Nakuchukia Baba yangu

Nakuchukia Baba yangu

Subiri na wewe uwe baba ndo utajua masahibu aliyokua anapitia baba yako!!!

Wanawake ni miongoni mwa viumbe hatari especially hawa single mingle mazazi
Na hapa ndipo kwenye point. Watoto wanaolelewa na mzazi mmoja, na hasa wa kike huwa wanamezeshwa sumu kali sana ya kuwaaminisha baba zao walikuwa ni watu wabaya! Na ndiyo maana waliwatelekeza na kwenda kuishi na wanawake wengine!

Wakati mwingine wanashindwa kutambua kumbe hao mama zao ndiyo chanzo cha kukimbiwa na waume zao, kutokana na kuendekeza kwao gubu na ujinga mwingine ndani ya nyumba.
 
M
Wakuu,
Nimelelewa na mama yangu kwa asilimia 90 mpaka hapa nilipo

Baba yangu aliondoka nyumbani 2011 akamuacha mama yangu akiwa amejifungua wiki mbili akaenda kusikojulikana na mwanamke mwingine, akatuacha kakuna chakula wala matumizi yoyote ya mama na sisi wanafunzi, Ilibidi mama aanze vibarua ili tule na tusome mimi na dada yangu ninaemfuata.

Hata sisi tulipotoka shule ilibidi twende kwenye vibarua kwa ajiri ya chakula na madaftari, sabuni na matumizi mengine.qq

Nimepitia mateso makuu sana mpaka nimefka hapa nilipo kwa sababu ya baba yangu! Siku nyingine nitawaletea mkasa mzima ila kifupi namchukia mno baba yangu!
Pole sana mkuu, maisha yetu sisi wanaume yana utata saana.Siwezi kukushauri lililojema zaid ya uwazacho. Lakin kama wewe ni mtoto wa kiume uangalie usije ukafanya mara mbili ya aliyofanya baba yako.

Binafsi ninawapenda sana watoto wangu lakin swala la kutmka its possible mission.

Sometimes kataa ndoa wako sawa. Maisha ya mwanaume yako karbu saana kifo, kulaumiwa na kukosea ili kupata amani.
 
Wanaume acheni kuwalaumu wanawake kuwa ndio sababu Mzee kakimbia. Tufanye ni kweli mama kasababisha Mzee akimbie, lakini je na hao watoto wamekosea nini?

Ukiachana na mke wako unawatupa na watoto wako? Mimi baba yangu na mama yangu waliachana nikiwa na miaka 6 tu lakini huniambii kitu kuhusu baba yangu. Ninampenda kupita kiasi kwa sababu hajanitupa alitekeleza majukumu yake kama baba japo aliachana na mama yangu na yeye alioa mwanamke mwingine.

Natamani kila mwanaume angekuwa kama baba yangu, nina hakika watoto wasingeteseka kwa kukosa mahitaji hata kama ndoa imevunjika.
 
H
Mtoa nyuzi amesema mzee alirudi na ameozesha watoto wake wa kike wa3 na kuchukua mahari. Kama kungekua na ishu ya kubambikiwa watoto iliyomfanya awatelekeze, je angerudi kwenye haya?
Huyo mshua yuko sober, nmeshuhudia mikasa kama hiyo kwenye familia za rafik zangu,wala hata hawakuchukua mahar za binti zao badala yake wanatoa baraka tuu ila sio kushiriki kwenye upokeaj pesa.
 
Mkuu mahusiano yana Mambo mengi we unaweza kumuona Baba yako ana roho mbaya kumbe amerogwa wanawake wabaya sana kwenye Mambo ya ndoa.
Sure ndo maana niliona Haina haja yakuweka Mambo moyoni
 
Wakuu,
Nimelelewa na mama yangu kwa asilimia 90 mpaka hapa nilipo

Baba yangu aliondoka nyumbani 2011 akamuacha mama yangu akiwa amejifungua wiki mbili akaenda kusikojulikana na mwanamke mwingine, akatuacha kakuna chakula wala matumizi yoyote ya mama na sisi wanafunzi, Ilibidi mama aanze vibarua ili tule na tusome mimi na dada yangu ninaemfuata.

