mambo madogo sana hayo, mi nimewahi kusikia kwamba kuna Baba mmoja wakuitwa jehova alitelekeza mwanae, wahuni wakasema nae msalabani. piga misumari, aaah nakufa kutakatha dhambi dhenu.Pumbavu ni huyo Baba anayezalisha kama panya halafu anatelekeza watoto.
Huyo Baba hafai kabisa.
Bro sorry kwa hiyo mwanaume aliyeondoka akaacha kichanga Cha wiki mbili ni wa kuongea huruma? Alifikiri kichanga na watoto wake watakula nini? Hata uchukie vipI, hizo damu zako usiziachw na mateso. Mmekorofishana watu wawili, je hao watoto unaosema wanalishwa simu na mama yao angewatelekeza kama baba? Si wangekufa ukute mifupa? Acheni kuendekeza msemo wanawake wana kera wakati uliambiwa ishi nao kwa akili. Tafuta Chaka la kumuacha mwanamke ila kamwe usiache watoto wateseke uje kusema oh shida ni mama yenu, kwani alikulazimisha kuzaa?Pole kwa yote uliyopitia!
Inaumiza mzazi kukutelekeza ama kutokupatia kitu fulani hasa kipindi Cha utotoni na wakati wa kukua hapa na inapelekea watoto wengi kuwa na maumivu, chuki, hasira na wengine hata ubinafsi!
Lakini jitahidi upate kupona, majeraha hayo ya kutokupata malezi na matunzo ya baba mzazi!
Kumbuka binadamu yeyote anakosea hivyo mzazi naye anakosea Tena pakubwa tuu, msamehe mzee.....
Najua mama yako alikulisha maneno na kumsema mshua, sana na ninyi watoto kuyachukua maneno mazima mazima na kujenga uadui kati yenu na baba yenu...... Acha kushikilia maneno ya mama yako au sumu aliyoiweka juu ya mumewe!
wewe fanya hivi hakikisha unapona unakuwa na amani ukimuona mzee wako usisikie kuumia!
Ikiwa yupo hai kamsalimie, mpe zawadi, mpe hela ondoa kinyongo wacha yeye apokee hukumu ya alichokifanya kwenu lakini wewe usiwe hakimu wa kumhukumu!
Muheshimu mpende mzee wako! Hakuna baba mwingine mzee,
Pia huwez jua tatizo lililomfanya akimbie ni nini ukiwa wewe ni wa kiume unayaelewa maisha basi nenda taratibu Jenga mahusiano mazuri na baba yako mzazi! Ikawe khery
Ndo maana nasema ni sheria ya Kristo ila sio lazima. Watu wanafanya ni lazima maana ni baba. Alikimbia majukumu. Hapo ni kwa vile una Roho Mtakafifu wa kukusaidia. Sio rahisi. Ni kumwombea neema maana mzazi hastahili lakini ba sisi pia hatustahili pia. Ni neema tu ya Yesu ila sio haki.Mm ni mhanga tena bora ww , story yangu ni ndefu mno lakin nakupa tu kifupi baba alikua askari lakin sisi watoto wote hajatusomesha yaaan yeye ndo alikua kikwazo cha sisi kusoma, mimi kwa uwezo wake mungu nikasoma kati yetu watoto watatu , baba aliwafanyia watu connection wakawa ma askari lakin sisi watoto wake hakuwahi kuthubutu, story ni ndefu mno nakupa tu summary sitaki kusema mali alizokua anamilik, sitaki kusema watoto wa nyumba ndogo ambao sio wake walivyokula mali zetu,
ni story ndefu naweza andika kitabu , mimi mungu alinitendea muujiza nimesomeshwa na mzungu , kutoka german, na kipind hiko baba bado yupo kazini na sikuwahi dhubutu kumwambia matatizo yangu yule mzungu, nilipewa kadi ya benk mpk leo ninayo nilikua nawekewa ada na pocket money kila mwezi suala la alinilipiaje lipiaje ni suala jingine, nimemaliza chuo mzee wangu hajui km nimesoma, nilikua na chuki sana moyoni na sikuweza kusamehe, nilikaa muda mlefu sana nna chuki moyoni namchukia sana mzee wangu,
siku moja moyo ukaniambia nitoe sadaka kwa baba yangu yule yule ninaye mchukia , haikua rahis ila nilipata pesa nikanunua nguo nzuri sana nikatuma mtu akapeleka maana mda huo tulikua hatukai nae alitufukuza sis na mama yetu,
baada ya sadaka hiyo mim ndo nilipata kazi, hebu fikiria nimemaliza kozi ya afya nimekaa home miaka miwili kila sehem nakosa kazi, had kujitolea nakosa na ni miak 7 iliopita sio leo....................................
