Nakodisha shamba kwa wajasiriamali wadogo wanotaka kujaribu Vitunguu

Nakodisha shamba kwa wajasiriamali wadogo wanotaka kujaribu Vitunguu

Kipindi cha mavuno gunia ni 70,000 mpaka 120,000.
Na unaweza vuna gunia 60 mpaka 80. Piga hesabu mkuu.

Hiyo bei niya kuuzia shambani ama niyakuuzia sokoni yaani baada ya kusafirisha
 
Mkuu unahaki kuona kuwa haya ni maajabu ya Musa na ndivyo wote tunavyostaajabu tunaposikia jambo kubwa kwa mara ya kwanza. Hata mimi niliwahi kukataa niliposoma humu JF kuwa aina mpya ya michungwa umri wa miaka 3 inazaa machungwa 4000. Sijawahi kuona nilibisha sana! Kikubwa kwa hili la vitunguu usiwe mgumu wa moyo kuamini kwa kuwa kitu hicho ni kawaida. Nikupe mahesabu kidogo uweze kupata picha.

Mkuu kwa vitunguu inawezekana hata kuvuka zaidi ya gunia 80 kwa eka! Ujue hawa wanaotoa data hizi huu ni wastani ambao wakulima wengi huwa wanaufikia lakini ukitumia mbegu bora na ufuate utaalamu kikamilifu inavyotakiwa lazima mtu apande juu zaidi ya hapo. Naomba mkuu utofautishe uzaaji wa mazao ya nafaka na mazao ya mizizi! Mavuno ya mazao yenye uzazi wa aridhini kama vitunguu, viazi vitamu, viazi mviringo, mihogo n.k kwa kawaida huwa yako juu sana.

Eka moja ni mita mraba 4000, eka za kienyeji za hatua 70 kwa 70 hazifikii hapo (ekari za kienyeji hizi ni kama theluthi mbili ya eka halisi). Sasa hizi eka za kienyeji ndiyo hizo wanasema zinatoka gunia 80.

Vitunguu vinavyopandwa kwa umbali wa sm 10 kwa sm 10 kama kweli vitazingatiwa vipimo hivyo vitavunwa vitunguu 100 kwenye kila mita mraba moja yaani mita 1 upana kwa 1 moja urefu.

Mita moja ya mraba unatoa vitunguu 100 punguza asilimia 10 vitakufa au kuwa dhaifu tunabakia na vitunguu 90 kwa kila mita mraba moja!

Siyo eneo lote mita mraba 4000 zitapandwa, punguza asilimia 15 kwa ajili ya mifereji ya umwagiliaji na matuta. Eneo halisi litakalopandwa ni mita mraba 3400.

Idadi ya vitunguu shamba zima = mita mraba 3400 x vitunguu 90 kwa kila mita mraba = Idadi ya vitunguu shamba zima 306,000

Je debe moja vinaingia vitunguu vilivyostawishwa vema vingapi?
Je gunia moja hujazwa vitunguu debe ngapi?

Debe moja linaweza kujazwa kwa vitunguu vilivyostawi vizuri 300 au chini ya hapo, lakini kwa mahesabu tuchukulie vitunguu 300!
Ukigawanya idadi ya vitunguu 374.000 kwa ekari moja kwa vitunguu 300 vinavyojaza debe = madebe ya vitunguu kwa eka moja ni 1,020.
Kama gunia moja ni debe 10 kutoka kwenye madebe 1,020 utatoa gunia 102! Haya ni mavuno kwa ekari ya mita mraba 4000.

Kwa makadirio haya utaona ni kweli kabisa kwamba inawezekana eka 1 ya kienyeji ya 70 kwa 70 kutoa gunia 80. Lakini inawezekana kutoa zaidi kwa kuwa nimeweka makadirio ya kujibana sana.



