Nakodisha shamba kwa wajasiriamali wadogo wanotaka kujaribu Vitunguu

Makadirio ya faida.. kwa anaejituma?!

mkuu ukisha jua utapata gunia 70 na gharama ni mil 2 basi ni kazi kwako kupiga mahesabu ya faida na inategemea na soko lako, Kwa hapa Arusha Gunia ni kati ya 120,000 - 140,000..60x 120,000 au 80x140,000 kazi ni kwako.....
 
mkuu kubota,inachukua muda gan tangu kuweka mbegu kwenye vitalu kupanda mpaka kuvuna?ma vip vipind vya umwagiliaj vikoje?yaan unamwagilia mara ngapi kwa juma ama mwezi?
Kitaluni hadi kupanda ni siku 45 yaani inapofikia kitunguu shina ni saizi ya penseli. Udongo ukishibishwa maji vema umwagiliaji ni mara moja kwa wiki. Taarifa zangu hizi ninazokuandikia hazitokani na kusikia au kuona kwa jirani bali nimefanya mwenyewe in large scale kwa kutumia pump aina ya JD.
 
kitaluni hadi kupanda ni siku 45 yaani inapofikia kitunguu shina ni saizi ya penseli. Udongo ukishibishwa maji vema umwagiliaji ni mara moja kwa wiki. Taarifa zangu hizi ninazokuandikia hazitokani na kusikia au kuona kwa jirani bali nimefanya mwenyewe in large scale kwa kutumia pump aina ya jd.

asante mkuu,na unashibisha shamba maji kwa muda gan? Yaan nina maana ya kuwa vijaruba/mashamba yanatakiwa yaandaliwe vip na kwa muda gan kabla ya kuhamisha shina?pole kwa usumbuf mkuu
 
Vitunguu hivi vinalimwa/kuvunwa mara ngapi kwa mwaka? au vinachlua muda gani tangu kupanda mpaka kuvuna? na shamba unakodisha kwa mwaka au msimu au mzunguko mmoja?
 
asante mkuu,na unashibisha shamba maji kwa muda gan? Yaan nina maana ya kuwa vijaruba/mashamba yanatakiwa yaandaliwe vip na kwa muda gan kabla ya kuhamisha shina?pole kwa usumbuf mkuu
Mkuu maandalizi ya shamba inategemea na aina ya umwagiliji, siku hizi kuna hadi umwagiliaji wa vitunguu kwa matone huko Arusha. Umwagiliaji wa mifereji na pump inabidi utengeneze vijaruba na mifereji shamba linakuwa mfano wa draft, Vijaruba vyaweza kuwa upana hatua tatu kwa saba na lazima usawazishe ndani ya jaruba level kabisa. Ukikosea kusawazisha maji hurundikana upande mmoja wenye kibonde na upande wa mwinuko uliokosa maji haulowi vya kutosha. Kwa hiyo ninaposema kulowanisha vya kutosha ni kile kitendo cha maji kuingia kweye jaruba na kusambaa kwa kina chenye usawa. Kusawazisha jaruba ndiyo jambo la muhimu zaidi. Kwa umwagiliaji wa matone hutengenezwa matuta ya kunyanyua kama matuta ya kawaida ya bustani ambayo ni mapana na flat hapo juu. Bila shaka nimekujibu. Karibu tena.
 
Umenijibu mkuu kubota na hili ni zaid ya somo kaka,nikusumbue tena kidogo mkubwa wangu.naomba kufahamu ni muda gan hutumika tangu kulatika/kuweka mbegu kwenye kitalu mpaka kuvuna.

Natanguliza shukran zang za dhat mkuu.
 
Kitaluni hadi kupanda ni siku 45 yaani inapofikia kitunguu shina ni saizi ya penseli. Udongo ukishibishwa maji vema umwagiliaji ni mara moja kwa wiki. Taarifa zangu hizi ninazokuandikia hazitokani na kusikia au kuona kwa jirani bali nimefanya mwenyewe in large scale kwa kutumia pump aina ya JD.

Mkuu hivi pump za JD ni nzuri? vp uwezo wake wa kivuta maji ni hadi mita ngapi? Zinauzwaje?
 
Umenijibu mkuu kubota na hili ni zaid ya somo kaka,nikusumbue tena kidogo mkubwa wangu.naomba kufahamu ni muda gan hutumika tangu kulatika/kuweka mbegu kwenye kitalu mpaka kuvuna.