Hata sisi tulipotoka shule ilibidi twende kwenye vibarua kwa ajiri ya chakula na madaftari, sabuni na matumizi mengine.qq

Nimepitia mateso makuu sana mpaka nimefka hapa nilipo kwa sababu ya baba yangu! Siku nyingine nitawaletea mkasa mzima ila kifupi namchukia mno baba yangu!
Hii story ya wewe kutusimulia habari za wakati una wiki 2 hauwezi kuwa ni zako, umesimuliwa na mama yako baada ya baba yako kumkimbia alipomfumania na mwanaume mwingine. Baba yako akajua wewe siyo mwanae akaona ajiondokee tuu.
Wanaume tuna mengi ya moyoni hatuwezi waambia watoto wetu ni aibu.
Kama una kifua mwambie baba yako akwambie kwanini alimkimbia mama yako ambae ni mwanamke akachukua mwanamke mwingine,
 
Ulitaka ukimchukia ndio atakufa.

Unamsamehe tu ila hapati kitu changu chochote........hii kubembelezana ni kulea ujinga.

Pesa zako unakula na mademu na pombe mimi za jasho langu uje kula bure tu? Huu ujinga mimi nilishaacha.

Sikufanyi kitu, wala sifatilii mambo yako ila changu cha jasho langu utakisikia kwenye redio. Maisha yanaendelea
Na yeye angekua mbinafsi akaamua kukojolea nje ungezaliwa?

Mwanaume kukimbia familia ni ngumu sana tena bila sababu ya msingi, ni bora angepata muda amsikilize mzee, hawa kina mama wanawalisha sana sumu watoto.
 
Subiri na wewe uwe baba ndo utajua masahibu aliyokua anapitia baba yako!!!
Kwa hiyo kupitia masahibu ndio kigezo au tiketi ya kutelekeza familia?

Kama huyo baba alijua kwamba hana uwezo wa kuhudumia familia, Kwa nini alizaa?

Kwa nini alileta watoto duniani?
Wanawake ni miongoni mwa viumbe hatari especially hawa single mingle mazazi
 
“Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.

— Kutoka 20:12 (Biblia Takatifu)
Baba au Mama mzembe, mjinga na mpumbavu hastahili heshima ya aina yeyote ile.
 
Bora umchukie mtu yeyote na sio baba baba hutoa baraka
Hakuna baraka kwa baba mzembe, mjinga na mpumbavu.

Ndio maana kina Baba Diamond wamebaki kulalamika tu.

Wanakula jeuri yao.

Ukisha telekeza familia, itelekeze mazima.

Sio usubiri mambo yamekuwa mazuri ndio urudi uanze kutia tia huruma kutaka msamaha.

Na kuanza kuja na kauli uchwara za baba hutoa baraka au laana.

Hakuna kitu kama hicho.
 
Na yeye angekua mbinafsi akaamua kukojolea nje ungezaliwa?
Kwani ilikuwa ni lazima kuzaliwa na yeye tu?

Hata angemwaga hizo sperm zake nje, Angeweza kuzaliwa na baba mwingine.
Mwanaume kukimbia familia ni ngumu sana tena bila sababu ya msingi, ni bora angepata muda amsikilize mzee, hawa kina mama wanawalisha sana sumu watoto.
Unasema mwanaume kukimbia familia ni ngumu sana, Wakati kuna kundi kubwa la wanaume walevi wametelekeza familia zao?

Nenda huko vijijini uone jinsi wanaume ni walevi na wake zao ndio wanapambana kulisha familia.
 
Hakuna msamaha kwa mzazi mzembe, mjinga na mpumbavu.

Huyo baba hastahili msamaha wa aina yeyote ile.
Mkuu unamisimamo mikali. Lakjn uposahihi coz kuna siku rafik yangu flan(me) tena mlokole aliwahi sema, at hivi kazi ya akina baba kwenye familia ni nin hasa?, akatoa sababu kibao ikiwemo wao wanatia mimba then akina mama ndo wanateseka nazo.
Alihitimisha kwa kusema haoni faida ya baba badala yake mama ndo kilakitu. Sina nilichomjibu, niliitikia tuu nikweli, coz mimi nimelelewa na Baba kwahyo niliona ntaanzisha ligi.
 
