Nakuchukia Baba yangu

Yes, hii ndo win win situation, hujifungi gereza la chuki na pia hujitesi kuhangaika naye, mtoto wa nyoka ni nyoka, kama yeye hakutunza, asitegemee matunda asiyopanda
 
Pole sana ndugu. Lakini ili kufuta hilo tatizo kwenye familia na ukoo wako ni bora umsamehe na umpende haijalishi ni wapi amewapitisha maana usipofanya hivyo kwanza utaendelea kupitia maumivu ya moyo na pia utakuwa unaendeleza roho hiyo ya kutelekezana kwenye familia au ukoo wenu.
 

sasa kumchukia kwako kunakusaidia nini. Unauumiza moyo wako bure kwa kuuwekea matakataka, moyo wa mtu haukuumbwa ubebe chuki, Bali upendo.

so take care!
 
Bro japo wanakera ila usitelekeze watoto. Fanya hata kama wataambiwa kivingine ila fanya. Kamwe usiwatelekeze, wakilala njaa wakilia Mungu anasikia.
Sasa hata ukifanya wala mama yao hatawaeleza kama umefanya
 
Msamehe bure
Siwezi kumchukia baba yangu hata iweje ugomvi wake na mama wewe unakuhusu nini na pia wewe unajua madhaifu yao?siku zote kila mtu haoni tatizo alilonalo bali huona la mwenzie. ushapandikizwa baba yako mbaya nawe imekuingia akilini.
 
Siwezi kumchukia baba yangu hata iweje ugomvi wake na mama wewe unakuhusu nini na pia wewe unajua madhaifu yao?siku zote kila mtu haoni tatizo alilonalo bali huona la mwenzie. ushapandikizwa baba yako mbaya nawe imekuingia akilini.
Mh! sasa mkuu mbona komenti yako inanilenga mimi tena..? mimi sio mwenye mada watu mmevurugwa kumbe!
 
Sasa hata ukifanya wala mama yao hatawaeleza kama umefanya
Bro najua umetoka kupitia matatizo na mke wako ila kama una uhaka wale ni wanao nenda kalipe ada wakiwa wanaona, ile 150,000 mwekee mama yao kwenye account halafu waambie. Usikubali yeye awe ndio mtoa maneno kwa watoto. Ana custody ya watoto ila bado utakacholipa hakikisha wanajua. Wanunulie nguo wapelekee wapokee kutoka mikononi mwako mwenyewe.
 
Unamchukiaje baba yako na ungali hai?
Shukuru Mungu kwa hiyo pumzi unayoivuta, mengine mwachie Mungu.
 
Unamchukia vipi na hujasikiliza kesi ya upande wake!!??

Huenda ww sio mtoto wake vilevile labda maza ako alichepuka.

Huenda na yy anakuchukia vilevile
 
Hasa kama alidanganya hajazaa Imemkuta afandesele hii
 
mzee ulisha jaribu kumtafuta na kuongeanaye akudadambulie chanzo cha yeye kuondok maana kwa age23 ni umesha kua njemba kabisa
 
Ukiwa na wiki 2 ulijuaje kama aliondoka na. Mwanamke mwingine? We unaamini tu sumu alizokulisha mama yako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…