Nakuja Dar kusaka maisha! Treni ndio imeanza safari kutoka Kigoma kuja Dar, Mwenye kazi naomba tuwasiliane

Nakuja Dar kusaka maisha! Treni ndio imeanza safari kutoka Kigoma kuja Dar, Mwenye kazi naomba tuwasiliane

upo wapi saa hizi labda tunaweza kutana kwasababu na mimi nawahi kuja huko
Tumesimama hapa Tabora mkuu! Nasikia wanasema tunasubiri treni ya kutoka mpanda au mwanza.
 
Wewe ni muogo sana hivi unafikiri watu hatijawahi safir kwa tren?
Hiyo njia nzima ina network?
Au siku hizi mmefungiwa wifi?
 
Nina kuwa na wasi wasi huyu muhanga wa kutafuta kazi muda wote yupo online lkn pia nimtaalamu mzuri sana wa kujibu majibu mazuri
Wasi wasi wangu huyu jamaa hana elimu ya std 7
Pili huyu jamaa hatafuti kazi wala hayupo safarini kuja dar huwezi kuja dar pasina kujua unafikia wapi ilihaki umejikoki bando la kuperuzi njia nzima kwani kutoka kigoma mpaka tabora njia nzima kuna network?
Mwisho muhanga ametoa namba sasa wewe jifanye kumpigia hutajuta maishani mwako....kuna mtu,kuna mamba,kuna kinacho tafutwa humu......
Kaka nimesoma na avatar yako inatoa utambulisho wa jambo fulani.
Kuhusu Bando, Natumia freebasic!
Kuhusu mtandao,si kwamba kutoka kigoma mpaka hapa tabora njia nzima nilikuwa najibu chati za humu, hapana, ila nikipata muda na tukifika sehemu yenye mtandao, ndipo nazijibu komenti karibia zote! Shukrani mkuu!
Naamini umenielewa, na nikifika Dar, utakuwa msaada kwangu!
 
Wewe ni muogo sana hivi unafikiri watu hatijawahi safir kwa tren?
Hiyo njia nzima ina network?
Au siku hizi mmefungiwa wifi?
Mbona ni mambo madogo haya mkuu! Ni kama hapa Tabora stesheni tumefika saa kumi na moja Alfajiri, Sasa mkuu, tangia saa kumi na moja mpaka muda huu, nitakuwa nimewajibu watu wangapi humu? Ni lazima watakuwa wengi. Kwahiyo hoja yako Kuhusu mtandao njiani ina mapungufu ndugu!
 
Nifundishe ukiwa free basic una reply vipi comet?
Sehemu ya kwanza imeandikwa Like, unaiacha hiyo! Sehemu ya pili imeandikwa Reply, unabonyeza hapo.
 
Wakuu leo ni siku maalumu, nataka niuanze mwaka kwa mambo mapya! Hapa nipo ndani ya treni nakuja Dar! Na muda mfupi treni ndiyo imeanza safari,
Sina sehemu ya kuaminika ya kufikia, kwahiyo kama utakuwa na kazi, Tafadhali nisaidie, Na elimu yangu ni darasa la Saba 0744472252 Ni namba yangu.
Mpigie simu mbunge wako Zitto Kabwe
 
Back
Top Bottom