Ghiti Milimo
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 5,160
- 7,702
Wakuu, hebu tufikirie, ukamatwaji wa Tundu Lissu, na ukamatwaji wa Alli Kamwe kule Tabora.
Kamwe, ilishaamuliwa akamatwe kabla hata ya ule mchezo wao na Tabora. Alikuwa anazunguka mjini akiendesha baiskeli, huku amezungukwa na Mashabiki wa Yanga.
Ma- Polisi walimuona, lakini hawakuthubutu hata kumgusa! Uwanjani siku ya mchezo, alikuwepo, polisi walimuona, hawakuthubutu kumkamata! Mpira, ulipokwisha, alirudi hotelini alikofikia, lakini pia, mashabiki wa Yanga, walikuwepo hapo, polisi walimuona, wakamuacha tu!
Giza lilipokuwa limezidi, mashabiki mmoja mmoja, wakaondoka na kwenda makwao. Usiku wa manane, Kamwe hakuwa tena na hao mashabiki wa Yanga. Ndipo hao Ma - Polisi, wakavamia hapo hotelini na kumkamata, na kuondoka naye! Hivyo, inaonyesha, hawakuthubutu kumkamata "Msemaji",mbele ya mashabiki. Wasingeweza. Mashabiki, wangempigania!
Angalia upande mwingine, kwenye mkutano wa Lissu. Kulikuwa na watu wengi sana. Waliinuwa mikono juu ikiwa imekunja ngumi, na kutamka 'peoples power'! Wakahamasika na ile 'NO REFORMS NO ELECTION'! Wakatamba, bila hilo, watakinukisha! Hakuna kufanyika uchaguzi!
Mara Ma-polisi wakavamia mkutano, bila kujali ni katika mazingira gani, Mheshimiwa Lissu, akakamatwa kama kuku. Waliokuwa wanaimba 'Peoples power', hawakujitolea kumpigania, asichukuliwe, kwenye uwanja huo ulipofanyika mkutano!
Hapo ndipo tujiulize. Kwa nini hao polisi, hawakumkamata Kamwe mbele ya mashabiki wa Yanga? Na kwa nini polisi hawakuogopa kumkamata Lissu, mbele ya mashabiki wake, tena kwenye mkutano wa hadhara?
Hizi timu, ni zaidi ya Timu!