Nakerwa sana na haya maneno: "P,PW,K,JOMONI"

Nakerwa sana na haya maneno: "P,PW,K,JOMONI"

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,623
Reaction score
8,442
Kiswahili kinazidi kuchungulia kaburi kila siku
Kuna mijitu hasa hii ya mjini hasa hasa wadada wanapenda sana kutumia haya maneno ,MTU unamtumia meseji anaishia kujibu P,Mara K,Mara PW
Mtu akinijibu kipuuzi hivi ndo mwisho wa mawasiliano nae

Kuna neno lingine limeibuka mitaani 'Jomonii" ndo ushenzi gani huu!? Nyie kina Dada nini maana ya Jomonii??

Unakuta hadi madume nao wanaita "Jomoni" Mara SMS wanajibu "P,PW,K"
Wee mwanaume unaemjibu mwanaume mwenzako vkiufupi ufupi hivi basi jua una dalili zote za ushoga ,haiwezekani mwanaume mzima unajibu kimkato mkato na kivivu huo ni ushoga na utatatuliwa marinda
Mzee kifimbo cheza endelea kuchakaza bakora kwa wote wanaoharibu Kiswahili chetu.

Hii ni lugha kuu ya Sizonje na watu wake acheni kuhiaribu na vimisamiati vyenu uchwara hivyo[emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16]
 
Kuna wengine wana penda kutumia neno "kwendraa" badala ya "kwenda"
 
Kuna jamaa,ni mwanaume kwa jumwangalia alichati na mimi halafu akamalizia kwa kusema usihofu wangu, ikabidi nimuulize unajua una chati na nani, akajibu anajua, nilichofanya ni kumbock tu
 
Mimi hata viemoji situmii kabisa maana naona vimekaa mahususi kwa wenzetu kina dada ni imani yangu tu lkn

Ila huwa nashangaa kidume kinatumia kiemoji cha vidole juu
 
Ila hata hivyo haina haja ya kupaniki, hizi zote ni sifa za lugha na ni dalili ya kiswahili kutumika miongoni mwa vijana ndio maana hata wanapata muda wa kuharibu haribu, hata kiingereza kinaaribiwa na vijana watumiao lugha hiyo kwa maneno kama ain't, gonna, wanna, gotta, watcha, bih na mengineyo mengi hizo ni lugha na misamiati ya vijana, hata siku moja watumiaji wake hawawezi kuyatumia ktk kuombea kazi ama kusomea hotuba ila watumiaji wake hutumia ktk kujumuika na wezao wa rika moja ama jinsia moja

Ukiona huyapendi eidha utakuwa huna uzoefu na tabia za lugha, dikteta wa lugha ama si wa rika la watumiao lugha hizo ama si wa jinsia husika ya watumiao lugha hizo.
 
Hata mimi niliambukizwa hako kaugonjwa! Kwa hisani ya wanajamii forums naahidi kuacha hii tabia........
 
Back
Top Bottom