Kama kinakutokea kwa siku 2 au 3 na kupotea, si tatizo. Kama kinakutokea na kinabaki muda mrefu hata miezi; ni ishara unapungukiwa na vitamin C mwilini, kama ni hivi:
1. Pata juisi ya ubuyu kikombe 1 asubuhi na 1 jioni (tengeneza mwenyewe, usiweke rangi rangi au takataka zingine tofauti na sukari na chumvi ya mawe punje 3 ktk kila kikombe).
2. Kila unapoenda kulala, lamba asali vijiko 2
3. Kila chakula unachokula ongeza kijiko 1 cha unga unga wa mti wa mlonge (kwenye sahani ya chakula)
4. Pata multivitamins nzuri, meza kidonge 1 kila umalizapo kula
5. Chungwa 1 kwa siku si vibaya.
Mhimu:
1. Kumbuka kunywa maji ya glasi 2 kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni. Kunywa tena maji glasi 1 kila masaa 2 baada ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni.
2. Epuka caffeina(chai ya rangi, kahawa, red blue, malta, cocacola, azam cola, sayona nyeusi) na soda au kinywaji chochote cha kiwandani.
3. Epuka tumbaku zote, fanya mazoezi na pata muda wa kupumzika siyo unasoma tu masaa yote kama mimi muda huu ni saa saba usiku nimetingwa nakuandikia hapa, ehe! ngoja nikalale.
Fanya kwa mwezi 1, mengine ni PM