Natanguliza shukran zang za dhat mkuu.
Mkuu Kititima, kitaluni ni siku 45, baada ya kupandikiza shambani ni miezi 3 kwa hiyo kutoka kusia mbegu hadi kuvuna ni miezi 4 na nusu. Tuko pamoja.
 
Mkuu hivi pump za JD ni nzuri? vp uwezo wake wa kivuta maji ni hadi mita ngapi? Zinauzwaje?
Mkuu sana Sabayi, pump za JD ni nzuri sana na sijaona dosari kabisa! Nimekuwa nayo miaka 5 inapiga mzigo vema. Nilikuwa naiweka ndani ya mto ambao kina chake hadi juu usawa wa ardhi mita 10. Na kuweza kusukuma maji ndani ya mpira wa nchi 3 umbali zaidi ya mita 150 ambako nako maji yaliendelea na mtelemko! Ni pump yenye ukubwa wa nchi 3 sikumbuki horse power yake vizuri niko mbali, ni kama 5.5 hadi 6. Nikitaka kuongezea ya pili sitahitaji zaidi ya JD labda kama zimeshachakachuliwa maana hii dunia hii aaah!!!
 
Elimu nzuri sana mkuu Kubota nitakucheck kwanza tuongee vizuri zaidi...

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu sana Sabayi, pump za JD ni nzuri sana na sijaona dosari kabisa! Nimekuwa nayo miaka 5 inapiga mzigo vema. Nilikuwa naiweka ndani ya mto ambao kina chake hadi juu usawa wa ardhi mita 10. Na kuweza kusukuma maji ndani ya mpira wa nchi 3 umbali zaidi ya mita 150 ambako nako maji yaliendelea na mtelemko! Ni pump yenye ukubwa wa nchi 3 sikumbuki horse power yake vizuri niko mbali, ni kama 5.5 hadi 6. Nikitaka kuongezea ya pili sitahitaji zaidi ya JD labda kama zimeshachakachuliwa maana hii dunia hii aaah!!!

Nashukuru kwa maelezo mkuu sasahivi natumia honda ya Mjapani bado sio mbaya ila nategemea kuongeza ukubwa wa eneo la kumwagilia soon so I will need a bigger and more reliable pump I think ntaenda kwa JD japokuwa bei yake si ya kitoto 6M ni parefu sana
 
Mkuu Sabayi pump ya mil sita ni heavy duty. Pump ya JD kama nilivyoonesha ni pump ya kawaida kwa kuhudumia eneo la hadi ekari tano hadi sita. Ni yenye horse power kama sita na upana wa mpira ni nchi tatu. Bei ya pump hizi nadhani iko chini kabisa ya milioni moja. Nashani hiyo ya mil sita itakuwa ni mtambo mnene zaidi. Mtambo kama huo unafaa kwa maeneo makubwa zaidi ya ekari hamsini, maana shamba halimwagiliwi kila siku.
 
Okay labda sikukuelewa vizuri mkuu hapo uliposema 5.5 hadi 6 nikajua ndo bei hiyo kama ni chini ya 1M nielekeze mahali zinapouzwa kaka nataka kuongeza pump nyingine next month
 
Nilinunua kwa jamaa wa TUNAKOPESHA ltd mwaka 2007 wakati huo ikiuzwa 400,000/= wakati huo pump zilikuwa chache si kama sasa ambapo supply ni kubwa. Sina uhakika kama bado wanaendelea na biashara hiyo. Ninaamini bei haitakuwa mbali sana. Sifahamu wauzaji wengine kwa sasa ila zamani hizo niliwahi kuona zikiuzwa maduka ya Boma road karibu na msikiti mkuu Morogoro mjini. Kama vipi nunua model uliyoizoea na kuifahamu ya Made in Japan maana wajapan wamejichimbia zaidi kwenye high quality products. Hawabahatishi ndiyo maana bei zao huwa ziko juu.
 
Okay nimekusoma mkuu
 
Thank you for this useful thread, infact nitawajoin wakulima very soon.

Nasubiri nihamie kwangu ili hata mambo yakibuma sidaiwi pango. Mkuu ninakuhakikishia kwamba nitakutafuta very soon unipe mkakati zaidi ikiwa ni pamoja na kuliona eneo kama liko strategic.

Thanks and regards
Raimundo
 
Back
Top Bottom