Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Dr naomba ufafanuzi juu ya hili, inawezekana MTU akawa mjamzito halafu akawa anaziona siku zake kama kawaida?

hilo haliwezekani mkuu... maana tayari kitakuwa na mabadiliko ya homoni, progesterone inakuwa high ili kushikiza mimba... ikitokea tatizo ikashuka basi mimba itatoka kwa mfumo uleule wa kama mwanamke anavyopata hedhi.
 
Naomba kuuliza Dr. Kuna relation gan kat ya premature baby na kuwa intellectual coz watu kama Newton, eastern, ect wote n premature
 
Dr nomba unisaidie dawa ya kuweza kutibu/kuondoa kisunzua(sina hakika kwa jinalake kama ni sahihi maana ninafahamu kwa hilo jina) kimeota kwenye shingo. Nimejaribu kwenye pharmacy mbalimbali nikapewa dawa flani ya kupaka iko kama acid hivi kama pencil. Lakini baada ya muda mfupi kinaota tena. Nilivyoenda hospital nimeambiwa kufanyiwa operation kitu ambacho sijaafiki kwanya. Previously kama 2001 kiliniota kwenye kidole mguuni lakini nilipatiwa na kikapotea hadi leo. Msaada please.

Kama caustic pencil haikukusaidia nenda hospitali tena sio lazima ulipoenda mwanzo huwa wanavikata. Pia kuna saloon moja iko posta ya wathailand jina sasa ndo sikumbuki wanatoa kwa mionzi tena wala sio ghali
 
Hellow wapendwa,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu dawa zozote zenye active ingredients (DRUGS). Kama una maswali kuhusu matumizi yake, matumizi yake pamoja na dawa nyingine, vyakula (interactions), athari zake (side effects) au hata kama unataka kujuzwa jinsi dawa inavyofanya kazi kutibu ugonjwa!!

Karibuni sana.
 
Mimi nahitaji kujua kuhusu mafuta ya nyonyo kwenye tiba ya genital warts
 
Ndo genital warts hizohizo

Dear kwa genital warts ni vizuri ukaenda kuzitoa hospitali hasa kama vineota vingi, na ili zisijirudie mchunguze na mwenzio nae kama anazo atibiwe pia.. Lakini kama ndio zinaanza kanunue caustic pencil pamoja na vaseline kisha upake mafuta kuzunguka visunzua kisha uichovye kwenye maji penseli yako na uweke eneo husika, vitaisha vyote. Kwasababu vipo sehemu za siri kama huwezi kujitibia mwenyewe muombe mtu akusaidie. Be careful na usisahau hii caustic pencil ni kwa matumizi ya nje tu.
 
Ahsante and what if nikipata podophyllin?
 
Ahsante and what if nikipata podophyllin?

Podophyllin siifahamu. Hiyo niliyokutajia ilinitibu mimi mwenyewe, nilikuwa na warts usoni ila nakusisitiza kwa kesi yako kujua ulizipata wapi ikiwezekana mtibiwe wote na aliyekuletea au uache kushirikiana nae vinginevyo kuna Hatari zikakupata tena

Warts ikikupata sehemu nyingine inakuwa ugonjwa wa kawaida ila ikiwa una genital warts basi hapo inakuwa ni sexual desease.

Kwa kifupi warts zinasababishwa na virus ila hao virus wanaishi kwenye ngozi hivyo tiba nzuri ni ya kuunguza eneo husika pia kuna mionzi maalum kwenye saloon za Wathailand kwa Dsm kuna moja ilikuwa posta maeneo ya bot sijui kama bado ipo au la na pia kuna dawa maalum za kuunguza mfano wake ndo hiyo caustic pencil. Na hospitali huwa wanaziunguza au wanakata inategemea na dr alivyoona tatizo lako

Unaweza kugoogle pia ili uweze kuelewa vizuri
 
Naomba kuuliza Dr. Kuna relation gan kat ya premature baby na kuwa intellectual coz watu kama Newton, eastern, ect wote n premature

hakuna uhusiano wa moja kwa moja mkuu. vipi kina Mendeleev, Galileo, Faraday hawakuzaliwa hivyo lakini ni ma-genius
 
Naomba ushauri wako, nina tatizo la fungus kwenye makorodan, nimeshaenda hospital 3 nikitumia dawa zinapoa ila nikimaliza ugonjwa unarud, nimeenda kwa masai kanipa dawa nimetumia ikatulia kw muda dawa kuisha ugonjwa umerud tena, nikajaribu tiba ya vitunguu swaumu ambayo niliitoa humu jf lakin bado, naomben ushauri zaid nifanyeje au hivyo vitunguu nilikosea kutumia???
 
Mwaka 2013 December karibu na mwaka mpya nilishikwa maumivu makali katika yangu ya kulia nilienda haspitali ila wakaniuliza kama nimeshawahi kusex hv karibun,wakanipa madawa ya pink ambayo nlitumia sku 2 bila kuona dalili zozote za kupona.Shemeji yangu alinipa dawa ya miti shamba nkatumia haikunisaidia,hadi nilipoenda kwa bibi yangu tengeru sku ya pili alinichemshia dawa na asubuhi ya siku ya tatu nlipona kabisa.alinisisitizia niendelee kuitumia maana inatibu vitu vingi.Siku moja moja nlikuwa natoa uchafu ninapokojoa,uchafu kama manii hv ila skuwa na maumivu,Baada ya sku kupita nikagundua hili pumbu linapungua ukubwa na linakuwa gumu bas nikaendelea na ile dawa ila pumbu lilipungua hadi saiz ya gololi za watoto wanazochezea.Wakati huu nilikuwa naskia maumiv kidogo ya sekunde kama 30 hv upande wa pumbu ambayo haikuugua.nilisoma internet na kujua tatizo langu ni ngiri ila nilikuwa na matumaini kwa sababu nasex na mpenzi wangu ninatoa manii na ninamridhisha.ila jana usiku nilikuwa nina ham ya kufanya mapenzi sana ilipofika mida ya saa 5 usiku huku uume ukiwa umeamka niliskia yale maumivu nliyopata mwanzon kama yanaanza kuja taratibu upande wa pumbu la kushoto ambalo halikuugua.Watu wengi wananiambia hospitali hamna dawa zaidi ya kufanyiwa upasuaji.NAOMBENI USHAURI WENU PLEASE
 
Naomba kujua mvulana atakumbwa na matatizo gani endapo Kama hajawahi shiriki tendo la ndoa na umri ni miaka 25 na kuendelea?
 
naomba mnisaidie kuna blood group yeyote ukiwa nayo ni mbaya maana nashangaa kuna mtu ukimwambia blood group yako kama kijana anakushangaa
 
Back
Top Bottom