Nakuja Dar kusaka maisha! Treni ndio imeanza safari kutoka Kigoma kuja Dar, Mwenye kazi naomba tuwasiliane

Nakuja Dar kusaka maisha! Treni ndio imeanza safari kutoka Kigoma kuja Dar, Mwenye kazi naomba tuwasiliane

Mkuu pale ndio sehemu salama watampa ramani ya mji wapi pakupita, maana huu mji sio mzuri watu wanaweza kumpokea begi wakatokomea kusikojulikana!
Mkuu mbona unampoteza akaombe maelekezo police tena central mkuu mpe raman ingine hata kwa wakigoma wenzake najua lazma watakua na umoja wao

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
karibu sana kwenye hili jiji la joto
uswahilini chumba kimoja baba mama na watoto
si ulisikiaga mabomu ya gongolamboto
yalifanya rafiki yangu Adamu akafia ghetto
yaliacha kovu kubwa kama la mbagala
dar es salaama watu wengi tu hawanaga pa kulala
kama unataka mirungi twenzetu mitaa ya ilala
magomeni, na ujanja wangu wote niliitwa ----
watu wanaingiza pesa wakiwa ghetto wamelala.....
watu wengi toka waje hawajawahi kurudi kwao
sababu hawana nauli japo wamemiss ndugu zao
kuhusu kushinda na njaa hapa ndo zao
wauza sura wanaishi kwa kuuza madem zao
mama anauza bangi, baba amekata ringi anashinda
anacheza bao
wake zao wanazini kurisha watoto wao
vijana wao wanatembeza karanga, wanatembeza
maji, wanatembeza vocha siyo kwa mitaji yao
jioni wanakabidhi hesabu kwa bosi wao
hii ndo dar, ukipenda unaweza kuita bongo
machizi wakikosa hela ya bia wanakula gongo
siri haiwi siri uswahilini ukipata mchongo
wapangaji watakuandama bro mpaka utahama
(bongo)
ni majungu mixer wanga
utaenda tu kwa mganga utakapolala ghetto kwako
halafu ukamwagiwa mchanga..........karibu dar mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu ile safari yangu nadhani leo itafika mwisho, Kwahiyo nisaidieni wakuu, Mnisaidie japo kazi ili nipate hela ya kula.
Dakika kadhaa nyuma ndiyo tumeondoka hapa stesheni ya Morogoro, Asanteni!
Ninakushauri ukishuka Dar stesheni nunua chupa ya maji lita moja na nusu (usiyanywe), pini na kipande cha sponji ile ya kuoshea vyombo.
Ajira inaanzia hapa, toboa kizibo cha chupa yako kwa pini tundu nyingi kiasi, hapo stesheni kuna foleni kubwa ya magari muda huo uliofika janjaruka chagua gari safisha kioo cha mbele chapchap nenda kwenye dirisha la mwenye gari kinga mkono, ATM itafunguka ndululu zitamwagika, Dar es Salaam fomu VI (SIX), mjini shule.
Jioni uliza soko la Kariakoo liko wapi huko ndiko kwa mwenyeji wako nenda kalale usiwe na hofu hapo hapafungwi.
Karibu mgeni wetu jisikie uko mwisho wa reli kama Kigoma tu.
 
JE UNASUMBULIWA NA WADUDU KAMA KUNGUNI, MENDE, NZI, MBU.... wadudu wotee watambaao na Watusi.

KARIBU M.I FUMIGATION MSIMU HUU WA SIKUKUU
TUKUPULIZIE DAWA ZA KUUWA WADUDU MAJUMBANI, OFISINI, KWENYE BUSTANI, SHAMBANI NA MAZINGIRA MBALIMBALI KWA BEI PUNGUFU YA 20%. TUNATOA HUDUMA BORA, HUTOJUTIA DAIMA.

TUPO DSM-UBUNGO EXTERNAL
CALL : 0655166597, 0766006509.
KARIBU. TUKUFANYIE USAFI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom