Habari wakuu, wajenga
Taifa na wachukuia mafisadi na ufisadi.
Kutokana na mipangilio yangu ya kikazi nimeamua kutokulima vitunguu
kwenye shamba langu la Ruaha Mbuyuni mwaka huu. Nina eka 50 kandokando
ya mto ruaha, ila ambazo nilishapanda vitunguu na kuvuna mwaka juzi na
jana ni ekari 15 hivi. Kwa maana hio ni kwamba hizo eka 15 zinamiundo
mbinu tayari ya upandaji vitunguu na hivyo kumpunguzia yeyote gharama za
maandalizi ya shamba kama ambavyo ataamua kuanza shamba jipya kabisa.
Gharama za kukodisha eka 1 ya shamba ni shillingi laki 2 na nusu (Ths
250,000/=) hii gharama ni pamoja na kutumia machine yangu ya kumwagilia
ambapo kama watumiaji ni zaidi ya mmoja basi umwagiliaji ni wa zamu.
Kwa wale wageni wa hii kazi mtaji unaohitajika kwa eka moja kuanzia
ununuzi wa mbegu,mbolea,palizi,mafuta ya kumwagilia na uvunaji ni
1,700,000/= mpaka 2,000,000/=.
Na kama kila kitu kikifanywa kwa usahihi na mother nature na mwenyezi
Mungu asiwe kagadhabika na chochote unao uwezo wa kutoa gunia 60 mpaka
80.
Mimi sitalima kipindi hichi kwasababu nataka nielekeze nguvu zangu
kwenye shamba jingine na sababu sina uwezo wa kusimamia sehemu kadhaa
effectively nikaona bora nikodishe hili lingine aidha lote au kwa
vipande vipande.
Natanguliza shukrani wadau.
ANGALIZO: Ukitaka mafanikio kwenye kilimo, usimamizi wako binafsi
wewe mtoa hela ni muhimu sana. LABDA uwe na bahati ndogo kama punje ya
mchanga bahari kumpata ndugu au mtu mwaminifu na mwenye usimamizi
maridadi wa mali zako. Hivyo zingatia hilo.