Good analysis na nimeipenda big up mkuu
 
Nimevutiwa na kilimo cha vitunguu, nina swali direct kwa Mr. Kubota au mtaalamu yeyote.
Nina ekari mbili za shamba maeneo ya Vianzi mpakani mwa Dar na Pwani, kwa kawaida nimekuwa nikilima mpunga na matikiti maji kwa kubadisha nikivuna mpunga na mpunga umekuwa nikivuna mpaka gunia kumi. Ni eneo lenye ukaribu wa maji kwa ajili ya kumwagilia.
Swali- jee naweza kuutumia msimu huu kupanda vitunguu? usimamizi mwenyewe naweza kusimamia lakini jee naweza kupata utaalamu na ushauri ili kufanikisha hili ?
natanguliza shukran
Mkuu Moudyjr ngoja nianze na wengine wataendeleza. Nianze na mpunga japo sicho ulichouliza, mbona mavuno yako ni madogo kiasi hicho? Hasa kama upatikanaji wa maji si kikwazo hata kama ungepata gunia 20 ingekuwa bado hujafanya kitu! Kama kikwazo ni maji hakuna jinsi. Kwa uzoefu wangu kwa ukanda wa pwani ninawasiwasi kwa tarehe hizi kwa kilimo cha vitunguu tunakwenda kwenye kipindi cha joto kali! Kipindi hicho huwa kuna tatizo la wadudu waitwao THRIPS, itakubidi ujidhatiti sana kwa sumu! Ni kipindi kisichofaa kwa mkulima anaeanza mara ya kwanza kwa sababu kunahatari ukipiga mweleka ukakichukia kilimo hiki jumla. Kama utapenda unaweza kupanda eneo dogo tu la kupima upepo ili kama utaona mambo yanakwenda vema msimu ujao ndiyo upige full throttle! Uzoefu wangu kwa maeneo ya Morogoro kilimo cha vitunguu miezi hii huwa ni cha mbinde sana shauri ya wadudu na ukame! Kama unaweza panga mzunguko wako ili uvune mpunga mapema kuruhusu upande vitunguu mwezi June. Kwa maana hiyo unatakiwa uweke kitalu mwezi mwezi April katikati au May mwanzoni. Kitunguu kinapenda majira ya baridi. Ninakuhakikishia utaweza kupata utaalamu na kufanikisha hili ili mradi tu kama JF itakuwa iko hewani!
 
Kama una maji ya kisima cha kuchimba maeneo ya kimanzichana kuna stawi vi2nguu? Au lazima iwe kando ya mto? Kwa huko Ruaha wanyama wakali vp?
 
Thanks so much mkuu Kubota umenipa mwanga, kwa maelekezo yako basi wacha nitumie mda huu kabla ya msimu wa mpunga kwa ajili ya kulima matikiti maji ingawa nayo bado utaalamu ni hafifu.
Kwa mtazamo wangu nadhani nitahitaji ushauri wa karibu juu ya hilo, nitaku-pm ili tuone namna gani tunaweza fanikisha ndoto yangu ya kilimo chenye manufaa.

Thanks.
 
Kama una maji ya kisima cha kuchimba maeneo ya kimanzichana kuna stawi vi2nguu? Au lazima iwe kando ya mto? Kwa huko Ruaha wanyama wakali vp?
Mkoa wa Tabora kuna eneo maarufu sana kwa kilimo cha vitunguu linaitwa Puge, kule hakuna mto bali ni kwa kutumia maji ya visima. Vitunguu husitawi vizuri sana kwenye umwagiliaji huo. Siyo lazima kulima kando ya mto. Angalia urahisi tu wa kuyapata maji maana huko Puge watu wanapiga mzegamzega wa maji shambani umbali wa kiwanja cha mpira cheza na pesa wewe, sijui kama wazaramo mtaweza. Kwi kwi kwiiii! Kuhusu wanyama pori wa Ruaha Mkuu Nyamgluu atatujuza.
 
Kama una maji ya kisima cha kuchimba maeneo ya kimanzichana kuna stawi vi2nguu? Au lazima iwe kando ya mto? Kwa huko Ruaha wanyama wakali vp?

Habari wakuu, nilikua AWOL kidogo nabishana na maisha. Nimetoka shamba leo kuku zangu 30 zimekufa, kondoo 1 nae kafa wengine 9 wamekimbia. Hehehe ALUTA CONTINUA mpaka kieleweke.
King Kong III sasa wewe tena mazee unaogopa wanyama wakali tena, trust me na sura kama hio watakakimbia wenyewe! Hehehe.
Aisee ruaha mbuyuni hakuna wanyama wakali wakutisha. Kuna mamba kwenye mto lakini ndani ya miaka 15 alibebwa mtoto 1 nae mamba alitaftwa akauliwa. Tembo wapo wanakatiza kwa mbali lakini hawasumbui binadamu. Sema nyani ndugu ndio vita ila hawapendelie sana vitunguu, mimi walinisumbua sana kwenye migomba na mahindi, lakini nilivoleta mbwa ikawa safi.
 
