Nakuja Dar kusaka maisha! Treni ndio imeanza safari kutoka Kigoma kuja Dar, Mwenye kazi naomba tuwasiliane

Mapambano yanaendelea vizuri,
Nilikuja sina pa kufikia wala mwenyeji (hili siyo jambo dogo),
Leo hii nimepanga chumba.
Ni hatua nimepiga mkuu ukilinganisha na kipindi kile.
Hongera Sana,Wewe Ni Mwanaume Jasiri.... Mwenyezi Mungu azidi kukufanyia wepesi
 
Hongera Sana,Wewe Ni Mwanaume Jasiri.... Mwenyezi Mungu azidi kukufanyia wepesi
Nashukuru sana mkuu, lakini hapo kwenye Mungu kwakweli mimi huwa napata ukakasi.
 
Nakuelewa.... Endelea kukuza Imani kuna siku yako itafika tu

Siku yangu?
Kupatwa na matatizo?
Ajali hata ulemavu, au kifo?
Hayo yanampata kila aliye hai.
Hayo hayaletwi wala kusababishwa na Mungu au Shetani.
Mazingira tunayoishi ndiyo hupelekea hayo kutokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…