karibu sana kwenye hili jiji la joto
uswahilini chumba kimoja baba mama na watoto
si ulisikiaga mabomu ya gongolamboto
yalifanya rafiki yangu Adamu akafia ghetto
yaliacha kovu kubwa kama la mbagala
dar es salaama watu wengi tu hawanaga pa kulala
kama unataka mirungi twenzetu mitaa ya ilala
magomeni, na ujanja wangu wote niliitwa ----
watu wanaingiza pesa wakiwa ghetto wamelala.....
watu wengi toka waje hawajawahi kurudi kwao
sababu hawana nauli japo wamemiss ndugu zao
kuhusu kushinda na njaa hapa ndo zao
wauza sura wanaishi kwa kuuza madem zao
mama anauza bangi, baba amekata ringi anashinda
anacheza bao
wake zao wanazini kurisha watoto wao
vijana wao wanatembeza karanga, wanatembeza
maji, wanatembeza vocha siyo kwa mitaji yao
jioni wanakabidhi hesabu kwa bosi wao
hii ndo dar, ukipenda unaweza kuita bongo
machizi wakikosa hela ya bia wanakula gongo
siri haiwi siri uswahilini ukipata mchongo
wapangaji watakuandama bro mpaka utahama
(bongo)
ni majungu mixer wanga
utaenda tu kwa mganga utakapolala ghetto kwako
halafu ukamwagiwa mchanga..........karibu dar mkuu
Sent using
Jamii Forums mobile app