Wakuu,
Nimelelewa na mama yangu kwa asilimia 90 mpaka hapa nilipo
Baba yangu aliondoka nyumbani 2011 akamuacha mama yangu akiwa amejifungua wiki mbili akaenda kusikojulikana na mwanamke mwingine, akatuacha kakuna chakula wala matumizi yeyeto ya mama na sisi wanafunzi,
Ilibidi mama aanze vibarua ili tule na tusome mimi na dada yangu ninaemfuata.
Hata sisi tulipotoka shule ilibidi tuende kwenye vibarua kwa ajiri ya chakula na madaftari,sabuni na matumizi mengine,
Nimepitia mateso makuu sana mpaka nimefka hapa nilipo kwa sababu ya baba yangu! Siku nyingine nitawaletea mkasa mzima ila kifupi namchukia mno baba yangu!