Nakataa Sera ya Elimu kubadilishwa na namuomba Rais Samia asiikubali

Nakataa Sera ya Elimu kubadilishwa na namuomba Rais Samia asiikubali

Nyie wakufunzi mmeambiwe muwe na masters naona hiyo imekupanikisha🤣🤣🤣, mko makazini mnabweteka mkijifariji kuwa kujiendeleza kielimu ni anasa Sasa mfumo utawatoa kwa lazima.
POLE SANA MKUU
 
Kichaa hakiponi huwa kinatulia kwa muda tu.

Mtoa mada hali yake inajulikana avumiliwe.
 
Mfumo wa Elimu wa sasa haujalisaidia Taifa kwa miaka 60 halafu bado mnataka usibadilishwe?...Hivi hamuoni athari zake kwa wasomi wetu?
MSOMI ZAO LA MFUMO WA SASA
1.Wezi wakubwa wanaibia Taifa lao wenyewe
2.Wengi hawana uzalendo na upendo kwa raia wenzao wanaowategemea wapate huduma kutoka kwao
3.Wengi hujawa na ubinafsi na kiburi na mwisho hujitenga na jamii isiyo na elimu inayofanana na wao
4.Wasomi wengi ni tegemezi sana kwa Serikali...bila Serikali kuwaajiri ndoto zao hufa kabisa..(Hawaiingizii Serikali mapato kwa kupitia taaluma zao)
5.Inazalisha watu wenye majivuno sana
6..Wasomi wengi hubadilika sana kimila na tamaduni zao,hata kama ni nzuri
7.Wengi hawapendi Manual work(hii ilianzia Secondary,mzazi hutengeneza kibali feki cha Daktari ili mwanae asifanye manual work)
MWISHO...Kumbuka Tanzania ina umri wa miaka 60 sawa na mataifa ya Pakistan,Indonesia,Malaysia,Vietnam,Mynmar/Burma,China nk..lakini tukilinganisha level za maendeleo kiuchumi kati yao na wao,utajiuliza kwanini sisi?....Kwangu, mabadiliko ya mfumo wa Elimu yetu ni muhimu sana...
 
Mda wa kutumia walimu wa certificate ndo janga linapoanzia. Hawafai kwa Sasa.Napendekeza waondolewe wote na nafasi hizoo wapewe level za Diploma na Degree kwa SM.............
 
Kama Mdau Tukuka wa Elimu, Mkufunzi na mwana Saikolojia nakataa kuwa Tatizo la Elimu ya Tanzania ni Mfumo.

GENTAMYCINE nimewavumilieni na huu Upuuzi wenu usiovumilika wa kutaka Kubadili Mfumo wa Elimu ya Tanzania na leo nawatoleeni Uvivu.

Tatizo siyo Mfumo wa Elimu uliopo kwani hata akina GENTAMYCINE na Wengineo tumeupitia huo huo na kuwa na hizi Akili Kubwa sasa iweje leo muukatae kwa Hoja zenu za Kipuuzi / Kipumbavu?

Ni hivi tatizo siyo huu Mfumo mnaohangaika nao bali Tatizo Kuu na Sugu ni kutokuwa na Walimu Mahiri na Mitoto mingi inayozaliwa na Ujuha ( Uzuzu ) mwingi kutokana na kupata Lishe Duni inayopata kutoka kwa Waliokurupuka Kuwazaa.

Najua kwakuwa Bunge letu la sasa lina 90% ya Wabunge hovyo hovyo ( Mazuzu ) na Wenye Unafiki mwingi watakubali Kuupitisha huu Upuuzi wao ila Mheshimiwa Rais Samia nakuomba sana usikubali Kuusaini bali uendelee huu huu ulioko na uliotukuza Sisi akina GENTAMYCINE bali Mapungufu hayo Mawili niliyoyataja yafanyiwe Kazi.

Na Rais nae akidanganywa na Kushawishiwa na Wanafiki wa Bungeni na Wanaomzunguka kisha akausaini kuwa Mfumo Kamili GENTAMYCINE nitamdharau mpaka Kiama na hata Kura yangu Tukuka ya 2025 kama atagombea/ akigombea hatoipata.

Nimemaliza.
Naunga mkono hoja! Elimu imeharibiwa na wanasiasa kutaka ufaulu uongezeke ili wapate sifa…..
 
Back
Top Bottom