Nakubaliana na Manara: Karia na TFF yake wameonyesha chuki yao Kwa Yanga hadharani

Nakubaliana na Manara: Karia na TFF yake wameonyesha chuki yao Kwa Yanga hadharani

Kwahiyo umeamua kuungana na roporopo Manara kumkataa Karia na kupingana na Rais wako wa klabu Hersi Said aliyependekeza Karia apite bila kupingwa kwenye uchaguzi ujao?
 
Nimekuwa nikimpiga mawe Manara hapa jukwaani kutokana na kauli na matendo yake yasiyo na staha, ila Kwa alichokisema Yuko sahihii

Karia ana chuki na Yanga na anatumia taasisi zake kuhujumu Yanga hadharani
Karia amekaa ushabiki na mapenzi Kwa Simba na kumfanya aache weledi ana aropoke ovyo kwenye media

1. Hakuna kiongozi wa Yanga amewahi kuongea na vyombo vya habari na kuchafua TFF na bodi ya ligi
Yanga wametumika mbinu sahihi ikiwa ni kuandika barua ya malalamiko na madai Yao Kwa bodi ya ligi,
Tulitegemea bodi ya ligi na TFF kuwajibu Kwa njia rasmi

2 Karia anasemaje viongozi wa Yanga hawapaswi kuwa kwenye madaraka Yao.
Hii ni dharau kwetu Wanachama tuliowachagua Kwa kura kihalali kwamba yeye anaona tulikosea.
Eng Hersi Said na Kamati tendaji ya Yanga ipo madarakani kikatiba wala sio Kwa kupendelewa

3 Karia anasemaje viongozi wa Yanga wanafanya utoto
Sijui kama Karia yupo sawa kichwani.
Yaani viongozi wa Yanga wameandaa timu Kwa gharama, wamelipa wachezaji, wamekodi uwanja, wamealika wageni na mashabiki.
Bodi ya ligi na Simba wakasingizia mazoezi na kukimbia mechi
Yanga wakaandika barua, Leo Karia anasemaje viongozi wa Yanga wana utoto
Hii ni kashfa kubwa na dharau Kwa Yanga, kuitwa watoto
Yanga imekuwa bingwa mara 30, Yanga amecheza final CAFCC, Yanga ni timu tishio Africa
Karia acha dharau

4. Karia amedhara tasnia ya Sinema.
Karia kusema kuwa Yanga wakacheze Sinema, hii ni dharau Kwa tasnia
Sinema ni tasnia kubwa, umeajiri Watanzania wengi kuanzia wasanii, directors, managers n.k
Kwanini Karia alinganishe tasnia ya film kama jambo la ovyo

5 Karia amejipa upofu juu ya makosa ya bodi ya ligi
Uzembe uliofanywa na bodi ya ligi ana uhalalisha, hatokei kukemea

Karia wewe ndo Rais wa mpira, weka hisia na mapenzi pembeni tenda haki

Karia Kwa wadhifa wako inatakiwa uchunge kauli yako, kama umeelewa madaraka utajua

Yanga tunahitaji kuifuta TFF nzima na taasisi zake Kwa hujuma dhidi ya timu yetu

Yanga bingwa
Kwani mkiambiwa mkacheze sinema ndiyo tasnia ya sinema imeharibiwa? Alimaanisha ndiko mnako fit zaidi kwa hizo akili zenu. .
 
Simba haina uweZo wa kuifunga Yanga.
Ndo maana Simba walikimbia
Hiyo mechi wanaweza wacheze vijana wa under 17 na kuwafunga 5imba 5 kama kawaida
Kwa akili za Utopolo na anaezitumia ni Utopolo, kwake inawezekana
 
Karia na ni mwanachama hai wa Simba na anatumia TFF kuinufaisha Simba
Yeye asimamie kanuni asitumie madaraka yake kuibeba Simba na kuhujumu Yanga
TFF anashirikiana na Simba kukwepa mchezo Kwa kuingia kichaka cha kuzuiwa kufanya mazoezi

Watu wanaongea facts wewe unaleta pumba.
Huna akili
 
Kwanini useme Sina akili kisa Sina mtazamo sawa na wako
Heshimu mawazo ya watu
Mbona sijakuita mjinga
Akili huna hilo tumeshalipitisha humu JF.

Yaan ukitoka wewe anafuata popoma
 
Akili Ndogo kuongoza akili kubwa ni changamoto sana. Ukimtazama na kusikiliza jinsi Hersi anavyozungumza kwa hekima utulivu na busara, alafu ukimtazama huyo anayeitwa boss wa mpira Tanzania, utagundua ni mbingu na ardhi.
 
Iandike hapa
Kanuni ya 34;
Mchezo unaweza kuahirishwa kutokana na sababu yoyote kati ya zifuatazo;
1.1. Endapo timu ya taifa inacheza.
1.2. Endapo timu shiriki inashiriki ktk mashindano ya kimataifa.
1.3. Sababu ya dharura au yenye msingi itakayokubaliwa na TFF.
1.4. Matukio yaliyo nje ya uwezo wa kibinadamu.
1.5..............

Kanuni ya 31;
Timu yoyote itakayokosa kufika uwanjani bila ya sababu za msingi zinazokubalika kwa TFF/TPLB na / au kusababisha mchezo usifanyike itakabiliwa na adhabu zifuatazo;
1.1. Kutozwa faini.
1.2. Kulipa fidia ya maandalizi.
1.3. kupokwa alama 15.

Simba alitumia 31 kwa kuitafsiri kwamba kumbe timu haijanyimwa haki ya kutofika uwanjani bali inawezekana kama tu ipo sababu ya msingi inayokubaliwa na TFF/TPLB na msingi wenyewe kati sababu hiyo iwe ni ukiukwaji wa kanuni kama kanuni ya 17(45) iliyokiukwa kwa simba.

Sasa wewe na wenzako tajeni kanuni inayomzuia tff/bodi kuahirisha mchezo au kanuni iliyokiukwa na simba.
 
Back
Top Bottom