuzwa madhara ya kutumia dawa za uzaziwa mpango kwa m2 ambaye hajazaa .
pia naomba kujua madhara ya kutumia condom kila mara
Condom haina madhara.
Njia za uzazi wa mpango zina athari tofauti kutokana na muhusika anayetumia na aina ya dawa unayotumia.

Kawaida athari zinajitokeza mwanzoni na kupotea baada ya muda. Athari za kawaida ni irregular menstruation, kuongezeka kwa uzito, maumivu ya kichwa, mood swings, kupungua kwa hamu ya kujamiiana, maumivu ya matiti, mabadiliko kwenye ngozi ambayo ipo exposed na jua inafanya ngozi kuwa hypersensitive na kuongeza risk ya pigments kwenye ngozo,risk ya kupata tromboembolism(chance kubwa ni kwa kurithi), inaweza vilevile kuwa na athari kwenye mifupa.
 
Vyakula kama mboga za majani na matunda vina fibers nyingi.Proteins kama samaki na nyama nyeupe (mfano kidari cha kuku) au kama nyekundu mfano filet/biff ni nzuri.Ni vyema vyakula hivi kuliwa vikiwa vimechemshwa au vimechomwa epuka kula mikaango.Epuka kula nafaka zilizokobolewa mfano vyakula vinavyotengenezwa kutoka kwenye unga mweupe wa ngano kama loff bread n.k.Vyakula vya jamii ya kunde ni vizuri mfano maharage,choroko,mbaazi n.k.
Epuka kula vyakula vyenye starch nyingi mfano viazi na mihogo
Epuka kula refined sugars..kula matunda yana sukari asilia,Ukinywa chai usitumie sukari!
Hakikisha ukila unagawa portion ya 1/3 kwenye sahani mfano 1/3 mboga,1/3 protein na 1/3 carbohydrate.Kunywa bilauri mmoja ya maji kabla ya milo.Usile masaa 3 kabla ya kulala.
Kula milo 3-4 kwa siku
Mazoezi unayoweza kuanza nayo ni simple jogging na ukitaka kujenga misuli nenda gym watakupa muelekeo zaidi.

asante sana naanza leo
 
Back
Top Bottom