Nakumbuka Mitihani yetu ya Darasa la Saba ilikuwa inaanza ivi

Nakumbuka Mitihani yetu ya Darasa la Saba ilikuwa inaanza ivi

Umekosea kdogo. Mtiti ulikua unaanzia swali la 31. Babu unatamani waseme ishieni hapohapo ulipofikia
nakumbuka headteacher alikuwa anafundisha hesabu so akija kugawa karatasi za mtihani unacheki swali la kwanza hadi thelathini, utakayokosa ndio idadi ya fimbo zako kwa siku hiyo
 
Jibu hazitakutana kwa SBB ndege IPO hewani na land cruser IPO (chini) barabarani
 
Mkuu samahani Kama utakuwa female naomba niwe mwanafunzi wako kwa kweli sijawahi fundishwa hesabu na madam nasikia wanaeleweka Sana yamkini namimi ningekuwa kipanga wa hesabu ntafurahi Kama ombi langu litakubaliwa
Mkuu mi mkaka haaaaa
Mwite chilalila akupige msasa
 
HILO swali ni sawa na swali Tanzania ilipata Uhuru lini??
 
Juma ana miaka 3 zaidi ya Jafeti.Jumla ya miaka yao ni 19 Tofauti ta miaka yao ni 6.Je, Jafeti ana miaka mingapi.

Haya maswali ya umri yalinikera.

Si wangetoa tu swali hilohilo kwa njia hii,

Umri wa Juma= x
Umri wa Jafeti=y

3x+y=19
x-y=6.
Manenooooooo kibao nilikua niko interested na haya maswali lakini sikuwahi kupata jibu sahihi.
 
Umekosea kdogo. Mtiti ulikua unaanzia swali la 31. Babu unatamani waseme ishieni hapohapo ulipofikia
Labda haya maswali yao ya siku hizi ya kushade, lakini yale yenyewe chaaa balaa lilikuwa linaanzia swali la 31!! Unasoma mara kumi kumi unahisi upo central na bwana siro.
 
Labda haya maswali yao ya siku hizi ya kushade, lakini yale yenyewe chaaa balaa lilikuwa linaanzia swali la 31!! Unasoma mara kumi kumi unahisi upo central na bwana siro.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] na bwana cro
 
Kufaulu ni kufikia malengo uliyojiwekea kwenye maisha yako, hiyo ni principle moja muhimu sana ukitaka kufurahia maisha, kwa bahati nzuri nilijifunza toka utotoni, kwenye mtihani wa hesabu kufaulu kwangu ilikuwa kuepuka kupata 0 hayo mengine niliyokuwa nikipata ilikuwa ni kuvuka maleng kama vile TRA walivyokuwa wanazikusanya kodi😀
 
Hapo unafanya x ndio muda gari litakaotumia kukutana

gari litakuwa limesafiri kilomta 220x
ndege itauwa imesafisafiri kilomita 350(x+1), hiyo ni 1 sababu ya ndege iliwahi saa moja kabla ya gari

Kupata x ambayo ndio muda unatakiwa uzi equate hizo mbili, kwa kuwa jumla ya km ni 900, kilomita ilizosafiri gari lilipokutana na ndege itakuwa ni sawa na 900 utoe km ilizosafiri ndege

220x= 900-350(x+1)
Ukikokotoa utapata x ni 30/19 ya saa
ukitaka kuhakiki unatafuta kilomita ilizosafiri ndege baada ya 30/19 ya lisaa kisha unatafuta na km ilizosafiri gari baada ya 30/19 ya saa, hizo km za gari na ndege ukizijumlisha lazima zilete jibu la 900 kwa kuwa km zote zilikuwa covered.