Toa lawama zikija Mungu anaona. Ila usitelekeze wanao halafu ujitetee ni mama yao kasababisha. Ndo sababu Adam hakusamehewa bustanini. Hakuomba msamaha alilaumu, ni huyu mwanamke. Adhabu ilitoka Bado pamoja na kulaumu!Baba kukimbia nyumba haina maana katelekeza watoto.Japokuwa kama huko alikoenda ataishi na mwanamke mwingine, huyo aliyekimbiwa lazma ajae sumu na hiyo sumu lazima awatapikie watoto wake.
Hapo hataukiuza figo uwatunze as long as huish nao huyo mama ndo atakaye amua watoto wako wakuone nani kwao, baba, kinyago, mshenzi au mwenda wazimu.
Bro japo wanakera ila usitelekeze watoto. Fanya hata kama wataambiwa kivingine ila fanya. Kamwe usiwatelekeze, wakilala njaa wakilia Mungu anasikia.Kwakua wewe ni mtoto na hujui sababu ya baba yako kukimbia. Wewe sio lazima umpende ila cha kukusaidia usimchukie mtu usiyemjua.
siku ukija kufahamu ni mama yako ndio alimkimbiza kwa kumtamkia kuwa "hawa sio wanao" sijui utajisikiaje.
Ngoja na wewe uwe baba, halaf uyajue mazonge ya akina mama ndio utapata fursa ya kutafakar sawa sawa
Upo sahihi ndg lakini tunaweza kuwa na mahasibu tofaut juu ya baba zetu lakini Mimi nachomshauri ama asikie moyo wake unataka nini juu ya mzee wake!Bro sorry kwa hiyo mwanaume aliyeondoka akaacha kichanga Cha wiki mbili ni wa kuongea huruma? Alifikiri kichanga na watoto wake watakula nini? Hata uchukie vipI, hizo damu zako usiziachw na mateso. Mmekorofishana watu wawili, je hao watoto unaosema wanalishwa simu na mama yao angewatelekeza kama baba? Si wangekufa ukute mifupa? Acheni kuendekeza msemo wanawake wana kera wakati uliambiwa ishi nao kwa akili. Tafuta Chaka la kumuacha mwanamke ila kamwe usiache watoto wateseke uje kusema oh shida ni mama yenu, kwani alikulazimisha kuzaa?
Baada ya kufika hapo ulipo umefanya jitihada gani za kujikwamua kiuchumi? Au bado unaendelea na kazi ya kumchukia baba yako Hadi kufa. Inuka simama peke yako lawama na chuki kwa baba yako hazitakusaidia chochote.Wakuu,
Nimelelewa na mama yangu kwa asilimia 90 mpaka hapa nilipo
Baba yangu aliondoka nyumbani 2011 akamuacha mama yangu akiwa amejifungua wiki mbili akaenda kusikojulikana na mwanamke mwingine, akatuacha kakuna chakula wala matumizi yoyote ya mama na sisi wanafunzi, Ilibidi mama aanze vibarua ili tule na tusome mimi na dada yangu ninaemfuata.
Hata sisi tulipotoka shule ilibidi twende kwenye vibarua kwa ajiri ya chakula na madaftari, sabuni na matumizi mengine.qq
Nimepitia mateso makuu sana mpaka nimefka hapa nilipo kwa sababu ya baba yangu! Siku nyingine nitawaletea mkasa mzima ila kifupi namchukia mno baba yangu!
Mkuu hilo lisikupe tabu. Kuna watoto ambao wamspiganiwa na baba zao mpaka baba zao wakapata magonjwa ya moyo. Lakina walipojipata wamewachuka mama zao nakuwaacha baba zao wamalizwe na BP. Nawengine huwapigia cm na kuwatumia hela mama zao tuu!.Wanaojibu ni wanaume tupu, wanajipalilia kwao tu kana kwamba wao ni malaika, hivyo wanawake ndiyo wenye makosa, wanasahau wanayo wafanyia wake zao, sasa mkiwakimbia wake zenu na watoto, mama zao wakipambana nao na wakapata mafanikio msirudi tena kuomba msaada mkale mlikopeleka mboga.
