Hellow wapendwa,
Nakaribisha maswali yoyote kuhusu dawa zozote zenye active ingredients (DRUGS). Kama una maswali kuhusu matumizi yake, matumizi yake pamoja na dawa nyingine, vyakula (interactions), athari zake (side effects) au hata kama unataka kujuzwa jinsi dawa inavyofanya kazi kutibu ugonjwa!!
Karibuni sana..
Dr shukrani kwa ushauri huu mzuri
Nina tatizo la kuwashwa kwenye kichwa, kwa sehemu kuna mba ila pia kuna viupele vidogo vinavyotoa maji na usaa,kuwashwa huku pia kuko kuzunguka masikio ambapo vipo viupele vinavyowasha, kwa mwonekano ni vyekundu, mpaka sasa nimetumia dawa za kupata Senoderm na Gentrisone bila mafanikio, nikitumia Senoderm viupele vinapotea hata kwa wiki then vinarudi upya
Dr naomba ushauri wako nifanyeje kutibu tatizo hili,