Mwambie uyo Mkuu,
Me sikioni cha maana Dar, Nimezaliwa, Nimelelewa na Kusoma Dar lakini sioni kama ni mji unafaa kwa mtu anayejitambua eti kuukimbilia kutafuta maisha?
Dar ni watu wa hovyo kweli kuchafu sana ustaarabu hakuna...Mara mia niishi mkoani kwenye uhakika wa chakula bei chee mashamba kibao hewa safi maji matamu ya asili hakunaga kipindupindu mikoani.
Kama ni fursa umeziacha kigoma Mkuu,Inategemea una jicho la namna gani kuziona fursa hakika nakwambia ni afadhali ungetoka kigoma ukaenda singida au kyela mbeya utatoboa ila Dar hapana utaishia kuuza pipi barabarani.
Anyway Fungu lako lipo kwa Muumba huenda ukalipatia huko Dar. Kila la kheri Mkuu Muhimu umeweza kuthubutu.
Ni hatua Muhimu Maishani.