Nakubaliana na mchungaji Msigwa kuwa level of thinking Tanzania imeshuka

Na moderator wamekuwa a akili chafu sana za kuwa biased hii miaka ya karibuni.

Kitendo cha kuzuia mijadala fulani isifanyike tayari unaitoa hadhi hii platform ambayo mojawapo ya misingi yake ya asili ni kuzungumza wazi wazi bila kificho ili kutafuta muafaka.

Hapa hatutumii hasira wala nguvu katika kujenga hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angeweza ku-think critically CHADEMA isingeserereka kwa huo mserereko! Kuna tofauti Kati ya muuza maneno ya ujanja ujanja na mtendaji mwenye maono na nia thabiti!
Mfano mwingine wa mamburula, nadhani hii pia inachamgiwa na udumavu wa akili unaosababishwa na lishe duni au utapia mlo...

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
" You are going to come across people in your life who will say the right words at all the right times. But in the ends, it's always their actions you should judge with them by. It's actions not words that matter"
Yesu alitufundisha kuwa tuwasilikilize mafarisayo pamoja na walimu wengine lakini matendo yao tusiyafuate.... kwanini? Walichokuwa wanafundisha sicho walichokuwa wanakifanya. Hivyo basi, ukiona mtu anakushauri jambo zuri, hata kama ni chizi, msikilize na kamwe usitamani kujua yeye anafanya nini... baadhi waliumbwa kwa ajili ya kuwafundisha wengine ili wafike hatua fulani. Ndo mipango ya Mungu hiyo.

KUHUSU MADA HAPO JUU: Awali nikushukuru mwandishi, Mch. Msigwa kasema mambo mengi mazuri, ambayo sisi kama vijana tunapaswa kuyatafakari umakini. Binafsi sijayasikia wala kuangalia hayo mahojiano ila kunaweza kukawa na nadharia mbili katika kuchambua hoja zake kutokana na taarifa aliyoiandika mleta mada hapo juu.

Mosi: Mrengo anauwakilisha Mch. Msigwa binafsi, "critical thinking" katika siasa. Watu wengi tumekuwa na mihemko ya kisiasa hasa sisi vijana kwa kushawishiwa mambo ambayo pengine hatuelewi yana maslahi gani kwa taifa letu. Tunasikiliza maneno ya wanasiasa pasipo kupima nia na madhumuni yaliyo nyuma ya maneno yale kama ni kwa maslahi binafsi au ya taifa letu la Tanzania 🇹🇿.

Pili: Mrengo anauwakilisha Mch. Msigwa binafsi, "critical thinking" katika mambo ya uchumi na kijamii.

A. Licha ya kuwa siasa imekuwa ikiamua mambo mengi katika jamii, matokeo yake hujionesha wazi wazi katika nyanya nyingine ikiwamo uchumi wa nchi. Ni lazima sisi kama vijana, tuweze kuwa na uwezo mkubwa wa ubunifu ndani na nje ya Taifa letu ili kusudi kuchochea maendeleo yetu kiujumla.

B. Kufikiri kuliko sawasawa kunaweza kuleta mageuzi makubwa sana katika kufanya mapindizi ya viwanda kama walivyofanya vijana wa mataifa mengi duniani ambayo kwasasa yanakula matunda ya vijana wao. Hapa lazima tuibue teknolojia hizo hizo ambazo zipo kwa wenzetu lakini kwa kuzioanisha na mazingira yetu ili kutatua changamoto ambazo jamii yetu inakumbana nazo kwa sasa na kizazi kijacho. Na wakati huo huo watu binafsi, mashirika binafsi na ya kiserikali yawe yanatoa mchango wao katika kuwainua wabunifu hawa.

C. Pia, vijana tunapaswa kujua na kukataa kabisa wewe uishi maisha ya kuteseka na kizazi chako kiishi vivyo hivyo. Teseka wewe kwa nguvu zote hata kama ni kwa jasho na damu ili kizazi chako chote kiweze kuishi kwa furaha. Kwa mfano hali ya maisha ya sasa kweli ni ngumu sana, lakini ni lini hali ya maisha iliwahi kuwa rahisi kiasi hicho....??? Kwa mfano mimi kwa zaidi ya miongo miwili sasa nimekuwa nikisikia kila siku maisha ni magumu maisha ni magumu... hata sasa nawaambia wadogo zangu vivyo hivyo... hakuna wakati ambao maisha yaliwahi kuwa rahisi hata enzi za Yesu... tena Yeye alizaliwa kwenye zizi la ng'ome (tujifunze kupitia Yeye). Leo hii watoto wetu wanazaliwa katika zahanati na hospitali zilizo nchi nzima isipokuwa baadhi ya maeneo. "There is no gain without pain".

Ahsante
 
Umenena vyema sana kiongozi.

Naitazamia JF niliyokuwa naisoma sana kipindi cha < 2018 na JF ya 2019> Ni sehemu mbili tofauti sana na hii inaonesha kwamba kipindi cha 2019 > vijana wengi wameegemea sana kwenye siasa za uvyama sana kuliko mambo ya msingi ya kujadili.
Vijana wengi wanakwenda na upepo wa huyu kasema nini mara yule kasema nini mwisho wa siku wanaanza kulalamika kuwa hakuna ajira.
 
bado mnamwita mchungaji huyo mchumia tumbo???
 
Hakuna nchi isiyo katiba Labda Kama ujui nini maana ya katiba.
Hakuna nchi isiyo katiba Labda Kama ujui nini maana ya katiba.
Wewe ndie hujui uingereza haina katiba inaendeshwa kwa sheria tu waliona katiba ni ujinga mtupu sharia kwao ndio supreme mfano uhuru wa kujieleza kwao hawahitaji kaandika kwenye katiba ni kitu koko obvious jieleze utakavyp ila ukitukana mtu utakumbana na sheria mahakamani ya kutukana mtu
Ukibagia mtu kwa jina is au dini kwenye ajira utakumbana.na sheria ya ajira uliyemwonea atakuburuza mahakamani

Katiba ni useless tool

Utawala wa sheria ndio kila kitu
 
Very true
 

Unazungumzia kitu kimoja sheria ndio katiba, sheria ipo ndani ya katiba
 
Lzm ipungue sababu ya ujamaa.
Wafanye wawe masikini ili uwatawale watu wakishauwa masikini thinking yao ni lzm ipungue sababu awatowaza chochote zaidi ya jinsi ya kumudu shibe.
 
Njia pekee tegemeo ya watu kushiba ni kuimba kwaya na muimbaji mzuri ndo utupiwa mifupa angalau
 
Unazungumzia kitu kimoja sheria ndio katiba, sheria ipo ndani ya katiba
Ni repeation kwa nini urudie kuandika kitu kike kile mara mbili uandike katiba halafu uandike sheria?wastage of time and money

Uingereza wako sahihi kukataa kuwa na katiba na kutaka tu utawala wa sheria yaani rule of law kutegemea sheria peke yake sio tabu la kibwege linaloitwa katiba
 
Hakuna serikali iliyifanikiwa kuwafanya wanadamu kuwa marobot kama hii ya bwana Jiwe,hebu fikiria eti wanatoza kodi YouTube channels za Tanzania ila za Kenya,Us nk hawazigusi
 
Hakuna serikali iliyifanikiwa kuwafanya wanadamu kuwa marobot kama hii ya bwana Jiwe,hebu fikiria eti wanatoza kodi YouTube channels za Tanzania ila za Kenya,Us nk hawazigusi
Kenya wanachaji pia zao lazima uwe na leseni
 
Sisi tuna vyote na hatuvifuati hapa ttzo Ni nn.Au sababu wao ni civilized
 
Kenya wanachaji pia zao lazima uwe na leseni
Sasa kwa nini tunachaji za kwetu tu lakini za nchi nyingine au za anonymous hatuzichaji wala hatuna ufumbuzi wa namna gani zichajiwe
 
Sisi tuna vyote na hatuvifuati hapa ttzo Ni nn.Au sababu wao ni civilized
Tatizo sisi rule of law hatujali wenzetu wanaheshimi sana sheria miliki chochote
Sisi huku katiba haizingatiwi wala sheria

Mfano katiba inasema kila binadamu wanastahili heshima na kuthaminiwa you wake unakuta wanasiasa anaporomoshea matusi mwanasiasa mwenzie walisema ohh katiba ina kipengele cha uhuru wa kujieleza!! Anasahau kuwa koko kipengele kinachokataza kumvunjia mtu heshima na uti wake

Na aliyetukwana haendi mahakamani kushtaki kutumia sheria ya kudhalilishwa kinyume na sheria!!!

Kutojali utawala wa sheria ni kama ndio sababu kubwa ndio maana uingereza ndio nchi inaongoza duniani kwa kujali utawala wa sheria
 
Sasa kwa nini tunachaji za kwetu tu lakini za nchi nyingine au za anonymous hatuzichaji wala hatuna ufumbuzi wa namna gani zichajiwe
YouTube walianzisha YouTube za nchi kujiongezea mapato mfano wewe ukiingia youtube unaingia YouTube ya Tanzania ambayo Tanzania ndie mumililiki na mlipa fees YouTube Tanzania kupeleka YouTube head office ndie owner
Za nje owner ni nchi nyingine e.g. YouTube Kenya huwezi taka TCRA iingilie youtube Kenya au zimbabw nk
 
Chadema wangekuwa wanathink critically wasingekuwa hivi walivyo kumbukeni maono na mtazamo wa Dr W Slaa. Rest in Peace Chadema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…