Darasa la saba kulikuwa hakuna maswali magumu kama hayo, huo ni ukilaza wako unashindwa kutofautisha hata maswali ya la saba na sekondari
usifikili kila mmoja alikuwa na uwezo kama wako wa kusema primary kulikuwa hakuna maswali magumu.
Hapo mtoa mada hajazungumzia hayo maswali manne ya kwanza yeye kazungumzia ugumu wa maswali ya mafumbo kwa nilivyomuelewa mimi
au tuseme kwa kufupi unaanza na maswali simple then unaenda kwenye pasua kichwa
 
mwendokasi ulikuwepo ila simple sana, kutafuta muda huku umepewa umbali na mwendokasi, au kutafuta mwendokasi huku umepewa umbali na muda, walikuwa hawaya complicate kama la mtoa mada,
maswali ya mtoa mada ni la sekondari form 3

I'm not seeking forgiveness
hayo maswali yalikuwepo aisee usibishe bana .
 
Wengi tulikua tukipata 25/50...Daa kuna Vyombo vilikua matata sana hujaenda Maumbo,Mwendokasi,Mzingo,kipenyo,Tena anakwambia tumia pai kama 3.144,Hujaenda mlinganyo,Mkuu unajikuta unangaa sharubu tuu na kutumia bikari bila kujua hata unafanya nn
ilikuwa ni hatari hivi vitu aisee ukipata 30 /50 unaringa kinoma.
Dah haya mambo yalikuwa mazito, sasa usiombe kukutana na swali la umri, yaani ukisolve vibaya unaweza jikuta mjukuu ana miaka mingi kuliko bibi!
maswali kama ya umri yalikuwa ni moto wa kuotea mbali aisee
Naomba niingilie huu ubishi mkuu chinchilla coat na wadau wengine, hili ni swali la topic gani kwa anayesema ni la darasa la saba, na kwa anayesema ni la form 3.
secondary hakuna maswali ya hivyo.
 
kinematics before ilikuwa kwenye mathematics na physics ila baade ilifutwa ikaachwa kwenye physics mkuu.

Check records zako vizuri mkuu, miaka niliyosoma mimi Kinematics haikuwa kwenye hesabu O-Level, ila baada ya hizi arguments nikaangalia syllabus ya Math Form 3 nikaona Kinematics imo, na ni current syllabus.
 
Sure nimeiona, nimejaribu kutafuta syllabus ya miaka ya 2000 kushuka chini sijaiona, nadhani hapo kuna topic mpya ziliingizwa na baadhi kuondolewa.

All in All uko sahihi.

Hesabu za form three topic zake ni hizi hapa chini:-

1. Relations
2. Functions
3. Rate and Variation
4. Statistics
5. Kinematics
6. Sequence and Series
7. Circles
8. The Earth as a Sphere
hii kinematics umeitolea wapi kwasasa haipo ila before ilikuwepo tena kwenye mathematics halafu hapo ujaiweka topic ya account
 
Labda haya maswali yao ya siku hizi ya kushade, lakini yale yenyewe chaaa balaa lilikuwa linaanzia swali la 31!! Unasoma mara kumi kumi unahisi upo central na bwana siro.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Check records zako vizuri mkuu, miaka niliyosoma mimi Kinematics haikuwa kwenye hesabu O-Level, ila baada ya hizi arguments nikaangalia syllabus ya Math Form 3 nikaona Kinematics imo, na ni current syllabus.
hapana mkuu kinematics wamekwisha itoa kipindi kirefu tu au labda pengine nisibishe labda inaweza ikawa imeludishwa tena but ngoja niingie kwenye mafaili yao nicheki.
 
hapana mkuu kinematics wamekwisha itoa kipindi kirefu tu au labda pengine nisibishe labda inaweza ikawa imeludishwa tena but ngoja niingie kwenye mafaili yao nicheki.

Mkuu kwa tuliosoma O - level miaka ya 1994 - 2007 hiyo topic haikuwepo kwenye hesabu za form 3, baada ya huu ubishi nikaingia net kucheki curent syllabus nikaiona.

Itakuwa iliondolewa miaka hiyo niliyotaja na then ikarudishwa baada ya hapo.
 
Back
Top Bottom