Mkoa wa Tabora kuna eneo maarufu sana kwa kilimo cha vitunguu linaitwa Puge, kule hakuna mto bali ni kwa kutumia maji ya visima. Vitunguu husitawi vizuri sana kwenye umwagiliaji huo. Siyo lazima kulima kando ya mto. Angalia urahisi tu wa kuyapata maji maana huko Puge watu wanapiga mzegamzega wa maji shambani umbali wa kiwanja cha mpira cheza na pesa wewe, sijui kama wazaramo mtaweza. Kwi kwi kwiiii! Kuhusu wanyama pori wa Ruaha Mkuu Nyamgluu atatujuza.

Mkuu kubota mm nakaa sumawanga vijijini je hk kilimo kinafaa kunaa maeneo yenyenye maji msimu wote

Je naweza kupata vijan wa kusaidiana kazi yaani kama wattaaalamu wangu
pia labour sina tatizo
 
Mkuu kubota mm nakaa sumawanga vijijini je hk kilimo kinafaa kunaa maeneo yenyenye maji msimu wote

Je naweza kupata vijan wa kusaidiana kazi yaani kama wattaaalamu wangu
pia labour sina tatizo
Mkuu kitunguu sumbawanga kinastawi bila shaka. Ili mradi maji ya umwagiliaji unayo. Unaweza kupata vijana wa kusaidiana kazi maana wengi wanatafuta ajira. Kuhusu vijana wataalamu kama umepania kulima eneo la kutosha nakushauri uende maeneo yanayolima kilimo hiki ukachukue kijana mzoefu ili akakuhudumie shambani kwako hiyo itatoa fursa kwa vijana wako wa huko wapate utaalamu kwa huyu mzoefu ili akiondoka uendelee kivyako.
 
Habari wakuu, wajenga Taifa na wachukuia mafisadi na ufisadi.

Kutokana na mipangilio yangu ya kikazi nimeamua kutokulima vitunguu kwenye shamba langu la Ruaha Mbuyuni mwaka huu. Nina eka 50 kandokando ya mto ruaha, ila ambazo nilishapanda vitunguu na kuvuna mwaka juzi na jana ni ekari 15 hivi. Kwa maana hio ni kwamba hizo eka 15 zinamiundo mbinu tayari ya upandaji vitunguu na hivyo kumpunguzia yeyote gharama za maandalizi ya shamba kama ambavyo ataamua kuanza shamba jipya kabisa.

Gharama za kukodisha eka 1 ya shamba ni shillingi laki 2 na nusu (Ths 250,000/=) hii gharama ni pamoja na kutumia machine yangu ya kumwagilia ambapo kama watumiaji ni zaidi ya mmoja basi umwagiliaji ni wa zamu.

Kwa wale wageni wa hii kazi mtaji unaohitajika kwa eka moja kuanzia ununuzi wa mbegu,mbolea,palizi,mafuta ya kumwagilia na uvunaji ni 1,700,000/= mpaka 2,000,000/=.

Na kama kila kitu kikifanywa kwa usahihi na mother nature na mwenyezi Mungu asiwe kagadhabika na chochote unao uwezo wa kutoa gunia 60 mpaka 80.

Mimi sitalima kipindi hichi kwasababu nataka nielekeze nguvu zangu kwenye shamba jingine na sababu sina uwezo wa kusimamia sehemu kadhaa effectively nikaona bora nikodishe hili lingine aidha lote au kwa vipande vipande.

Natanguliza shukrani wadau.

ANGALIZO: Ukitaka mafanikio kwenye kilimo, usimamizi wako binafsi wewe mtoa hela ni muhimu sana. LABDA uwe na bahati ndogo kama punje ya mchanga bahari kumpata ndugu au mtu mwaminifu na mwenye usimamizi maridadi wa mali zako. Hivyo zingatia hilo.

Mkuu Nyamgluu,

Nikitaka kununua na sio kukodi shamba yanapatikana kwa bei gani?
 
Last edited by a moderator:
Unahitaji roho ya Silver kuwa Mkulima.... unawekeza hizo pesa kisha ukalia hadi machozi yakauke.... na ukabakia kujisemea bora ningenunua Ng'ombe niwe nakunywa maziwa kila siku.....

Kilimo Bongo...!
 
tuko pamoja mkuu

mkuu kubota,inachukua muda gan tangu kuweka mbegu kwenye vitalu kupanda mpaka kuvuna?ma vip vipind vya umwagiliaj vikoje?yaan unamwagilia mara ngapi kwa juma ama mwezi?
 
Back
Top Bottom