Nakemea vikali hoja ya kuwa walimu wa msingi kuwa walifeli kidato cha nne

Nakemea vikali hoja ya kuwa walimu wa msingi kuwa walifeli kidato cha nne

hawadharau ila mfumo ndo unaudhalilisha ualimu
serikali ingekua inachukua wenye division four kuwapeleka advance halafu div.one ualimu na mshahara heavy ungedharaulika kweli
hebu nipe mfano wa mtu mmoja aliyepata div one akaenda ualimu wa certificate
 
Nani kawaambia hayo? wengine tulifaulu vzr fm 4 na tulikuwa na sifa za kujiunga "A" level ila kwa hiari zetu tukaenda teaching as a right way of achieving triumphs,sasa wale wanaobwatuka2 eti wlm wa pr. walifeli mthn wa fm 4 wafunge bakuli lao.

Samahani mkuu ila nitaeleza kwa uzoefu wangu,
Nilipomaliza kidato cha nne kuna rafiki zangu wanne walijiunga sehemu hizi
Msichana mmoja alipata div 4 ya 26 kwa sasa ni askari polisi yuko Bukoba, jamaa mwingine alipata div 4 ya 30 nae ni askari polisi yuko Tabora, mwingine room mate wangu alipata div 4 ya 29 kwa sasa ni askari magereza huko bukoba, jamaa mwingine alipata div 4 ya 27 kwa sasa ni askari jeshi yuko monduli arusha.
Nirudi kwenye mada wanafunzi wengine wapatao sita walipata div 4 ya 26-27 kwa sasa ni walimu wa shule za misingi sehemu mbalimbali.
Kwa wanafunzi waliofaulu kuanzia div 3 ya 25 hadi div 1 watatu wamemaliza UDSM, na mmoja kati yao bado anasoma Telecommunication engineering ndo anaanza mwaka wa mwisho chuo kikifungua tarehe 20October.
Mwingine kati ya hawa waliofaulu amemaliza SUA BSc.in Food science.
Najiuliza kwanini hizi takwimu ziko hivi??
Ukipata jibu utaamini kwamba waliofeli wengi wao ndio hujiunga na ualimu wa shule ya msingi.
Kwa kawaida mtu anayejiunga na hizo nafasi wakati elimu yake ni ya kidato cha nne hua darasani ameharibu, ikiwa kuna taarifa ya mwanafunzi aliyewahi kupata credits (div 1-3 nzuri) na bado akajiunga huko basi atujuze kwa uthibitisho.
 
kuna mwalimu wa shule ya msingi alijiendeleza kusoma sheria,akapiita law school akafaulu first sit,kwenye ile interview ya Takukuru wale wa Law yeye ndiye alikuwa wakwanza...huwa nikimwana namheshimu sana

Kwanini ukimwangalia unamueshimu? Inamaana alifanya jambo ambalo ni zuri kuliko ulivyotegemea na hiyo ni exceptional case, tukizungumza in terms of percent walimu wa shule ya msingi walifeli form four, huo ndio ukweli jamani.
Watanzania tumekua na kawaida ya kuukimbia ukweli kwanini, jambo liko wazi watu wanaleta malumbano ya nini sasa.
 
sikufaulu sana nilikua na dv 3 ya 23 mwaka 2003 but nilienda clash program nikaua. niaajiliwa nikapiga six kitaa nikapiga nimeenda dip nimemaliza na nna 2.8 najiandaa kuchukua shahada! afu napiga pindi darasa la tatu stadiza kazi.
Kumbe div 3 ndio kufaulu?
 
Kumbe div 3 ndio kufaulu?

Usipotoshe maana ya thread mkuu, jadili kwa kuunga mkono hoja au kupinga hoja za mtoa mada/wachangiaji sasa hapo unapoenda wewe mada itahama mtaanza kulumbana na huyo mwenye div 3
 
sio kila afundishae primary anacheti.wengine wa stashahada na shahada

Kuna bogus walioharibu mfano baraza la mitihani ndio wakawa demoted. Vinginevyo wa shahada hapaswi kufundisha primary.
 
mm nafundisha primary ila sijawahi kufeli hata siku moja.pia kufundisha primary wakat mwingine kuna family back ground au umaskin

Ulifaulu kwa kiwango gani? Kufaulu is a relative term.
 
Unajidanya ndugu mi nimefau form 4 nikaenda ualimu nikafanya form 6 nikiwa kazin pia nilifaulu nikenda dip nikafaulu nasasa nipo chuo

Ungekuwa ulifaulu form six ungeenda university moja kwa moja. Kupitia diploma inamaana hukufaulu
 
Ungekuwa ulifaulu form six ungeenda university moja kwa moja. Kupitia diploma inamaana hukufaulu

Bora umpe ukwel wake mkuu, watu hawapendi kuambiwa ukweli siku hizi mtu amefeli anaanza kutafuta maneno ya kupambapamba ili aonekane alifaulu! Lol!
Sasa mtu alikua bright iweje azunguke sana hadi kupata degree keshapoteza miaka na ela nyingi sana,
Anaanza cheti-2yrs,hiyo advanced level ya kuunga unga 1-2yrs, diploma-2yrs, degree 3-5yrs!!!!
Miaka yote hiyo ya nini??
 
Mimi ni mwalimu tena wa cheti tangu mwaka 1991.Ni mzee wa almost miaka 45.Nime experience hali fulani ya kudharau sana Ualimu.Nami nasema is well ila ina madhara makubwa sana.Kwanza inaua moyo wa kujituma miongoni mwa walimu walio wengi.Ni kweli wengi tulikosa sifa za kujiunga na kidato cha tano.Mfano mimi binafsi nilifanya mtihani Oktoba 1988 na kupata div. three points 25.Aidha nikuwa na credit 3 ila Shule za A level private nazo zilikuwa haba nakumbuka Kilimanjaro boys Rombo(W) ndo Shule pekee ya A level private Moshi.Mimi sioni haja ya kuwadharau walumu maana ndo BASIS kwa kila fani.I MEAN poor teacher produces poor Doctor,Engineer, farmer,etc.Kwa hiyo wewe unayemdharau Mwalimu pia ni ovyo maana you are a teacher product.Nitaweka uzi siku moja ole wako unayetudharau poor you!
 
Inaudhi mkuu,kuna comment fln kwenye thread ya "kuhusu teaching" mchangiaji amesema kwa wlm wa cheti ambao wamekosa sifa za kujiunga fm 5 hivyo walifeli mtihani wa fm 4

Walio wengi wamekosa sifa za kuendelea na kidato cha tano hasa credit 3.
 
Waliofeli ni wale waliopata div.0
walimu wengi wa msingi sio kwamba wamefeli bali wamekosa sifa za kujiunga na kidato cha tano na si vinginevyo,exception iko kwa wachache sana.
 
Back
Top Bottom