Gorgeousmimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2010
- 9,296
- 7,683
- Thread starter
- #1,541
Ametumia dawa ya aina gani?Ni kawaida kwa baadhi ya watoto walozaliwa premature kutatizwa na asthma!Je amechekiwa hio?Mtoto wangu alizaliwa kabla ya muda alopaswa kuzaliwa. Madaktari walisema yupo sawa hana shida yoyote. Tulikaa hospitali kwa wiki tatu tukaruhusiwa kurudi nyumbani. Awali alikua sawa kabisa na ukuaji wake upo vizuri Sana na sio rahisi mtu kujua Kama alizaliwa njiti ukimwona sasa. Ila baada ya kufikisha miezi minne alianza kukohoa kikohozi kikavu, mwanzoni tulidhani ni kawaida tukaenda hospitali akapewa syrup za kikohozi kikawa kinapoa na baada ya muda kinarudi palepale. Sasa ana miaka miwili na miezi mitano, tumeenda hospitali kubwa Hadi ultera sound zimefanyika wanasema hakuna tatizo. Anaongea, Ni mchangamfu Sana na hana shida nyingine yoyote isipokua hiki kikohozi kikavu na kisichopona. Tumeshapewa dawa nyingi lakini hajawahi pona akaacha kabisa kukohoa.
Hii inaweza kuwa Ni shida gani na nifanye Nini mwanangu awe aondokane na shida hii.