Wakuu,
Nimelelewa na mama yangu kwa asilimia 90 mpaka hapa nilipo

Baba yangu aliondoka nyumbani 2011 akamuacha mama yangu akiwa amejifungua wiki mbili akaenda kusikojulikana na mwanamke mwingine, akatuacha kakuna chakula wala matumizi yoyote ya mama na sisi wanafunzi, Ilibidi mama aanze vibarua ili tule na tusome mimi na dada yangu ninaemfuata.

Hata sisi tulipotoka shule ilibidi twende kwenye vibarua kwa ajiri ya chakula na madaftari, sabuni na matumizi mengine.qq

Nimepitia mateso makuu sana mpaka nimefka hapa nilipo kwa sababu ya baba yangu! Siku nyingine nitawaletea mkasa mzima ila kifupi namchukia mno baba yangu!
Mm ni mhanga tena bora ww , story yangu ni ndefu mno lakin nakupa tu kifupi baba alikua askari lakin sisi watoto wote hajatusomesha yaaan yeye ndo alikua kikwazo cha sisi kusoma, mimi kwa uwezo wake mungu nikasoma kati yetu watoto watatu , baba aliwafanyia watu connection wakawa ma askari lakin sisi watoto wake hakuwahi kuthubutu, story ni ndefu mno nakupa tu summary sitaki kusema mali alizokua anamilik, sitaki kusema watoto wa nyumba ndogo ambao sio wake walivyokula mali zetu,
ni story ndefu naweza andika kitabu , mimi mungu alinitendea muujiza nimesomeshwa na mzungu , kutoka german, na kipind hiko baba bado yupo kazini na sikuwahi dhubutu kumwambia matatizo yangu yule mzungu, nilipewa kadi ya benk mpk leo ninayo nilikua nawekewa ada na pocket money kila mwezi suala la alinilipiaje lipiaje ni suala jingine, nimemaliza chuo mzee wangu hajui km nimesoma, nilikua na chuki sana moyoni na sikuweza kusamehe, nilikaa muda mlefu sana nna chuki moyoni namchukia sana mzee wangu,
siku moja moyo ukaniambia nitoe sadaka kwa baba yangu yule yule ninaye mchukia , haikua rahis ila nilipata pesa nikanunua nguo nzuri sana nikatuma mtu akapeleka maana mda huo tulikua hatukai nae alitufukuza sis na mama yetu,
baada ya sadaka hiyo mim ndo nilipata kazi, hebu fikiria nimemaliza kozi ya afya nimekaa home miaka miwili kila sehem nakosa kazi, had kujitolea nakosa na ni miak 7 iliopita sio leo....................................
 
Mkuu unamisimamo mikali. Lakjn uposahihi coz kuna siku rafik yangu flan(me) tena mlokole aliwahi sema, at hivi kazi ya akina baba kwenye familia ni nin hasa?, akatoa sababu kibao ikiwemo wao wanatia mimba then akina mama ndo wanateseka nazo.
Alihitimisha kwa kusema haoni faida ya baba badala yake mama ndo kilakitu. Sina nilichomjibu, niliitikia tuu nikweli, coz mimi nimelelewa na Baba kwahyo niliona ntaanzisha ligi.
Baba au Mama anayezaa kisha anatelekeza watoto, Huyo hafai kabisa.

Na wala hastahili heshima ya aina yeyote ile.
 
Subiri na wewe uwe baba ndo utajua masahibu aliyokua anapitia baba yako!!!

Wanawake ni miongoni mwa viumbe hatari especially hawa single mingle mazazi
Pamoja na wanawake kuwa chanzo sa zingine, hawakusema kwenye vikao vyenu mtelekeze watoto, kwanini watoto wawe victims zaidi kwenye ugomvi wa baba na mama?
 
Back
Top Bottom