Wakati mwingine unaweza kufikiri kwamba Historia ya Tanzania ilianza na Magufuli na kuishia na kifo kwamba hakuna Historia ya Tanzania bila Magufuli kama ukiwasikiliza baadhi ya watu wanaongozwa na emotions badala ya logic, maraisi wote wote wa Tanzania waliopita walizuia uuzwaji wa mazao nje ilipobidi lkn imegeuka ni Magufuli ndiye aliyeanzisha na kuuwa kilimo kana kwamba kabla ya Magufuli kulikuwa na kilimo chochote cha maana ambacho kimeuliwa.
Wakati mwingine intelligence ya watu humu iko chini ya kiwango, kuzuia kuuza mazao nje ni mfumo wa CCM na siyo kwamba ulianzishwa na Magufuli, besides unatumika Dunia nzima hata capitalists kama USA, Europe au hata China hufanya pale inapobidi, huwezi kuexport chakula nje wakati wananchi wanakufa njaa!