Na kwa akili zenu mnadhani wakulima wanafaidika?
Wanaofaidika ni madalali. Mteja (tajiri) anatoka Dar au nje ya nchi anaenda kijijini kutafuta mazao, madalali wanamdaka wanamwambia we tulia usihangaike sisi tutakutaftia kwa bei nzuri, wao ndo wanawajua wakulima, wanaenda wanawalangua kwa bei wanayo taka wao madalali, wakipeleka bidhaa kwa mteja wanapandisha cha kwao.
Sasa hiyo nimeongelea wale wakulima wa chini kabisa. Hamna faida ya tofauti wanayopata ila middle men ndo wanafaidika. Mkulima ukigoma kutoa mazao kwa bei wanayotaka wanaenda kusambaza mtaani kwamba bidhaa yako haina ubora. So ili visidode mkulima anaamua tu akubali.
Na kumbuka sio wakulima wote wenye uwezo wa kusafirisha mazao yao wenyewe kwenda nje. Wanawategemea madalali. Things are absurd kwa ground