Nakubaliana na Lema, Watanzania tunazithamini Simba na Yanga, kuliko mambo ya maana!

Nakubaliana na Lema, Watanzania tunazithamini Simba na Yanga, kuliko mambo ya maana!

Wabongo wamechoshwa na siasa za wanasiasa wasio na misimamo.
2015 walituuza kwa mafisadi kwa kigezo cha gia ya angani.

Waliungana na mafisadi ya CCM kumpinga Magufuli hasa pale alipokuwa akileta maendeleo na kuwachukulia hatua mafisadi.
Walipinga bwawa la umeme.
Walipinga SGR.
waliwatetea wazungu kwenye makinikia.
Wakafanya sherehe kifo cha Magufuli.

2022 wakaingia maridhiano yasiyoeleweka na SAMIA ( CCM)

Wapinzani watanzania wameonesha hawana hata dalili ya kumkomboa mwananchi isipokuwa hitaji lao kuu ni wao kuingia madarakani ili nao wakale km CCM.

Wananchi wamebaki yatima hawana mtetezi kwa lolote tunaomba tu kudra za Mungu .
CCM na wapinzani ni kopo na mfuniko.
Tunatamani chadema ilee ya katibu Dr Slaa, walau ilithubutu kuongelea na kupambania maslahi ya Nchi na wananchi kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom