Nakubaliana na ndugu Bashe kuruhusu wakulima kuuza mazao popote wanapotaka

Nakubaliana na ndugu Bashe kuruhusu wakulima kuuza mazao popote wanapotaka

Kwanza mkulima anauza mazao yake akisha vuna tu kwa mfanyabiashara. Labda Serikali iwe inanunua na kuhifadhi(NFRA) kwa bei ya soko.
Yes na hayo ndo maisha yao. So faida wanayopata sio kubwa kama anavyoelezea bashe
 
Nimeona humu watu wengi sana wakiishambulia serikali Kwa kutozuia mazao kuuzwa nje ili kupunguza mfumuko wa bei. Ukweli ni kwamba serikali inaweza kuzuia mazao kuuzwa nje.

Jambo hilo ni hatari sana Kwa mustakabali wa kilimo na wakulima wa Tanzania. Gharama za uzalishaji zimepanda sana, kila nyanja ya maisha vitu vimepanda je hayo mazao ya kilimo yakiuzwa bei chini nani atafidia gharama za ziada?

Mwaka ambao nililaani kilimo ni ule mwaka Serikali ilizuia mazao kuuzwa nje eti kwa sababu ya kulinda bei tuliuza gunia shs 30 elfu hata hivyo hapakuwa nawanunuzi. Kuna kipindi serikali ikatutangazia kuwa itanunua mahindi yetu sijui tani ngapi lkn haikusaidia chochote wakulima tukiendelea kusota na mazao.

Likiwa hilo halijapoa serikali ikakosana na wanunuaji wa mbaazi badala yake nikamsika manyanya anasema mbaazi ni tamu sana wakulima kuleni.

Ndugu zangu soko la uhakika na lenye bei nzuri la mazao yote ya kilimo ni muhimu sana kwa uhai na ukuaji wa kilimo kuliko kushinikiza mazao yashuke bei.

Nakumbuka mama alipo apishwa alizinguka sana kwa majirani kuomba waruhusu mazao ya Tanzania yauzwe kwao. Kuna wakati Kenya walisema mahindi yetu yana sumu ilileta maafa Kwa wakulima
Msaada kwa wakulima wa Nchi hii ni kuimarisha vyama vya Ushirika, ambavyo watawala wafanya biashara hawataki. Mengine yatabaki kuwa porojo tu.
 
Back
Top Bottom