Usimlalamikie huyu umzaniaye ni baba yako, usikute alishajuwa ukweli wewe si mtoto wake na ndiyo maana akasepa kutotaka kutunza mtoto wa mwanamme mwingine. Muulize mama yako baba yako halali ni nani, akiwa anakupenda kweli atakuambia tu.Wakuu,
Nimelelewa na mama yangu kwa asilimia 90 mpaka hapa nilipo
Baba yangu aliondoka nyumbani 2011 akamuacha mama yangu akiwa amejifungua wiki mbili akaenda kusikojulikana na mwanamke mwingine, akatuacha kakuna chakula wala matumizi yoyote ya mama na sisi wanafunzi, Ilibidi mama aanze vibarua ili tule na tusome mimi na dada yangu ninaemfuata.
Hata sisi tulipotoka shule ilibidi twende kwenye vibarua kwa ajiri ya chakula na madaftari, sabuni na matumizi mengine.qq
Nimepitia mateso makuu sana mpaka nimefka hapa nilipo kwa sababu ya baba yangu! Siku nyingine nitawaletea mkasa mzima ila kifupi namchukia mno baba yangu!
Siwezi jigarantee moja kwa moja.. naamin hivyo kwamba ndo baba angu! Maan sijawahi kuambiw mwingneUna uhakika ni babako?
Kataa ndoa inahusiana vip na kukimbia familia?Kataa Ndoa wanaokimbia familia hapa Hutawaona
We Nawe Lakini Basi.......Kwanza pole sana kiongozi, hii huwa inaumiza mno.
Nawaona watu wanajaribu ku-excuse tabia zisizofaa kwa kisingizio labda mama yako ndiyo alikua na shida.
Hata kama ingekua ni ukweli, kwani ukikorofishana na mkeo ndiyo unaacha kua baba na kujitoa kabisa kwenye kuhudumia watoto wako? Baba unawezaje kumtelekeza mama watoto wako na kichanga cha wiki mbili 😢 na watoto wengine saba.
Watu kama mzazi wako wapo wengi na ni mwiba sana kwenye jamii. Kaa naye mbali huyo mzee, ni mwanaume mwenye uwezo wa kuzalisha ila siyo baba!
Wale walioshindwa ndio waliokataa ndoa. Kushindwa ni kukimbiaKataa ndoa inahusiana vip na kukimbia familia?
Kwamba ukikataa mkataba wa ndoa ndio umekimbia ndio umekimbia familia yako?Wale walioshindwa ndio waliokataa ndoa. Kushindwa ni kukimbia
Wakuu,
Nimelelewa na mama yangu kwa asilimia 90 mpaka hapa nilipo.
Baba yangu aliondoka nyumbani 2011 akamuacha mama yangu akiwa amejifungua wiki mbili akaenda kusikojulikana na mwanamke mwingine, akatuacha hakuna chakula wala matumizi yoyote ya mama na sisi wanafunzi, Ilibidi mama aanze vibarua ili tule na tusome mimi na dada yangu ninaemfuata.
Hata sisi tulipotoka shule ilibidi twende kwenye vibarua kwa ajili ya chakula na madaftari, sabuni na matumizi mengine.
Nimepitia mateso makuu sana mpaka nimefika hapa nilipo kwa sababu ya baba yangu! Siku nyingine nitawaletea mkasa mzima ila kifupi namchukia mno baba yangu!
Kuna mtu aliwahi semaWakuu,
Nimelelewa na mama yangu kwa asilimia 90 mpaka hapa nilipo.
Baba yangu aliondoka nyumbani 2011 akamuacha mama yangu akiwa amejifungua wiki mbili akaenda kusikojulikana na mwanamke mwingine, akatuacha hakuna chakula wala matumizi yoyote ya mama na sisi wanafunzi, Ilibidi mama aanze vibarua ili tule na tusome mimi na dada yangu ninaemfuata.
Hata sisi tulipotoka shule ilibidi twende kwenye vibarua kwa ajili ya chakula na madaftari, sabuni na matumizi mengine.
Nimepitia mateso makuu sana mpaka nimefika hapa nilipo kwa sababu ya baba yangu! Siku nyingine nitawaletea mkasa mzima ila kifupi namchukia mno baba yangu!
Ndoa ni masuala ya mume na mke, watoto wote wanahitaji huduma na haki sawa.Kama Baba yako alikuwa hajamuoa Mama yako, alichokifanya ni sawa tu sababu watoto wa nje ya ndoa hawatakiwi kulalamika,
unachotakiwa kufanya ni kushukuru tu harakati za huyo mzee ukazaliwa basi, mengine yote keep constant