Nakohoa damu, nimeenda hospitali wanasema kuwa sina shida yoyote

Nenda hosipitali ya serikali, achana na hizo za mitaani.
 
Elezea na dalili zingine kama unazo ukiacha hii ya kukohoa damu.

Ikiwezekana elezea pattern ya kukohoa ikoje? Muda gani unakohoa sana na muda gani kinapoa? Nini ukifanya kinazidi?

Rangi ya damu ni nyekundu (fresh wound) au damu ya mzee (damu iliyoganda)

NB. Mimi siyo daktari nipo mortuary hua nasikia wakiongea
 
1. Kuna dawa zozote ulkua unameza kabla ujaanza kukohoa?

2. Uliwahi kuugua Gout?
(Ugonjwa wa miguu na joint kuwaka Moto)

3. Unawahi au ulishawahi kuvuta sigara?

3. Umepima kifua kikuu?
 
Amina!
Wafilipi 2:10 neno la Mungu Yehova linasema "kwa bwana Yesu kila goti litapigwa,"
nafurahi kwa kukiri kwako naona unaanza kukunja goti taratibu kitukuu ya babu mdogo Ishmail...Hakika Yesu atamponya na tutaendelea kuwa nae hapa jukwaani
Ila lazima aende Hospital ndio Yesu amponye kama ulivyo mshauri,si ndio?

Vipi kuhusu wale ambao hua wanapona kwa maombi au kwa mafuta na chumvi? au hiyo njia haifai? au hua ni geresha tu ya hao wachungaji?

πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Pole. Usi-panic sana. 1. Una uhakika kuwa unakohoa damu? Nasema hivi kwa sababu unaweza kuwa tatizo lako liko kinywani eg kwenye meno au kuna mchubuko wewe ukadhani damu inatoka ndani. 2. Koo halina tatizo? Inawezekana kuwa kooni kuna mchubuko mdogo sana ndiyo unasababisha. Mwisho niulize, walifanya uchunguzi gani na kusema huna tatizo.? Jambo la muhimu ni kusubiri na ukiona tatizo haliishi, urudi tena hospital.
 
Kuna virus wabaya sana huwa wanashambuli koo na kuweka kidonda. Unajisikia kuwa na dalili za flu?
 
Kapime TB kwenye hospitali inayoeleweka achana na vizahanati uchwara.
 
Ila lazima aende Hospital ndio Yesu amponye kama ulivyo mshauri,si ndio?

Vipi kuhusu wale ambao hua wanapona kwa maombi au kwa mafuta na chumvi? au hiyo njia haifai? au hua ni geresha tu ya hao wachungaji?

πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Vyema.Ni vizur kama umeamini Yesu anaponya...hayo ya chumvi na mafuta kama huamini hayana ulazima.....binafsi siwezi kuwa wakili wa chumvi na mafuta
 
Umepima madonda ya tumbo?
Na pia upime Tb kwa vipimo sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…