Nakubaliana na Rais Mwinyi kwamba Manaibu Waziri wanaongeza gharama za Serikali naamini Rais Magufuli atafanya hivyo pia!

Kama ni hivyo basi ni kwa nini bado ameamua kuwa na makamo rais wawili? Kuna haja gani ya kuwa na Rais wa nchi ndogo kama zanzibar kuwa na makamo wawili? na hawa nao wanafanya kazi gani hasa ambazo rais mwenyewe na makamo mmoja hawawezi kuzitekeleza?
 
Ma Naibu waziri wakitumika vizuri wanakuwa na manufaa,kama tulivyomuona Bashe.
Lakini imezoeleka tabia ya watawala wetu kuwatunukia uwaziri mdogo kama zawadi.
Matokeo yake wanajikuta wanaishia kuwa na ofisi bila majukumu yenye tija.
Nchi tajiri kama Ulaya zina mawaziri kidogo sana ukilinganisha na Afrika. Nguvu nyingi huko Ulaya imewekwa kwenye idara za wizara.
 
Sio kweli...

Ni Bora makatibu wakuu wawe wawili na naibu waziri asiwepo.
 
Mkuu wizara haimtegemei waziri tu kujiendesha na watendaji wengi Tena walio somea kabisa juu ya mambo ya wizara hiyo na ndo Maana hata kipindi hiki ambapo nchi haina mawaziri bado inaenda na Mambo yanaenda vizuri tu.
Kazi ya waziri ni kama msimamizi wa wizara tu Ila siyo mtendaji.
Hivyo Basi kila wizara ikiwa na Waziri mmoja, katibu na watendaji Kazi waliobaki hakuna kitakacho haribika. Otherwise Kama wizara ina Mambo mengi Sana ndo unaweza ungeza na naibu Waziri.

Tujifunze kubana matumizi kwa faida ya wote.
 
Hakika mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…